CUF Mtaliwa wote, tafuteni suluhu! Shauri yenu!

CUF Mtaliwa wote, tafuteni suluhu! Shauri yenu!

Hayo majina yote 8 atapanga Lipumba. Hii game Lipumba kashawin na ataendelea kuwin

Sent using Jamii Forums mobile app
Shughuli ya Maalim Seif na akina Mtatiro inabidi akae nao wote maana hawawezi kuteua nje ya majina yaliyopendekezwa la sivyo lipumba na team yake watakaa nao na kuwashawishi wamuunge mkono ili wateuliwe na tume

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanajamvi salaam!

Kufuatia taarifa ya spika iliyotolewa leo ambayo inaeleza kwamba spika amejiridhisha kwamba wabunge nane waliokuwa wana muunga mkono Maalim Seif wamefukuzwa uanachama hivyo kukosa sifa za kuwa wabunge.

Kwa kuwa kazi imebaki kwa msajili na tume kujaza nafasi zilizo wazi.

Na kwa kuwa utaratibu wa kujaza nafasi husika unajulikana na unafanywa kwa tume kuteua miongoni mwa majina ambayo yalikwisha pendekezwa na chama kabla ya uchaguzi.

Na kwa kuwa Maalim Seif ndiye aliyependekeza hayo majina ambayo yapo tume ya uchaguzi.

Namshauri Maalim Seif awatafute wanachama wote ambao majina yao yalikwisha kupendekezwa tume ambao ndiyo watakuja kujaza nafasi zilizo wazi ili kuhakikisha anaongea nao na anapata uungwaji mkono la sivyo timu lipumba ikishawateka itazidi kuimarika zaidi na zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mnahangaika sana aisee tena na jambo ambalo lina waingizia gharama bila sababu
 
Kitakachokwenda kutokea ni propesa kukaa na baadhi ya wanawake ambao majina yao yapo tume ya uchaguzi na kuomba wamuunge mkono ili wateuliwe na baada ya makubaliano propesa anakwenda tume na kuomba awateue wale alioongea nao labda kuwe na ulazima wa kufuata wingi wa kura

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CUF acheni kutunishiana misuli, wenye hekima tushaona mnavyoenda mnaenda kubaya wote na sasa tunaona ipo haja ya kuwashauri kwa hekma ili muweze kunusurika.

Kimsingi kwa mtu yeyote ambaye ni mdau wa demokrasia, hawezi kufurahia kuona migogoro ndani ya vyama vya siasa ambayo inatishia kuviua vyama hivyo. Kwa mantiki hiyo, umefika muda sasa wa wadau wa demokrasia kuwasaidia CUF kupata suluhu ya mgogoro unaowakabili. Aidha, kwa kuwa CUF ni chama cha upinzani, vyama vingine vya upinzani vina jukumu la kuwasaidia CUF kufikia Suluhu kuliko mtu mwingine yeyote.

HATARI ILIYOPO KAMA MGOGORO HUU UTAENDELEA KAMA ULIVYO;
Ikiwa, mgogoro huu utaendelea kama ulivyo bila kusuluhishwa kwa njia za kidiplomasia, madhara ya fuatayo yanatarajiwa kujitokeza.
1. Kuzidi kwa chuki miongoni mwa wana CUF wenyewe kwa wenyewe hasa chuki kati ya wana CUF wa zanzbar/ pemba dhidi ya wale wa Bara.

2. Kuzidi kwa chuki ambayo haiwezi kuwa na faidia kwa yoyote kati ya Prof. Lipumba na Maalim.
3. Kwa upande mmoja CUF ya maalim Seif itakufa kwa kukosa uungwaji mkono wa kitaasisi na kisheria (kutokana na position ya mgogoro kwa sasa) na kwa upande mwingine CUF ya Lipumba itakufa vile vile kwa kukosa uungwaji mkono wa kutosha Zanzibar lakini pia kwa kukosa "Cause and Purpose" bara. CUF itapoteza wabunge wengi toka pande zote. Kwa hiyo wakiendelea hivi matokea yanatarajiwa kuwa "Zero sum game" kwa pande zote.

NINI CHA KUFANYA;
Kwa kuanzia,
1.Tunaziomba pande zote (Maalim na Prof. Lipumba) kwanza waache kutoleana kauli kali na za kuudhi ambazo zitaendelea kuleta uhasama.

