CUF haina viongozi Tanzania Bara? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF haina viongozi Tanzania Bara?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Antsadism, May 27, 2008.

 1. A

  Antsadism Member

  #1
  May 27, 2008
  Joined: Mar 22, 2008
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nafuatilia malumbano yaliyoshamiri baina ya chama cha CUF na CCM kuhusu mapendekezo ya vyama vyote viwili kutaka kuwe na Serikali ya Mseto Visiwani Zanzibar.

  Wakati katika upande wa CCM nimekuwa nikiona au kusoma viongozi kutoka sehemu zote mbili kama Rais Amaan Abeid Karume, Ramadhan Salehe Ferouz (Zanzibar), Luteni Yussuf Makamba, Kingunge Ngombale – Mwiru au Tambwe Hiza (Tanzania Bara) wakizungumzia suala hilo, upande wa CUF hali inakuwa kinyume.

  Ukiomwondoa Mwenyekiti wa Chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye kama ulivyosema Umoja wa Vijana wa CCM kuwa anaburuzwa na Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharrif Hamad, hakuna kiongozi mwingine kutoka Tanzania Bara anayezungumzia suala hili.

  Badala yake, viongozi wa CUF “waliolishikia bango” kwa kiasi kikubwa jambo hili ni Maalim Seif; Mbunge wa Wawi kisiwani Pemba, Hamad Rashid Mohammed na Msaidizi Maalum wa Maalim Seif (Mambo ya Nje), Ismail Jussa Ladhu.

  Mbali na hao, wengine wanaosikika kwa mbali ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Zanzibar), Juma Duni Haji pamoja na Mkurugenzi wa Taifa wa Haki za Binadamu wa Chama hicho, Saidi Miraji ambao wote wanatoka Zanzibar.

  Ninachojiuliza na kushindwa kupata jawabu ni je: kama ni kweli jambo hili linaihusu CUF kama chama cha siasa kilichosajiliwa kisheria na kinafanya kazi pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano kwa maana ya Zanzibar na Tanzania Bara, mbona sura hii inakosekana?

  Ina maana ukimwondoa Lipumba “anayeburuzwa” na Maalim Seif kama walivyosema Vijana wa CCM, viongozi waliobaki katika chama hiki wote ni Wazanzibari?

  Kama sivyo, mbona matamko yote yanayotolewa na CUF kusisitiza juu ya kutokuwa na haja ya wananchi kupiga kura ya maoni ili kubariki kuundwa au kutoundwa kwa Serikali ya Mseto yanatolewa Dar es Salaam (Tanzania Bara), lakini wanaozungumza siku zote ni viongozi kutoka Visiwani?

  Kama suala hilo ni la kitaifa ambapo ni agenda ya CUF kama chama cha siasa, kwa nini hata lilipozungumzwa nje ya Dar es Salaam katika mkutano wa hadhara ulioitishwa mjini Tanga hivi karibuni na kukosa mafanikio nako lilizungumzwa na Saidi Miraji, kiongozi ambaye pia alikwenda huko kutoka Zanzibar?

  Mbona hatumuoni angalau Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Wilfred Muganyizi Lwakatare na viongozi wengine waandamizi kutoka Tanzania Bara?

  Je, hii inaamisha kwamba CUF haina viongozi waandamizi wa kitaifa katika upande wa Tanzania Bara?
   
 2. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2008
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 705
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  CUF wote hamna kitu, SI LIPUMBA, SI SEIF wote wamekaa pale kwa kutolea Macho hela za Ruzuku.
   
 3. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2008
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,310
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mimi sio mwanachama wa CUF kama wapo watanikosoa kama nimekosea lakini nafikiri CUF hawana CUF bara wala CUF zanzibar, na ndo maana wana safu ya uongozi mmoja tu wa tanzania badala ya zanzibar na bara.
   
 4. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2008
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,571
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Sawa na jinsi CHADEMA wasivyo na viongozi Tanzania visiwani.
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,981
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Naomba ufafanuzi mnapo sema vyama vya upinzani havina uongozi?
   
 6. N

  Ndivyo Ilivyo JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2008
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 243
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe kabisa. Zaidi, suala hilo la mseto si ajenda ya Cuf as Chama, bali ni ajenda ya viongozi binafsi wa CUF kutoka Pemba na wapambe wao wa (Unguja) hao wanaoishikilia bango kwa madhumuni yao binafsi. Mengi yanayoelezwa ni uongo na propaganda (za hali ya juu). Zanzibar hali ni shwari, na Wapemba na Wa-unguja wa kawaida pale Zanzibar mjini bukheri wa hamsini na shughuli zao.
   
