Elections 2015 CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima! Vinginevyo, huo ndio mwisho wake

Hilo kaulize nchi zilizoungana kama Uingereza, Marekani, Uchina na Taiwani, Ujerumani, AK n.k

Tazama facts zako vizuri

Uingereza juzi tu Wa Scotland wamepiga kura kuamua waendelee au wasiendelee na muungano
sio dhambi kule kusema muungano uvunjwe
na wala watu hawa api kuulinda kwa nguvu zote
muungano unajadilika na kupiga kura watu walipiga

Taiwan Rais mpya aliahidi uhuru kamili kutoka China na akapigiwa kura akashinda

na jifunze historia ya Checkslovakia Ethiopia na Eritrea pia
 
pasco

kimsingi upo sahihi, ila kunajambo moja ambalo naliona tatzo la zanziba si uchaguzi, wala cuf o ccm, ila kuna mambo ya utamadun na utawala, ndiyo maana viongozi wakuu wanasema watailinda na kuitetea katiba ya jmt,

sasa hoja ni kuwa kama cuf watatawala 99%muungano utavunjika, maana kuna elemit ya udin humo ndan kujiunga na mashirika ya kidin,

pili ki ulinzi tz haitakuwa salama, na zaidi kunauwezekano unguja na pemba zikameguka kila moja ikadai mamlaka kamili,

kwa hyo kinachofanyika ni kuulinda muungano kwa nguvu hata kama wananchi hawaupendi ili changamoto hzo ziendelee kutatuliwa taratibu,

nionavyo kwa sasa changamoto zilizopo ni rahisi zaidi kuliko ambazo zinaweza kuwepo baada ya zanzibar kuwa ktk utawala mwingine,

huo ndio ukweli kwa hyo wamependa kwenda kwenye uchaguzi au hawajapenda, mwisho wa siku rais ataamliwa na watawala, wananchi wanakwenda kupoga kula as simplicial,

duniani hakujawahi kuwa na haki kwa 100% huo ndo ukweli na cuf wanataka haki kwa 100%jambo ambalo litabaki kuwa ndoto tu..
 
Huwezi kushiriki uchaguzi
bila kujua mwenyekiti Wa
Tume ya uchaguzi bwana
Jecha atashauriwa nini
na mkewe kabla ya Matokeo kutangazwa.
Ukishiriki halafu akafuta tena uchaguzi kwa kuwa
wapiga kura hawakuvaa
Kanzu na walikuwa wame
nuna sijui utakubali mato
keo au utaanzisha vurugu

Dawa ni kutoshiriki kabi
saaa kama Biblia isema
mavyo "mwanangu usika
e Barazani mwa watu wen
nye mizaha.

Kule Barma viongozi Wa kijeshi wametawa kwa ma
mabavu na kumuweka kizuizini kiongozi Wa upinzani zaidi ya miaka
Ishirini lakini sasa wame
kubali kumkabidhi madaraka.

Hakuna marefu yasiyo
na ncha wahenga wame
sema.
 
Tazama facts zako vizuri

Uingereza juzi tu Wa Scotland wamepiga kura kuamua waendelee au wasiendelee na muungano
sio dhambi kule kusema muungano uvunjwe
na wala watu hawa api kuulinda kwa nguvu zote
muungano unajadilika na kupiga kura watu walipiga

Taiwan Rais mpya aliahidi uhuru kamili kutoka China na akapigiwa kura akashinda

na jifunze historia ya Checkslovakia Ethiopia na Eritrea pia

Tatizo lako unaamini sana Wazungu na sarakasi zao, Wazungu ni wasanii wakubwa klk unavyodhani hiyo kura za maoni Scotland ni usanii na ziliruhusiwa tu kwa sababu matokeo yalikuwa yanajulikana tayari na ili kudanganya watu kama ninyi ili muamini kwamba ni demokrasia ya kweli lkn hakuna chochote Ufalme wa Uingereza hauwezi kukubali kuipoteza Scotland hata siku moja na ndiyo maana hata kabla ya kura za maoni vitisho vilikuwa vingi sana kuanzia Waskotland kupoteza pensheni zao mpaka kufilisiwa kwa sababu Uingereza ingesitisha matumizi ya pauni mara moja, na sasa kura ya maoni nyingine itajadiliwa baada ya miaka 50 ijayo!
Yugoslavia ni ngumu sana na Muungano ulivunjika kwa sababu ya shinikizo ktk nje na siyo ndani, Marekani na nchi za Magharibi waliingilia kwa sababu wanazozijua wao wenyewe, hata AK Waafrikaans wanataka wa Jimbo lao la Orange au Orange Free state wanataka kujitenga na muda mrefu sana lkn siyo rahisi
kihivyo!
 
