MWANAWAVITTO
JF-Expert Member
- Dec 2, 2011
- 258
- 220
Habari za wakati huu wapendwa. Najua ndugu zetu WAISLAM wapo katika mfungo wa mwezi mtukufu wa RAMADAN, kipekee niwatakie kheri na fanaka"RAMADAN KHAREEM"
Ni siku ya tisa tangu nimerejea jijini Arusha baada ya kukosekanakwa mwezi mzima.
Kama ilivyo ada, kurejea kwangu kumekutana na mambo kadha, yakufurahisha na kuhuzunisha pia,
Baada ya kuwasili nilipokelewa kwa furaha na marafiki zangu, jambo la kushtusha walinipa habari za kufariki kwa mwanachama mwenzetu wa CHADEMA na rafiki yangu Ndugu SAID ABDALLAH, sikuamini nilihisi kama nipo ndotoni, wakati naondoka tuliagana naye vema akiwa buheri wa afya, ghafa naambiwa amefariki, ni pigo kubwa kwetu. pumzika kwa amani KAMANDA SAID ABDALLAH.
Nikiwa nimezama ndani ya dimbwi la Tanzia, ghafla napewa TAARIFA ZA UJIO WA CUF-ARUSHA MJINI.
Ilikuwa ni habari ya kushangaza sana, kama inavyoeleweka jimbo hili ni ngome ya CHADEMA yenye wafuasi wenye ITIKADI ZA KIGHAFIDHINA wasiopenda UONEVU, UBAGUZI, DHULUMA na UPENDELEO. kwa ufupi huwezi kuzitaja siasa za TANZANIA bila kulitaja JIJI HILI.
Ujio wa viongozi wa CUF ulitanguliwa na uzinduzi wa mashina na kusaka wafuasi na himaya, nakumbuka kipindi cha nyuma niliwahi kueleza kuwa nimekutana na ujumbe wa CUF kutoka makao makuu Dar es salaam wakiwa na harakati za kusaka wanachama,
Hatimaye ujumbe wa kitaifa ukiwa na salamu kutoka kwa PROFESA IBRAHIM LIPUMBA.
Katika mbio hizi za kisiasa CUF walifanikiwa kuibomoa CCM kwa kuwachukua baadhi ya wanachama wake, akiwemo kada maarufu wa chama cha mapinduzi Ndugu HAMZA ambaye pia alitawazwa kuwa Mwenyekiti wa Vijana CUF wilaya ya Arusha.
Mpaka ujumbe huu mkubwa unaondoka haukufanikiwa kuvuna wanachama kutoka CHADEMA, hata mmoja, huu ni ujumbe tosha ya kuwa CHADEMA iko imara na ni NGOME isiyotikiswa.
Kwa mujibu wa taarifa ni kuwa wanakampeni wa kuinadi na kuhamasisha watu kujiunga na chama chao walitumia njia zisizofaa katika harakati zao na hivyo kujikuta katika wakati mgumu na hata kunusurika kupigwa.
Moja ya mbinu zao ilikuwa ni udini. Chini ya mwamvuli huu waliwahamasisha WAISLAM walioko CHADEMA kujitoa na kujiunga CUF kwa hoja kuwa CHADEMA ni chama cha KIKRISTO.
Hoja hizi zilitumiwa sana na baadhi ya MAIMAMU ambao siyo wazawa jambo ambalo lilizua hasira kubwa miongoni mwa WANACHADEMA WAISLAM, ambao hawakupendezwa na UPUUZI huo.
Mmoja wa WANACHADEMA WAISLAM (namtaja kwa jina moja) RAMADHANI aliniambia huku akiwa amekasirika "kamanda, eti Imamu ananiambia niachane na CHADEMA kwa sababu niya KIKRISTO halafu tujiunge na chama chetu CUF," akaongeza kusema "hawa jamaa wajinga sana, kwanza hata HUKO MSIKITINI siendi tena nitaswali nyumbani" aliongea kwa lafudhi ya KISAMBAA huku akihamaki.
Tukio hili linanikumbusha miaka miwili iliyopita ambapo kampeni kama hizi ziliendeshwa na kuwafanya marafiki zangu sita kugoma kwenda MSIKITINI kwa sababu kama hizi, leo CUF wameshindwa kutambua HISTORIA na wameyarudia matapishi ya CCM kwenye uchaguzi mkuu wa 2010.
Habari hizi zimekuwa "HOT CAKE" JIJIN ARUSHA. Kwani ukihoji mashina na matawi pamoja na viongozi wake utakuta ni wale wale wanaoendeleza siasa za ubaguzi,
kama ilivyo ada watu wa ARUSHA kwa asili yao hawapendi UBAGUZIwala UONEVU. Kwa mtindo huu niwaase viongozi wa ngazi ya juu TAIFA-CUF, huenda hawazijui habari hizi, ninaheshimu PROFESA LIPUMBA, najua HAKIKA ya kuwa yeye sii MBAGUZI wala MDINI lakini JAHAZI alilopanda limejaa watu wenye DHAMIRA MBAYA na MBOVU ambao watamwangusha kama siyo kumwangamiza kabisa kisiasa.
Kwa mwendo huu atambue "CUF INAKUFA KIFO CHEMA" cha udini na ubaguzi kwani watu wa upande wa pili hawatawaunga mkono, hivyo umefika wakati mwafaka wa yeye ama KUONDOKA CUF au kukifumua chama hicho.
Lakin mimi namshauri ni bora kuondoka kuliko kubaki.
CUF wasitegemee kukua na kuchukua dola bali wategemee kudumaa hatimaye "KUFA KIFO CHEMA"
wasalaam.
Mwanawavitto kiraro