2. Maalim aitishe vyombo vya habari akiwa pemba na kueleza wafuasi wake kuwa yuko tayari kufikia maridhiano na prof. Lipumba na Lipumba aitishe Press Dar akieleza utayari wake wa kufikia maridhiano na Maalim.

3. ACT (kwa sababu wanaweza kuaminika na pande zote), wawasaidie CUF kuwatafutia msuluhishi ambaye anaaminika na pande zote ambaye kwa haraka sana ataita wajumbe wa pande zote na kuanza hatua za maridhiano, kwa kuangalia uwezekano wa Lipumba kuendelea kuwa Mwenyekiti na Maalim kuwa Katibu kama ilivyokuwa awali.

MSULUHISHI
Napendekeza Msuluhishi awe ni Shekhe, Maalim Ally Basalleh wa dar es salaam. Hii ni kwa sababu kwa sasa kitu pekee kinachowaunganisha Lipumba na Seif ni dini, wote wanamfahamu vizuri Basalleh na wamekuwa wakiswali nyuma yake mara kwa mara. Aidha Shekhe basalleh ni msomi, mtu mzima, muelewa na mwenye busara kubwa sana.Naamini suluhu itafikiwa.

Nawatakieni suluhu njema.
Aamini.

Mungu amfanyie wepesi Maalim....apate kuona umuhimu wa suluhu.
 
Haya mambo ndio huwa yanazalisha ugaidi. Halafu ikifikia hali hiyo tunaanza kumtafuta mchawi
Shida sijui ni kwa nini baadhi ya watu wanakuwa wagumu sana kuelewa

usitembee juu ya ardhi kwa majivuno
 
Tatizo maalimu huwa ana msimamo mno,
hapa duniani inatakiwa kuwa flexible,
saa ingine unajifanya mjinga ili ufikie malengo,
rip Cuf
 
Mkuu huyu ni ZWAZWA asiyejitambua hata chembe mara aseme yeye ni Chadema mara yuko ACT mara karudi chama cha wahuni na mafisadi. Ali mradi hajitambui hata chembe.



Mkuu unaongea kama upo Kenya vile ,eti wapinzani hawaongei, spika akitajwa moto ,ukitaja Rais moto zaidi na kupewa kesi ya uchochezi.

Kwa mfano naomba uvae viatu vyao ungefanyaje? Chadema wameshaingilia mara nyingi wakazodolewa ,tena walitaka wakamtoe kabisa Lipumba Biguruni ,we mwenyewe shahidi kilichotekea .Kwa kifupi wabunge waongeaji wote chadema tayari wanakesi si chini ya 4 kila mtu.Labda Zitto na Mbatia wasio na kesi wabebe jukumu hilo
 
CUF wadisolve tu waangalie namna nyingine

agent kapiga kazi ya nguvu
 
Mkuu huyu ni ZWAZWA asiyejitambua hata chembe mara aseme yeye ni Chadema mara yuko ACT mara karudi chama cha wahuni na mafisadi. Ali mradi hajitambui hata chembe.

Muda ni mwalimu mzuri sana

usitembee juu ya ardhi kwa majivuno
 
Spika anakosa busara.

Lipumba hatambuliki kama Mwenyekiti wa CUF na kesi bado ipo mahakamani.

Upi uhalali wa Lipumba kupendekeza kuvuliwa ubunge wa wabunge wa CUF?
 
Ushauri mzuri.

Kwa upande wangu nashauri Maalim Seif ahamie chadema pamoja na wabunge wake , na chadema wamuachie Maalim seif chadema upande wa visiwani ambapo ataweka wagombea wake anaowataka yaani aliotoka nao cuf.Hii itazididha uimara wa chadema na upinzani kwa ujumla.

Hasara yake Cuf itakufa.Lakini hata Maalim asipohama bado cuf itakufa tu maana sioni Lipumba akilegeza kamba wakati huo Maalim kabanwa
Maalim Seif anapenda ukuu wa chama.
Mbowe anapenda ukuu wa chama.

Wote wanapenda kuwa signatories wa Ruzuku. Hapo patachimbika mkuu.

[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji126] [emoji126] [emoji126]
 
Spika anakosa busara.

Lipumba hatambuliki kama Mwenyekiti wa CUF na kesi bado ipo mahakamani.

Upi uhalali wa Lipumba kupendekeza kuvuliwa ubunge wa wabunge wa CUF?
Nyie endeleeni tu kutokuelewa hivyo hivyo eh!

usitembee juu ya ardhi kwa majivuno
 
Back
Top Bottom