Uchaguzi wa marudio Zanzibar ni batili
Mkuu
hassanninga14 uongo ukisemwa sana na kurudiwa rudiwa bila kukanushwa unageuka kuwa ukweli!. Na ubatili ukiachwa kwa muda muda mrefu kuendelea kuwa ubatili, unageuka kuwa halali!.

Nakubaliana na wewe kuwa uchaguzi wa marudio wa Zanzibar ni batili kwa sababu uchaguzi halali uliishafanyika na mshindi halali kupatikana ila hakutangazwa, na badala yake uchaguzi ule ukafutwa kwa mtu batili, mwenye mamlaka batili na kwa kutumia sheria batili!.

Uzuri wa Zainzibar ni nchi inayofuata katiba kwa utawala wa sheria unaotumia sheria taratibu na kanuni!. Kama aliyetangaza kufutwa kwa uchaguzi alikuwa ni mtu batili na ametumia sheria batili, zipo sheria taratibu na kanuni za kuushughulikia ubatili huo!, lakini hakuna yoyote aliyechukua hatua yoyote kuuzuia ubatili ule!.Hivyo ubatili umeachwa hadi kugeuka halali!.

Sasa batil ile iliyofuta uchaguzi kwa ubatili na kupanga uchaguzi wa marudio batili, lakini matokeo ya uchaguzi huo batili yatakuwa ni matokeo halali, yatakayotangazwa na mamlaka halali kwa kutumia sheria, kanuni na taratibu halali, kwa kufuata ile kanuni ya the end justify the means, hata kama ni uchaguzi batili na rais akapatikana kwa ubatili, akiishatangazwa rasmi kuwa ndie rais, anakuwa ni rais halali, and nothing more Maalim, CUF or anyone can do kwa sababu the end will justify the means!.

Hivyo batili inatageuzwa kuwa halali na haramu kujipatia uhalali!.

Dawa ya batil ni kuitangaza kuwa ni batili, taasisi pekee yenye mamlaka ya kisheria kutangaza jambo fulani ni batili ni taasisi moja tuu, ambayo sio CUF, sio Maalim Seif, sio wanasheria, sio jumuiya ya kimataifa, bali ni mahakama kuu ya Zanzibar pekee!.

Kama hakuna yoyote aliyeitaka mahakama kuu ya Zanzibar kuutangaza ubatili wa Jecha, na sasa ameishatangaza tarehe ya uchaguzi wa marudio, kama hakuna yoyote atakayekwenda mahakamani kuupinga huo uchaguzi batili, siku ya siku ikifika watu watapiga kura katika uchaguzi batili na mshindi atapatikana katika ubatili huo huo, ila akiishatangwa tuu kuwa fulani ndio mshindi, huo sasa ndio unakuwa mwisho wa ubatili wote na mwanzo wa uhalali, kwa sababu kwa mujibu wa sheria zetu, rais akiishatangazwa kuwa ni rais, basi ndio mwisho wa mchezo, uchaguzi unakuwa umekwisha, kunakuwa hakuna tena mjadala!.

Kilichobakia ni heshima na adabu kuziheshumu mamlaka halali!, na iwapo kutajitokeza chokochoko ya aina yoyote, ya kutishia amani na utulivu wa Zanzibar, hapo ndipo vikosi vya polisi na JWTZ chini ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa JMT, Dr. John Pombe Magufuli, atakapowajibika kuingilia kati kuhakikisha uwemo wa amani na utulivu!.

Pasco
 
Pasco.

Zanzibar ni zaidi ya siasa kusema CUF itakufa Zanzibar kwa sababu ya kususia uchaguzi ni kujidanganya.

Mgogoro wa Zanzibar ni zaidi ya siasa wana matatizo yao makubwa ya kihistoria baina ya Unguja na Pemba.

CUF Zanzibar siyo kama Tadea au UDP refer kura za maruhani, CUF wanaweza kususia uchaguzi na CCM wakashinda kila kitu lakini huko kutakuwa ni kujiliwaza na kuhairisha tatizo ni suala la muda tu matatizo yatakuwa pale pale.

