CUF: Masikini hafilisiki na kichaa hachanganyikiwi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF: Masikini hafilisiki na kichaa hachanganyikiwi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MsandoAlberto, Feb 3, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  CUF ni wanafiki sana. sana.

  Unafiki wao unajionyesha wazi kwa jinsi walivyowasahaulifu na wepesi kujitetea ili mradi waonekane wao ndio wao. Wanajiaminisha kwamba CHADEMA wanawachukia au wanawaonea wivu.

  Wanasahau kwamba "Masikini hafilisiki" na "KICHAA HACHANGANYIKIWI"

  CUF wameumia sana CDM wamekataa kuingia kwenye mtego wao na CCM. Inaendelea kuwauma na kutuliza roho zao wameamua kuwarushia makombora CDM.

  Viongozi wa CUF wanajificha nyuma ya pazia jepesi la 'sauti ya wazanzibari'. Tunajua wazanzibari ni kina nani. Tunajua ni asilimia ngapi ya dini gani inaunda sauti ya wazanzibari. Hivyo kwa kujificha nyuma ya sauti hiyo CUF wanategemea CHADEMA wataumia kwa kuhukumiwa na baadhi ya watu wa dini fulani.

  CUF wanasahau kwamba kura zilizopigwa Zanzibar kuhusu serikali ya 'umoja' wa kitaifa haikuwa kwa aina yoyote inayofanana na kura iliyopigwa sudan kusema kwamba asilimia 99 wamekubali. Kuna waliopinga na bado wanapinga. Kwani hao sio wazanzibari??

  Kama kigezo ni vifo vya wanaCUF kuunda serikali wao na CCM peke yao na kusema kwamba vyama vingine havina wabunge je walivishirikisha hata kupata mawazo yao kuhusu umoja wao na CCM? waliwaeleza nii kwa nini kwao ni muhimu kuungana na CCM ilihali vyama vingine vitabaki nje ya serikali hiyo ya umoja wa kitaifa?

  CUF kama wangekuwa wamefanya hivyo basi wangewalaumu CDM kwa kutokuwaelewa. Hawakuwahi kuwashirikisha wengine kuhusu Zanzibar. Vikao vyote vilikuwa kati ya Katibu Mkuu wao na CCM!! Mbona hawakutaka kushirikiana katika hilo?

  Sasa wanaanza maneno, CDM wamelewa madaraka. Madaraka yapi? CDM ni wasaliti, wamemsaliti nani? Mbatia? Mrema? Lipumba?

  Turudi kwenye ukweliushirikiano wa wapinzani bungeni ni nini? Wanashirikiana ili iweje?

  Tukumbuke, CDM walitoka bungeni, hatuhitaji kujua ilikuwa ni sawa au si sawa lakini vyama vilivyobaki haraka haraka vilienda kukaa kwenye viti walivyotoka wabunge wa CDM. Baada ya hapo CCM wakashangilia.

  Huo ni unafiki. Ni lini CUF na hivyo vyama vingine waliomba msamaha au walielezea sababu za kuwadhalilisha CHADEMA ili wananchi waelewe?

  Hilo hawalioni badala yake wanataka ushirikiano kwenye bunge lile lile!! Ushirikiano kwa sababu wenye viti vyao wamerudi??

  CHADEMA hakuna kushirikiana na CUF na wanaofuta mpaka pale wote watakapokuwa wamejifunza kwamba ushirikiano ni wa vitendo na si wa maneno tu. Haiwezekani utake uwaziri kamili, uone hautoshi ung'ang'anie uwaziri kivuri. Kwani kushirikiana mpaka upewe cheo?

  Kwa nini basi kama ni muhimu kiasi hicho CUF na CDM wasiungane na kuwa chama kimoja?

  CUF na vyama vingine lazima waonyeshe kwa vitendo kuipinga serikali ya CCM. Wao wanakuja na approach "if you cant fight them join them'

  CHADEMA approach yake ni "if you cant fight them, fight them' sasa hiyo ni approach tofauti na ya CUF.

  Mwisho, tunataka tuone matunda ya muungano wa CUF na CCM zanzibar baada ya miaka mitano. Kama hali ya maisha ya wazanzibari itakuwa imebadilika CDM wataomba msamaha na watajirudi kwa kukataa kujiunga na CUF. Na CUF watafanya hivyo hivyo endapo hali itakuwa haijabadilika.

  Pia tutaona bunge linalokuja kwamba kutokuungana na CUF na vyama vingine kutakuwa na athari gani kwa taifa.

  Kwa sasa hivi msimamo wa CDM ni kwamba CUF na vyama vingine rafiki kwa CCM waendelee na urafiki wao. CDM itabaki chama kinachoipinga CCM kwa vitendo na kitaendelea kuchukua maamuzi magumu na yasiyowafurahisha CUF lakini ukweli utasimama.

  CDM haikuungana CCM Kigoma. CUF waache uongo na uzushi! CDM na CCM walikubaliana kuachiana madaraka baada ya kuwa wamefungana katika idadi ya wajumbe. Hiyo ilikuwa ni kwa faida ya watu wa kigoma. Sio kwamba CDM walishindwa basi wakapewa kipoozeo kama walivyofanyiwa CUF zanzibar.

