CUF: Masikini hafilisiki na kichaa hachanganyikiwi!

Bw. Msando, kiswahili sanifu ni Maskini au Fukara?...... Pili, ni Mwendawazimu au Kichaa? au both! lol

Fukara

Mimi nafikiri the way maneno yametumika ujumbe umefika na kwa wakati kama huu ambao muda wa ukombozi unakuwa mdogo zaidi ( kabla ya kusema sasa basi liwalo na liwe ) tusiangalie neno gani limetumika na ilimradi sio tusi it has no problem.

Shida ya watu ambao sio serious ni kuamisha watu katika flow nzuri ya fikra za kimaendeleo na kuwaingiza kwenye discussion yenye harufu ya kitaarabu flani.
 
Cuf wamejichakchua wenyewe, hata wakifungiwa kwenye chumba kimoja kwa siri, watasema wao sio wapinzania, Duuu.
 
Sanga, tunafanyaje kuhusu CUF? Bado tuna tatizo, wananchi wa kawaida hawaelewi CUF wanasimamia nini na kwa nini wanapingana na CDM!
 
Sasa comrade sisi wengine tuchangie nini? kama ingekuwa pambano la ngumi na mimi ndie kocha wa CUF natupa taulo ulingoni. NI KWELI KABISA MASKINI AFILISIKI na KICHAA HACHANGANYIKIWI.

Cha Msingi ndugu zetu CUF waelewe kuwa mshika mawili yote umponyoka (uwezi kuwa mtawala upande mmoja na mpinzani wa utawala upande wa pili) Katika siasa hakuna methali za mtumikie kafiri upate mradi wako. Katika ukomboozi tunapaswa kuwa na moyo kama wa hayati CHE GUEVARA aliamua kuja CONGO/ZAIRE kupigana vita ya ukombozi wakati yeye si MCONGOMAN aliikomboa CUBA awakati yeye si MCUBA na alifia mapambanoni CAMBODIA wakati yeye si MCAMBODIA kwake yeye ni ukombozi wa wanyonge ndio ilikuwa nia yake ya dhati moyoni na HADI LEO wanaharakati na wana mapinduzi wanamkumbuka hakuamini ktk dhana ya "if you cant fight them join them" na ndio maana hadi leo tuna MUONA NI MWANAMAPINDUZI WA KWELI . HKATIKA KUWANG'OA MADHALIMU NA MAFISADI UWEZI UKAENDESHWA NA KAULI MBIU YA "HATUWEZI KUWAACHIA SHAMBA NGURUWE WALIFAIDI PEKEYAO"
 
Kimsingi.........CUF wanatamani kuwa popo............. WAWE NDEGE NA VILE VILE WAWE WANANYONYESHA.
CUF wanasahahu yafuatayo..........
1. Wao miaka kadhaa iliyopita kanuni ziliwalazimisha kuungana .............. HIVYO KUUNGANA NA VYAMA VINGINE KUUNDA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI HAIKUWA KWA MAPENZI YAO KWA VYAMA VINGINE BALI KANUNI ZA BUNGE ZILIWALAZIMISHA kuanya hivyo. Hawakuwa na idadi ya wabunge wa kutosha kuwa na uwezo wa kuunda kambi ya upinzani wenyewe

2. CDM KANUNI ZINAWARUHUSU KUUNDA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI............ HIVYO HAWALAZIMISHWI KUUNGA NA YEYOTE katika kambi hiyo unless otherwise kanuni zibadilishwe.

3. CUF NI SEHEMU YA SERIKALI hivyo kujiunga na serikali ni kupoteza sifa za upinzani............. na mwisho wa siku kama wote mtajiunga na serikali YOU ARE BACK TO SQUARE ONE............ CHAMA KIMOJA
 
Tunawajua viongozi wao ni wabinafsi na wanafiki wakubwa wa upinzani Tanzania!, we kama si ubinafsi unawezaje kuongoza chama na kugombea uraisi kwa miaka zaidi ya 20 peke yako? Kama mtatiro ana kichwa kizuri na ni mpinzani wa ccm wa kweli anatakiwa ahamie cdm mapema!, shauri yake atanikumbuka! Au akamuulize Rwakatale alipotaka demokrasia ndani ya cuf viongozi walimfanyaje!
 