Jambo la msingi Zanzibar ni kuwaacha Wazanzibar wenyewe wahamue wanachotaka zaidi ya hapo mgogoro wa Zanzibar hauwezi kuisha huo ndiyo ukweli.

Ubaya na uzuri Zanzibar CUF ipo kwenye mioyo ya watu siyo kwenye makaratasi nawajua vizuri Wazanzibar kusema CUF itakufa huko ni kujidanganya mkuu wangu.
Naunga mkono hoja wazanzibar cuf kwao ni Zaidi ya chama cha siasa
 
Wanabodi, baada ya kutangazwa tarehe ya uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar, kuna watu wanadhani Chama cha Wananchi CUF, kina hiyari ya kushiriki uchaguzi huo au kutoshiriki, as if kushiriki uchaguzi wa marudio ni jambo la hiyari!, no way!, watakuwa wanajidanya!. CUF hakina option yoyote ya kuamua ama ishiriki ama isishiriki uchaguzi huo, kwa sababu ushiriki wa uchaguzi wa marudio sio suala la option bali ni jambo la lazima, watake wasitake ni lazima washiriki, kwa sababu kila kitu kiko vile vile kama mwanzo!, nikimaanisha hata wakisusa, picha na majina ya wagombea wao yatakuwepo kwenye karatasi za kura!.

Wenye option ya kuamua kushiriki au kutoshiriki uchaguzi huo ni wapiga kura, ndio wanaweza kuamua ama kujitokeza kushiriki kupiga kura, au kususa kupiga kura kwa kutokujitokeza, na mgombea hata kama atapata kura moja ya ndio, ndio atatangazwa mshindi!, hivyo kupiga kura au kutopiga kura ndio bado ni option!, lakini kushiriki uchaguzi huo sio option ni jambo la lazima!.

Iwapo CUF itatangaza kususia uchaguzi huo, tangazo hilo ndilo litakuwa tangazo rasmi la kifo rasmi cha kilichokuwa kinaitwa Chama cha Wananchi CUF, kwa sababu, ngome kuu ya CUF ni Pemba, kususia uchaguzi ni kuipoteza Pemba ambapo na ngome kuu ikiishakuangua, it is just a matter of time, chama chenyewe chote kielekee kaburini!.

Hata kama CUF watatangaza kususa, majina ya wagombea wa CUF tayari yako kwenye karatasi za kura katika uchaguzi huo, hivyo wakitangaza kususa, maana ni wagombea wa CUF hawatachaguliwa, hivyo kuipatia CCM ushindi wa mezani, ikiwemo kuitwaa ngome ya CUF kule Pemba na kuivunja uti wake wa mgongo, kwa CCM kuvitwaa viti vyote vya Uwakilishi Zanzibar na Pemba, ambapo pia huo ndio utakuwa mwisho wa SUK na CCM kutawala peke yake na kuhitimishwa kwa kifo rasmi cha chama cha wananachi, CUF!.

Nakiri kupandisha uzi huu kufuatia bandiko la mwana jf huyu

Hoja katika badhiko hilo mi kitisho cha CUF kuwa kisiposhiriki, hali ya amani na utulivu wa visiwa vya Zanzibar, utakuwa mashakani!. Maadam Zanzibarr sio nchi bali ni sehemu ya JMT, dhima ya muungano, ni undungu wa asili kati ya watu wa Tanganyika na watu wa Zanzibar, lakini sababu halisi ya muungano ni kuipatia Zanzibar ulinzi na usalama, Zanzibar haina polisi wala jeshi, hivyo jukumu la ulinzi na usalama wa Zanzibar, sio jukumu la Zanzibar tuu, bali ni jukumu la JMT, haiwezekani sehemu moja ya JMT iwe katika hali tete, wakati JMT ni nchi moja, ulinzi na usalama wa JMT utakuwa mikononi mwa JMT!.

Hivyo CUF washiriki uchaguzi huu wa marudio, au wasishiriki kwa kuususia, it will not make any difference kwenye amani na utulivu wa Zanzibar kwa sababu jukumu la ulinzi na usalama wa Zanzibar, sio jukumu la Wanzanzibari wenyewe pekee, bali pia ni jukumu la serikali ya JMT, chini ya Amiri Jeshi Mkuu, Dr. Joh Pombe Magufuli!.