 7. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #7
  May 28, 2008
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,571
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Umepata taarifa ya vipeperushi vilivyozagaa Unguja?
  Hali si shwari ndugu yangu, si shwari hata kidogo.
  Taarifa ninazopata ni kwamba watu wa kutoka bara wanashindwa hata jinsi ya kupata marafiki maana ukijihusisha na waupande mmoja wa upande mwingine wanakuchukia automatically.

  Tatizo la Zanzibar kimsingi si baina ya wapemba na waunguja ila ni baina ya wanamapinduzi na wale wanaochukuliwa kuwa wapinga mapinduzi.
   
 8. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #8
  May 28, 2008
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,571
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Katika siasa ni vigumu kutenganisha agenda za Chama kwa ujumla na agenda za viongozi ! It is almost impossible.
   
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,014
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Antsadism, ni kitu gani kimekufanya uione tofauti hiyo ya uongozi baina ya CUF na CCM hivi sasa? Mi nilidhani hivi vyote ni vyama vilivyosajiliwa na ni halali kwa mujibu wa sheria. Sioni ajabu ya viongozi wa CUF Zanzibar kulizungumzia suala hili kwa sababu wanalifahamu sana kuliko wengine. hao akina makamba waliojiingiza kichwakichwa si unaona waliyoyafanya?
  lakini kwa upande mwingine tusisahau kuwa CUF ni chama cha siasa ambacho nacho kila political strategies zake
   
 10. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 201
  Trophy Points: 160
  Wewe acha kuzuka na uzushi ,CUF wanafahamu Nyerere alikuwa msomi kuliko Karume halikadhalika Viongozi wa wakati hua akina Thabit Kombo na vizee vyengine vyote vilikuwa mbumbumbu ukilinganisha na timu ya Nyerere ndio maana akina Karume wakapigwa bao ambalo hadi leo badu awajalirudisha.
  Na kwa vile mambo hurithiana Wairsi wa Nyerere wanaijua hali ya udhaifu wa watoto wa Kalume kuwa nao wamerithi umbumbu na wanajua fika hawaiwezi timu ya CUF katika masuala ya kujadiliana maana safu ya CUF sio mchezo kila mtu anamshinda mwenziwe ,na kwa vile ngoma wanaiweza ndio wameachiwa wenyewe ukizingatia ujuaji wa siasa za Zanzibar na Makamba na Kingunge wamepelekeshwa mbio hadi makubaliano yamefikiwa na kuweza kuyaweka katika jalada tayari kwa kutiwa saini ,nini kilichotokea walewale mambumbu wamezuka na kulia butiama na kudai warudishiwe ASP yao ili waende wakaendeleze mambo ya mauaji na kupoteza watu ,kuwachukuwa na kuwapeleka kusiko julikana ,si umiona juzi waliwakamata waPemba Muungwana akaona sasa jamaa wanataka kuvuka mipaka na kumuharibia .akawambia nyooni nyie haya warudisheni haraka mliko wachukua msio kuwa na haya wala msioona vibaya ,na ndivyo ilivyotokea wamerudishwa mpaka walipochukuliwa. Toka lini mtuhumiwa akaachiwa na vyombo vya polisi halafu akarudishwa alipochukuliwa ,basi jamaa walikaripiwa na kuambiwa wasije wakafanya tena mchezo huo wa kuwakamata WaPemba kwa kisingizio cha uhaini. Je umesikia lolote si wahafizina wameufyata na sasa Muungwana wakapelekea umeme kwa kasi akawaunguzia kila kitu.
   
 11. N

  Nyadundwe Senior Member

  #11
  May 28, 2008
  Joined: Jan 16, 2008
  Messages: 179
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Usije ukatuuliza baadae kwa nini Raisi wa Zanzibar hajawahi kuwa Msukuma!
   
 12. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #12
  May 28, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,597
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  CUF ni Zenj..hakuna CUF bara, huko Bara labda kuna Kafu
   
 13. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #13
  May 28, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  kamanda hii haijatulia kabisaa....
   
 14. Bikirembwe

  Bikirembwe JF-Expert Member

  #14
  May 28, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 250
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ikiwa CCM na wafuasi wake wanapiga mbiu ya mgambo kuwa Tanzania ni nchi ya amani, usishangae kusikia kuwa Zanzibar ni shwari lakini wajue kuwa wanaficha moto unaowaka chini kwa chini ukipata upepo utachoma wengi.
   
 15. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #15
  May 28, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,597
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Sasa nawe usiwe unaleta vitisho hapa, ilhali tuna kila sababu ya kusema kuwa Bara kuna Kafu na sio CUF
   
Loading...