Nimetazama hata list ya wanachama wa UN nimekuta haya kuhusiana na Tanzania:-
Tanganyika was a Member of the United Nations from 14 December 1961 and Zanzibar was a Member from 16 December 1963.
Following the ratification on 26 April 1964 of Articles of Union between Tanganyika and Zanzibar, the United Republic of Tanganyika and Zanzibar continued as a single Member, changing its name to the United Republic of Tanzania on 1 November 1964...
Kwa hiyo hata UN wana mwanachama mmoja tu! .
Hapo ulipopigia mstari ndipo kinaonekana kipo kizuizi fulani ...zimeendelea kama ni single member kwa mtazamo huo unaweza kusema nchi moja tu kati ya hizo ikipeleka maombi kuwa sasa basi kila mmoja kivyake vyake tumechoshwa na matatizo yanayotokana na kuendelea kama nchi moja,wandugu hakuhitaji kura ya maoni wala maono hapo, ni kazi ya UN kutengua au kutegua mstari tu pamoja na kutangazia katika Baraza la UN kuwa kumewakilishwa hoja hii na upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ,yeyote mwenye pingamizi alete mbele hoja yake .
Tatizo nchi iliyopo na inayojulikana ndani ya Tanzania ni Zanzibar ,Tanganyika haipo ,hivyo kama Zanzibar wakiamua kupeleka ombi hilo mbele basi hakutakuwa na msemaji wa Tanganyika ambae ataweza kuisemea au kuitetea ,ndio ikasemwa machogo wameshikwa pabaya ,ndio mkasikia Muungwana akisema itumike busara ,anajua fika kuwa suala hili likifika UN halitachukua hata wiki ,ndio itakuwa mwisho wa Muungano na Tanganyika itabidi waanze kulana nyama kila mmoja anataka kuwa Raisi mpya wa Tanganyika na waziri mpya waTanganyika.
Hili ni jambo la kuvutia sana ,WaZanzibari wanaonekana kuishika amani ya Tanganyika mikononi mwao japo hilo watanganyika vichwa mchungu hawalioni mbali na usomi wao, hatari iliyopo sio kwa WaZanzibari ambao akili zao zimeshaona mengi tofauti na WaTanganyika ambao bado damu za kikabila zinachemka ,mapigano mangapi yamezuka ndani ya Tanzania ,ardhi na mifugo ,madini na kadhalika ,hilo WaTanganyika wanalifumbia macho lakini ukichunguza ni kiini cha mapambano ya ndani ya nchi katika nchi nyengine ,ukiweka mbali mambo ya siasa na uchu wa madaraka ,kama wengi wa MaCCM wanavyoitupia Zanzibar suala hilo.
Leo hii Zanzibar ikiamua kwenda huko UN ,basi Tanganyika itakuwa kwenye matatizo makubwa na si kama mnavyofikiria,hilo napenda mlifahamu na pia mlitafakari kwa akili yenye kuona mbali ikichanganya na matokeo.
Wazanzibari wanasema mambo na kero za Muungano ambazo si kuwa hazipo zipo na zinajulikana na walio wengi , madai ya WaZanzibari na serikali zao zinazopita kila siku yanajulikana na viongozi na maraisi wote walioshika wadhifa wa kuingoza Jamhuri hii ya Muungano wa Tanzania ,wanasema yashughulikiwe yatatuliwe ,uwepo uwiano wa nchi mbili zilizoungana ,iwepo heshima kwa Raisi wa Zanzibar (siwezi kusema na waTanganyika kwa sababu wanazozijua wao hawataki iwepo Tanganyika ,japo kuna ushahidi wa huyu Kikwete kudai kuwepo kwa Tanganyika)
Haiwezekani awepo Raisi wa Nchi iliyokuwemo ndani ya Muungano halafu mumfanye kama mwandishi wa habari ,hii itasomeka kama dharau kwa WaZaznibari na kwa hali ilipofikia sasa hivi huwezi tena kuiondoa Zanzibar kwani hali ya hewa hairuhusu kufanya jambo hilo kwa njia za amani ni too late kinachowezekana ambayo naona ni busara aliyosema Muheshimiwa Kikwete ni kuivuta na kuiamsha serikali ya Tanganyika na kuendelea kwa msemo uleule uliotumika UN kuwa :-
United Republic of Tanganyika and Zanzibar continued as a single Member, changing its name to the United Republic of Tanzania on 1 November 1964...
Lakini kusema watu wagawane mbao nakuhakikishieni WaTanganyika mtauwana na kugawana mapande mapande na msitarajie kama mtakuwa wamoja kuigandamiza Zanzibar kama mnavyofanya sasa ,hio ni ndoto mbaya sana kwenue asiefahamu historia za mapambano ,hivi kunakoonekana kujikaza kwa baadhi yetu ,kuwa tuwaachie Zanzibar yao na tuchukue Tanganyika yetu ,basi hayo sio maneno ya kuitakia mema Tanganyika mtauwana kama ngedere ila kama mnataka hivyo basi kwanza ni kuirudisha Tanganyika wakati Tanzania ipo as a transit ,natumai nimefahamika.