Zanzibar kama sehemu ya JMT, inayo assuarance ya Amri Jeshi Mkuu wa JMT, kuhakikisha kuwa Uchaguzi wa marudio wa Zanzibar, uliotangazwa, utafanyika kwa uhuru, amani, usalama na utulivu, mshindi atapatikana kwa haki, atatangazwa, ataapishwa na kuunda serikali nyingine ya Zanzibar yenye jina la SUK lakini wawakilishi wa CUF kuendelea kuitawala Zanzibar kwa uhuru na amani kabisa bila`wasiwasi wowote kwa ile falsafa ya kule ya Mapinduzi Daima!.

Demokasia ya kweli ni serikali ya watu, inayoongozwa na watu kwa manufaa ya watu hao!, (of the people, by the people, and for the people), ila demokasia hiyo haikuwe kiwango cha asilimia ya watu hao!, hivyo hata kama nchi ina watu milioni moja, serikali ikachaguliwa na watu 10 tuu, bado serikali hiyo itakuwa ni serikali halali kisheria, japo itakosa peoples legitimacy, kwa watu hao ndio watakuwa wametumia haki yao ya kidemokrasia kwa kutokupiga kura!.

Kushiriki uchaguzi wowote, kwa kugombea nafasi yoyote ni hiyari, pia kuamua kutokushiriki katika uchaguzi pia ni hiyari, sambamba na kujiandikisha kupiga kura ni hiyari, kutokujiandikisha pia ni hiyari, na kujiandikisha kupiga kura na kisha kuamua kutokupiga kura pia ni hiyari, zote hizo ni demokrasia.Kama CUF itawashawishi wafuasi wake kususia uchaguzi huo, hiyo itakuwa ndio demokrasia yao!.

Kitendo cha CUF kushiriki uchaguzi wa mwanzo kunaifanya CUF ni lazima ishiriki uchaguzi wa marudio sio kwa hiyari ua kwa kupenda, bali ipende, isipende, ni lazima ishiriki uchaguzi huo!.

Hapa hakuna suala la choice. Na iwapo CUF watasusa kushiriki uchaguzi huo wa marudio, kususa huko kutakuwa ni kususa batili kwa sabu picha na majina ya wagombea wa CUF yataendelea kuwepo kwenye karatasi za kura!, hivyo kususa huko ndiko kutakao ipatia CCM ushindi wa mezani, tena this time CCM itashinda viti vyote vya uwakilishi Unguja na Pemba, na huu ndio utakuwa mwisho rasmi wa CUF. Kamwe CUF isikubali kuingia katika mtego wa kususia uchaguzi wa marudio!.

Turufu ya CUF kutishia kususa ni kwa kisingizio cha itabembelezwa ili kusitokea machafuko Zanzibar!. Kiukweli JK alikuwa ni mpole sana, hivyo Zanzibar imemchezea sana hadi kumtia vidole machoni katika yale mabadiliko batili ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010.

Kwa sasa Amiri Jeshi Mkuu ni Dr. John Pombe Magufuli, hii ni namba nyingine, huyu sio mtu wa mchezo mchezo au kuchezewa kama JK, hivyo CUF kama wanadhani watasusa na kubembelezwa, ili kuepusha machafuko Zanzibar, nawahakikishia this time watakuwa wame bugi step, hata wakisusa, hakutakuwa na vujo wala ,achafuko yoyote Zanzibar kwa sababu sasa ni zamu ya hapa hapa ni kazi tuu!.

Wanzanzibar, na Watanzania wote, chini ya Amiri Jeshi Mkuu, wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya JMT, tuna jukumu kubwa la kuilinda amani na utulivu wa eneo lote la JMT, ikiwemo Zanzibar, kwa gharama yoyote!, hii ikiwa ni pamoja na kuulinda muungano kwa gharama yoyote!.
Wasalaam
Pasco
Pasco kumbe mnafiki kiasi hiki!!! Hivi Luna haja gani ya cuf kuendelea kuwepo wakati mshindi ni lazima atoke ccm? Muda mwingine jitahi
 
W

Kama wamezoea JK zamu hii kwa JPM wamekanyaga waya wa HT
 
Umetumwa au?kwanza umeandika kama ni mtoto wa chekechea hata hujui kupitia maandishi na kufanyia editing kama ni posho utapata tu,nenda taratibu watu tusome tukuelewe
Pasco Leo kasema yote!hajamung'unya maneno!huo aliosema ndio kweli yenyewe!hakuna mzaha wala kubembelezana!
 