  Narudia, masikini hawezi kufilisika, na kichaa hawezi kuchanganyikiwa!!:msela:
   
 2. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2011
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,868
  Trophy Points: 280
  Duh! mi title yako tu mkuu nimeipenda. Hope ujumbe wamepata, maana wapo wengi tu humu..)
   
 3. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Umeongea kila Kitu Msando, Umeweka Unafiki Pembeni umezungumza Ukweli ambao unawauma CUF
   
 4. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Albedo, hizo divesheni four na zero inakuwaje sasa? Mbona itakuwa balaa, 310,826!! Halafu ndio inakuwaje? Duh!
   
 5. Marunde

  Marunde JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2011
  Joined: Jun 9, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 60
  Naomba wananchi wafafanuliwe hili ili waelewe vizuri unafiki wa CUF,Ila mkuu title yako nimeikubali sana nimeicopy nitaipaste kwa wadu wote wanafiki kama CUF.
   
 6. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nimeweka kwa Kifupi kama Signature kwa sababu naamini itasomeka kwa Urahisi na inabeba Ujumbe Mpana sana, Labda watawala wetu tukiwawekea Mambo in Summary wata act
   
 7. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  CUF wala UROJO

  Yaheee sasa tuna sirikali ya umoja wa kitaifa yaheeee

  Tuendelee kula UROJOOOOO :msela: inshaalah
   
 8. Mtembea_peku

  Mtembea_peku Senior Member

  #8
  Feb 3, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umemaliza kila kitu ...message sent n delivered
   
 9. Mtembea_peku

  Mtembea_peku Senior Member

  #9
  Feb 3, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Kwa hiyo kwa mwaka 2010 Divisheni Four + Divisheni Zero Jumla yake ni 310,826 ====== 88.1%" Albedo Mwenyewe

  nimeipenda hii muno.
   
 10. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #10
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Albedo, kuna kila dalili kwamba ipo siku nchi itakuwa haikaliki. Vijana 310,826 ambao wamefeli wanaelekea wapi? hao waliofaulu tu hawana uhakika wa kuja kupata ajira acha ambao tayari wako mtaani na walifaulu lakini hawana ajira!!

  Vijana hao wakashawishiwa kuingia mataani hawatajiuliza mara mbili, itakuwa 'heri tukose wote'.


  Gradually class struggle will take speed, this is what is happening in Egypt! Class struggle! the Poor versus the Rich!

  Our leaders should see it coming! And it wont be very long!
   
 11. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #11
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Cobra, umenikumbusha mbali sana.....butua uwakomboe wenzako......

  Najaribu kutafakari ujumbe huo mzito! nakumbuka enzi za utoto mchezo wa kujificha!

  Now I can relate the lesson, its a sacrifice! Ukifanikiwa wenzako wamekombolewa, ukishindwa you and them have the same fate! But for the game to continue one has to sacrifice!!
   
 12. d

  dos santos JF-Expert Member

  #12
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 240
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  tatizo wagalatia walipenda kuona wazenj wakiuana ili wafanye mambo yao. Kuwa wamoja imewauma sana na wa kulaumiwa ni CUF,hakuna hoja ila chuki,wivu,ubaguzi,udini na uongo
   
 13. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #13
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Simply, one of the best articles on this unwanted vendettas by CUF against CDM.
   
 14. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #14
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Bw. Msando, kiswahili sanifu ni Maskini au Fukara?...... Pili, ni Mwendawazimu au Kichaa? au both! lol
   
 15. T

  Topical JF-Expert Member

  #15
  Feb 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Chadema endelee na uzi huo huo kila chama kinatakiwa ki-fight kivyake si kulazimishana kuungana ok

  CUF waache kulialia wanzashe organized movement kupata wanachama hata kushinda uchaguzi

  Wananchi tunafurahi kutengana kwenu ili tupate mawzo mengi kadiri inavyowezekana.
   
 16. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #16
  Feb 4, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Alberto, this is so powerful and succinct. Natumaini wale waliojiita "neutral" kwenye ile thread ya Julius Mtatiro jana watakuwa wameisoma analysis yako.

  thank you
   
 17. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #17
  Feb 4, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  ningekuwa mwanahabari ningechapisha hii. Au Alberto, kwanini usiitishe wanahabari na kutoa hii kama kauli yako?
   
 18. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #18
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Duh, Reagan hapo nadhani uko sahihi! Kiswahili changu ni kibovu! Fukara Hafilisiki na Mwendawazimu Hachanganyikiwi!

  Nashukuru kwa elimu kiongozi!
   
 19. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #19
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nashukuru Gurudumu, lalamiko kubwa la CDM ni tabia ya CUF kutumia vyombo vya habari kuwafikishia ujumbe CDM! Juzi wamejitetea wakasema 'mbona CDM tamko lao la Kamati Kuu limetolewa kwenye vyombo vya habari'. Nakuachia upembue kilichotumika kwenye kauli hiyo ni nini!
   
 20. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #20
  Feb 4, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Wagalatia!
   
Loading...