Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,396
- 21,976
Najua kwamba Rais Samia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, lakini ni jambo lililo wazi kwamba yeye kama Rais wa Tanzania, maamuzi yake kwa zaidi ya 98% yanahusu upande wa Tanzania bara peke yake, kwa sababu upande wa Zanzibar wana raisi wao na serikali yao.
Katika hali kama hii, na ukizingatia kwamba Rais Samia anatokea upande wa Zanzibar, ningeshauri sana kwamba Rais Samia ajiepushe kufanya maamuzi makubwa ambayo ni ya muda mrefu (yana lock-in effect ya muda mrefu) upande wa bara peke yake. Kumekuwa na hisia zinazozidi kukua kwamba Rais Samia anafanya maamuzi ambayo baadaye yatakuwa na athari mbaya upande wa Tanzania bara, wakati yeye amemaliza muda wake na kurudi Zanzibar, na kuwaacha Watanzania bara wakisumbuliwa na matokeo ya maamuzi yake.
Mifano ya maamuzi ambayo Rais Samia anachukua juu ya mambo yanayohusu bara peke yake ni kama suala la mkataba wa bandari kwa DP Word ya Dubai, na hili la kuchimba madini ndani ya mbuga ya Serengeti na nyinginezo, ambapo, TANAPA, chombo cha utalii Tanzania bara, kilishalikataza sana.
Ingekuwa busara sana kama Rais Samia angeonyesha subira na kuacha maamuzi juu ya mambo makubwa kama hayo, yenye long term lock-in effect, yafanywe wakati Rais wa Tanzania ni mtu kutoka upande wa bara. Hii itasaidia kutokuza chuki na kutoa hofu upande wa bara kwamba Raisi Samia hafanyi mambo kwa manufaa ya watu wa bara, na labda ana ajenda ya siri.