Pasco Maskiniii
Kutoshiri uchaguzi kwa CUF kinadharia inaweza onekana ni mwisho wa CUF. Lakini kwa siasa za Zanzibar zilipofika wana haja ya kutathmin nini wana kitaka. Je waridhie kushiriki chaguzi huku wakijua kuwa kamwe hawawezi shinda?
Yaani wao objective yao iwe ni ving'ora tu na kuishia kupewa nafasi za wizara nyepesi kwenye SUK huku washindani wao wakinawwir kwenye hatamu za uongozi?
Kwa wapenda demokrasia wote siasa zinazoendelea Zanzibar zikitiliwa mkazo na maneno ya kihafidhina ya kina marehemu bi Asha Bakari ya CCM hawawezi kuachia nchi kwa karatasi ni msiba mkubwa.
Mimi nadhhani CUF wana option muhimu katika kubadilisha hali hii..waridhie hali iliyopo na kisha waendeleze Ubwege wa kulalamika kama walivyoitwa hapo awwal...au wajipange upya kwa kuendelea kususia uchaguzi ili warudishe misingi imara ya demokrasia kuwa mshindi ndio atawale?
Kwa maoni yangu hii ndio option bora zaidi. Lazima status quo iliyokuwepo ambayo ni hatari zaidi ikomeshwe..na hapa hakuna haja ya kuangalia vyeo kwenye SUK ambayo kumbe formula yake iko pre-defined.
Maalim una kazi kubwa..lakini hili si la CUF peke yao..ni la wote wenye kuamini kwenye misingi ya demokrasia.
Mkuu Kikwebo, asante kwa mchango wako, nimeipenda objectivity na kuheshimu mchango wako!.

Pasco
 
kukosa legitimacy ni ishu nzito sana kwenye uongozi wa siasa.

CUF hawana haja ya kushiriki kwenye uchaguzi ambao imepangwa CCM Itashinda...by hooks and crooks
 
Naiona nchi ya Pemba ikianza kudai Uhuru wake kutokana na hizbu iliyoasisiwa na CCM.

Hawa wazee waliotawala miaka nenda rudi wanaitakia nini hii nchi kwa vizazi vijavyo?
Kila mara nawaza lkn sipati jibu, binadamu wa Leo si yule wa kipindi chao walipopewa vyeo vya mdomo.
Mambo yamebadilika na yanabailika haraka sana kila kukicha.

Wazee wa CCM pumzikeniii.

Ni hasara kubwa sana kukaa na mtu mjinga.
 
Hivi pasco hao wawakilishi wa ccm kutoka Pemba watafanya kubwa gani hadi wabunge wa cuf kutoka Pemba na unguja wakafunikwa na kupotea na cuf yao? Labda kama cuf isingekuwa na mbunge hata mmoja
 
Mkuu Pasco umeongea mengi kwa mtazamo wako unawashauri CUF wasisue uchaguzi kwa sababu ulizozieleza. Nadhani unasahau.kitu cha.msingi sana kuwa hata wakirushiri na kushinda hawata tangazwa washindi milele!

Je unaona ni busara kwa chama hicho cha upinzani visiwani zanzibar kuingia katika mchezo ambao wanajua hata wavue nguo hawawezi kutangazwa washindi hata kama wameshinda eti kwa kuwa serikali iliyopo madarakani ni ya kimapinduzi kwa hiyo haiwezi kuachia nchi kwa sanduku la kura?

Kama CUF itakufa si ndio sawa watawala wanataka?! Nitawaona wendawazimu kama chama hicho cha upinzani kushiriki ktk uchaguzi wa marudio.
 
