Nimekuwa nafuatilia malumbano yaliyoshamiri baina ya chama cha CUF na CCM kuhusu mapendekezo ya vyama vyote viwili kutaka kuwe na Serikali ya Mseto Visiwani Zanzibar.
Wakati katika upande wa CCM nimekuwa nikiona au kusoma viongozi kutoka sehemu zote mbili kama Rais Amaan Abeid Karume, Ramadhan Salehe Ferouz (Zanzibar), Luteni Yussuf Makamba, Kingunge Ngombale Mwiru au Tambwe Hiza (Tanzania Bara) wakizungumzia suala hilo, upande wa CUF hali inakuwa kinyume.
Ukiomwondoa Mwenyekiti wa Chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye kama ulivyosema Umoja wa Vijana wa CCM kuwa anaburuzwa na Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharrif Hamad, hakuna kiongozi mwingine kutoka Tanzania Bara anayezungumzia suala hili.
Badala yake, viongozi wa CUF waliolishikia bango kwa kiasi kikubwa jambo hili ni Maalim Seif; Mbunge wa Wawi kisiwani Pemba, Hamad Rashid Mohammed na Msaidizi Maalum wa Maalim Seif (Mambo ya Nje), Ismail Jussa Ladhu.
Mbali na hao, wengine wanaosikika kwa mbali ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Zanzibar), Juma Duni Haji pamoja na Mkurugenzi wa Taifa wa Haki za Binadamu wa Chama hicho, Saidi Miraji ambao wote wanatoka Zanzibar.
Ninachojiuliza na kushindwa kupata jawabu ni je: kama ni kweli jambo hili linaihusu CUF kama chama cha siasa kilichosajiliwa kisheria na kinafanya kazi pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano kwa maana ya Zanzibar na Tanzania Bara, mbona sura hii inakosekana?
Ina maana ukimwondoa Lipumba anayeburuzwa na Maalim Seif kama walivyosema Vijana wa CCM, viongozi waliobaki katika chama hiki wote ni Wazanzibari?
Kama sivyo, mbona matamko yote yanayotolewa na CUF kusisitiza juu ya kutokuwa na haja ya wananchi kupiga kura ya maoni ili kubariki kuundwa au kutoundwa kwa Serikali ya Mseto yanatolewa Dar es Salaam (Tanzania Bara), lakini wanaozungumza siku zote ni viongozi kutoka Visiwani?
Kama suala hilo ni la kitaifa ambapo ni agenda ya CUF kama chama cha siasa, kwa nini hata lilipozungumzwa nje ya Dar es Salaam katika mkutano wa hadhara ulioitishwa mjini Tanga hivi karibuni na kukosa mafanikio nako lilizungumzwa na Saidi Miraji, kiongozi ambaye pia alikwenda huko kutoka Zanzibar?
Mbona hatumuoni angalau Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Wilfred Muganyizi Lwakatare na viongozi wengine waandamizi kutoka Tanzania Bara?
Je, hii inaamisha kwamba CUF haina viongozi waandamizi wa kitaifa katika upande wa Tanzania Bara?