Duh, Reagan hapo nadhani uko sahihi! Kiswahili changu ni kibovu! Fukara Hafilisiki na Mwendawazimu Hachanganyikiwi!

Nashukuru kwa elimu kiongozi!
Nadhani hapa ni utofauti wa hali zao ndo unafanya jina kubadilika na tunaanza hivii;
Tofauti ya kipato ya huyu asijiweza hupangwa kuanzia yule aliyejuu kidogo ambapo tunaanza na;
1.MASIKINI.
2. FUKARA.
3. FAKIRI.

Na suala la Mwendawazimu sina uhakika sana japo najua kuna visawe vyake kama, KICHAA, PUNGUANI, MWEHU,
Na hapa tunaweza tusimhusishe moja kwa moja na Mwenye Mtindio wa Ubongo kwani upungufu mwingine ni wa kuzaliwa nao na mwingine ni kujitakia ( kutokana na matumizi ya madawa au viathiri ubongo)

Hivi ndivyo nilivyojaaliwa kuelewa juu ya dhana au mchanganua wa majina hayo.
 
tatizo wagalatia walipenda kuona wazenj wakiuana ili wafanye mambo yao. Kuwa wamoja imewauma sana na wa kulaumiwa ni CUF,hakuna hoja ila chuki,wivu,ubaguzi,udini na uongo

Dos Santos, ni sababu zipi zinakufanya uamini kwamba hao wagalatia walipenda wazanzibari wauane? Kwa nini ni furaha kwao?
 
Nadhani hapa ni utofauti wa hali zao ndo unafanya jina kubadilika na tunaanza hivii;
Tofauti ya kipato ya huyu asijiweza hupangwa kuanzia yule aliyejuu kidogo ambapo tunaanza na;
1.MASIKINI.
2. FUKARA.
3. FAKIRI.

Na suala la Mwendawazimu sina uhakika sana japo najua kuna visawe vyake kama, KICHAA, PUNGUANI, MWEHU,
Na hapa tunaweza tusimhusishe moja kwa moja na Mwenye Mtindio wa Ubongo kwani upungufu mwingine ni wa kuzaliwa nao na mwingine ni kujitakia ( kutokana na matumizi ya madawa au viathiri ubongo)

Hivi ndivyo nilivyojaaliwa kuelewa juu ya dhana au mchanganua wa majina hayo.

Swahilian, hili nalo neno! Sikuwahi kujua umasikini ni daraja! Kwa hiyo madaraja ni matatu? Masikini, fukara na fakiri! Je ni lipi daraja la chini kabisa? Yaani, lenye shida/taabu/matatizo/mahangaiko zaidi? Na kigezo au vigezo gani vinatumika kuwa na madaraja hayo?
 
Humu watu wanauelewa mkubwa hivyo hung'amua mambo magumu mepesi yanawapa shida , kama haujawahi kuwa tajiri basi ukiwa huna chochote ni kawaida watu hawawezi kusema umefilisika sanasana watasema leo afadhali ya jana ,
ukiwa kichaa unakuwa umepitia hatua zote za kuchanganyikiwa akili zikaenda mbele zikaruka ukawa kichaa kwa hiyo ukifanya makirikiri yako kukimbia au kupiga kelele hakuna atakayesema umechanganyikiwa saaana leo kimechachamaa .
Nadhani nimejaribu kuweka clear
 
Ni ukweli kusema kwamba CUF kuna kitu kinawaongoza na wala sio maslai ya Taifa kama wanavyotaka kila mtu aamini.Kwa macho ya haraka kuna ulevi mkubwa wa kutaka madaraka na hilo ndio Tatizo kubwa.