Pasco, naomba kupingana nawe. Chama chochote kina option ya kujitoa kwenye ugombea wa nafasi fulani. CUF wanaweza kuiandikia tume na kujitoa kwenye uchaguzi. Pia,SUK inaundwa na mshindi wa kwanza na wa pili, CUF wasipokuwepo kuna chama kitakachofuatia kwa kura, hata kama kwa kura kumi. Kuvunjwa kwa ngome ya CUF pemba hiyo ni ndoto,kutokuwepo kwenye uchaguzi hakutaondoa harakati za kisiasa za CUF Zanzibar,wataendelea! 2005-2010,wawakilishi wa CUF walisusia Vikao vyote vya BW, haikuwafuta kwenye ramani ya siasa, and it was the same as if they had not participated in the election. Leo wamemtimua aliyekuwa mgombea kupitia ADC, Hamad Rashid, je! Ataebdelea kuwa mgombea?
Mkuu
LENDEYSON, kwanza asante kuchangia uzi wangu huu, pili kupigana kwa hoja ndio spirit ya mijadala yote healthy. Chaguzi zote zinaendeshwa kwa kufuata taratibu sheria na kanuni, na kuna muda maalum ambapo mgombea anaweza kujitoa rasmi, muda huo ukipita jina lake likiishachapishwa kwenye karatasi ya kura, hawezi tena kujitoa rasmi!, anachoweza kufanya ni kujitoa kwa kujifurahisha tuu, kwa kuwaomba wafuasi wake au wasimchague au kura zake wampigie mgombea fulani.

Marudio ya uchaguzi wa Zanzibar, yanatawaliwa na kitu kinachoitwa "the same status quo as 24th October, 2015 saa 12:00 jioni", hivyo hakuna ruhusa kubadilisha chochote!, unless litokee jambo linaloitwa " force majeure" kama kifo cha mgombea, uchaguzi utaahirishwa kwa jimbo husika!.

Uundwaji wa SUK nao una masheti yake!, kwanza lazima chama kiwe na zaidi ya asilimia 10% ya kura zote za urais, na pili lazima chama hicho kiwe na wawakilishi katika BLW, kwa siasa za Zanzibar zilivyo, CUF kikijitoa, hakuna cha`ma kingine chochote kinachoweza kupata asilimia 10% na CUF ikijitoa hakuna chama kingine chochote kinachoweza kupata hata mwakilishi mmoja zaidi ya CCM, hivyo sasa huu ndio utakuwa mwisho wa SUK!.

Hata kama ADC wamentimua Hamad Rashid, the status quo ya uchaguzi wa marudio ni as saa 12;00 jioni 24/10/2015 hivyo nothing changes!, hafukuziki!.

Pasco
 
Njaa ni kitu hatari sana ! yaani pasco unajidhalilisha kwa kiwango hiki ! kwa bei gani uliyolipwa ? huwezi kufuta cuf kwa kusimika wabunge wa uongo pemba , yalitokea haya siku za nyuma .
pasco huyu mganga njaa ndio wa kumtisha naye humu ? Nimekudharau sana .
Umetumwa au?kwanza umeandika kama ni mtoto wa chekechea kama ni posho utapata tu,nenda taratibu watu tusome tukuelewe
Hiyo ni njaa mkuu inasumbua hadi mtu anaamua kujiondoa ufahamu wake aliojaliwa kuwa nao
Mkuu ni kweli nami nashindwa kujua huyu jamaa kwanini ameamua kujivunjia heshima kiasi hiki,ni mjinga na lofa tu atakaye muunga mkono pasco kwenye huu uzi wake wa kijinga kabisa
Wakuu
Erythrocyte, na Mmawia, hili la uganga njaa ni kweli, kwa sababu baada ya kufukuzwa kazi TBC ile 2002, tangu wakati ule mpaka leo, ni miaka 14 sijabahatika tena kupata kazi popote, hivyo mpaka sasa ninapoandika hapa, mimi ni jobless sina ajira na maisha yangu ni ya kubahatisha bahatisha tuu kwa kuganga njaa!.

Hata hapa nilivyopandisha uzi huu, ni njaa tuu, nimelipwa zile buku 7 za Lumumba ili angalau mkono uende kinywani na siku yangu ipite!. Mkisikia kuna mahali popote wanahitaji waandishi wa habari, mnistue, hata kama ni gazeti la Kiu au Ijumaa nijulisheni tuu!.

Hakuna mtu yoyote aliyesema anataka kuifuta CUF, nilichosema ni iwapo CUF watasusia uchaguzi huu wa marudio, wakombea wa CUF wataendelea kuwemo kwenye kaatasi za uchaguzi, siku ya uchaguzi ni wana CCM tuu ndio watajitokeza kuichagua CCM ambapo itavitwaa viti vyote vya Zanzibar na Pemba, hivyo sio kuwa CUF itafutwa bali itajifia yenyewe natural death!.

Hizi kauli za matishio ya amani, hakutakalika, kumwagika kwa damu etc, vikosi vya Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama, yako imara kulisimamia hili!.

Pasco
 
Back
Top Bottom