Historia japo ya karibu inasema kwamba CUF bunge la mwaka 1995-2000 waliunda kambi ya upinzani wenyewe huku wakishirikiana na wabunge tu 4 wa UDP ili wakidhi matakwa ya sheria/kanuni za bunge zinazosema kwamba kuunda kambi RASMI ya upinzani bungeni ni lazima Chama kifikishe asilimia 12 ya wabunge wote.Sasa CUF walipochanganya na 4 wa UDP wakafikia asilimia hiyo hivyo wakapata mamlaka ya kuunda kambi ya upizani bungeni.NCCR Mageuzi kipindi hicho ilikuwa na wabunge 28 wakiwemo mabere marando,James Mbatia,Masumbuko Lamwai na wabunge wengine vichwa kibao.NCCR hawakubwabwaja wala kujaribu kukusanya uongo,umbea na majungu ili kujiingiza kwenye haki ambayo sio ya kwao.Walielewa vizuri kanuni za bunge na wakajua kwamba kutoingia kwenye hiyo kambi rasmi ya upinzani bungeni hakuwanyimi haki yao ya msingi ya kuwawakilisha wananchi katika chombo hicho cha kutunga sheria.

Katika bunge la tisa pamoja na mambo mengine kulikuwa na suala la kubadili kanuni za bunge ama tuseme kuzifanyia marekebisho.Katika kamati ile alikuwamo Mh Hamad Rashi ambae na kwa sababu alikuwa na kinyongo cha kuangushwa na Mh John Cheyo katika uenyekiti wa kamati ya PAC sio tu alisema iitwe kambi ya upinzani bungeni bali neno RASMI liwepo ili kutofautisha KAMBI YA UPINZANI BUNGENI na KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI

Hivyo Hamad Rashid anaelewa vyema swala hili,sasa kwamba anajaribu kujifanya amesahau ni kawaida kwani bado ana hamu ya kuwa katika kamati za bunge.Na alisema neno rasmi liwekwe akiamini kwamba CUF watakuwa na wabunge wengi zaidi hasa ukizingatia tayari wana mtaji mkubwa wa kisiasa Zanzibar.

Hivyo ni sahihi kusema kwamba Hamad tayari alikuwa amejihakikishia nafasi ya kuwa kiongozi wa upinzani bungeni at least kwa vipindi vingine viwil au zaidi.Sasa kukosa nafasi hiyo kumemfanya atapetape ashike hoja hii na nyingine.Mwanzoni alisema hawezi kushirikiana na Chadema bila NCCR na UDP lakini baada ya kuona Spika hana muda wa kubadili kanuni za bunge ili kumfavour akahama akaanza kuwapigia magoti chadema japo wawashirikishe katika kamati za bunge.

Hamad na CUF wanatakiwa waelewe mambo muhimu yafuatayo

1) Kama Hamad alivyoshauri neno RASMI kutumika basi yeye limemrudia na sasa anaweza kuwa mwakilishi wa wananchi wake wa WAWI na taifa kwa ujumla ndani ya bunge bila kuwa katika Kambi RASMI ya upinzani bungeni.

2)Ni vizuri wakaelewa pia kwamba siasa za ujanja ujanja hazina tena tija kwenye Tanzania ya leo.

3) Ni vizuri wakaelewa kwamba CDM ni chama cha kidemocrasia kinapima na kupanga mikakati yake ndani ya vikao vya kichama.Wasitegemee wataingia katika mtego wa siasa maji taka kupitia vyombo vya habari.
 
Umesema vizuri Noel, CUF lazima waelewe kwamba wao na CDM ni entities mbili tofauti, suala la wote kuitwa vyama vya upinzani haliwanyi kufanana! Sisi wote ni watanzania lakini makabila, dini ni tofauti!

Ushirikiano si jambo la kuzungumzwa kwenye vyombo vya habari, halihitaji wanachama wote wa CDM na CUF kujadili! Linaanzia kwa viongozi! Kama viongozi wetu wangekuwa na utashi wa kutosha wangekaa wakazungumza wakaelezana yale yote ambayo wanayafikiria ni kikwazo na manufaa ya ushirikiano! Hakukuwa na haja ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari na kuonyesha kutofautiana kwao waziwazi kama kweli wote mbaya wao ni CCM! Kitendo hicho ni kuipa nguvu CCM, kuwachanganya wananchi na kujidhalilisha!
 
Back
Top Bottom