CUF/CHADEMA - Ni kweli Taifa Limegawika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF/CHADEMA - Ni kweli Taifa Limegawika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, May 3, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  HATUA ya Mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi, kutaja hadharani majina ya baadhi ya wafanyabiashara na mwanasiasa mmoja kuwa ni ‘mafisadi papa’ imeonekana dhahiri kuligawa taifa katika makundi mawili yaliyoanza kujengeana chuki.
  Makundi hayo ambayo yako ndani na nje ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), serikalini na nje ya chama hicho tawala ni yale ambayo ama yanamuunga mkono au kumpinga.

  Miongoni mwa watu ambao wameshaonyesha kuguswa na hoja hiyo na kuitolea kauli ama za kuonyesha msimamo wao, au wakishikwa na kigugumizi cha kuisemea kwa ujasiri ni pamoja na Rais Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba.

  Mbali ya hao, wengine ambao nao wameweka mguu katika hoja hiyo ni wabunge, Dk. Wilibrod Slaa (CHADEMA), Anne Kilango (CCM), Christopher ole Sendeka na wanasiasa wengine kutoka makundi tofauti ya kisiasa....!

  _______________________

  Je wanamageuzi wa Tanzania ambao kwa pamoja tunashiriki katika kuushawishi umma wa KiTanzania uachane na siasa za CCM na kuelekea kwenye mageuzi makubwa ya kiutawala ,inakuwajekuwaje tunafikishwa katika hitimisho la aina hii ,kuwa tumegawanyika kwa maana sote ni wafuasi wa Sultani CCM ila tunafanya kazi nyuma ya pazia.

  Kwa maana Vyama vya upinzani navyo vinaonyeshwa kuwa vimejibanza katika kambi za CCM ,kwa jinsi habari hiyo hapo juu ,mwananchi wa kawaida akiona na kusoma habari hii ,kusema kweli itamvunja moyo kabisa na kuona kuwa kumbe hata wakuu nao ni washangiliaji na wanakingia kifua upande mmoja kati ya pande za CCM.

  Napenda kutoa onyo kwa wakuu wa Vyama vya Upinzani kama walivyoainishwa hapo juu ,CUF (Lipumba) ,CHADEMA (W.Slaa) ,kuwa wakae mbali na kuacha kuwakumbatia waliotapakaa mavi (Machafu) ,wasiwakaribie wala wasiwatetee kwa kutoa maelezo ambayo yatawaonyesha wapo upande fulani ,hilo ni kosa katika siasa za upinzani dhidi ya chama tawala ,tena ni kosa kubwa sana ,linaweza kuhatarisha msimamo wa Chama dhidi ya serikali tawala.

  Mambo haya ya ufisadi yanayotokea ndani ya Chama Tawala ni turufu kubwa sana inayohitaji kutunzwa na kuenziwa kwa hali na mali ,isipotezwe kwa maana hiyo ni faida kwa upande wa upinzani.

  Ikiwa utagongana na waandishi habari ambao huwa na mitego yao na lengo lao ,mara nyingi kuwadai viongozi wetu wakuu ,kuwa msimamo wao upo wapi kutokana na madai ya fisadi huyu dhidi ya fisadi yule au yaliyosemwa nao ,hili ni suala mtego ambalo namna watakavyoliandika na kulifanyia usanii ni kama tuonavyo hapo juu.

  Upinzani ni kuponda tu mpaka kieleweke na si kujibamiza katika kambi yeyote ile ya Chama tawala ,mafisadi hawa wanatafuta huruma ya wananchi na kwa hivyo hujaribu kila njia ikiwemo kuwahusisha viongozi wakuu wa Vyama vya upinzani na kinachotokea ni wafuasi wa vyama pinzani kusapoti wakuu wao na hapo kupata mlegezo kwa kiasi fulani kwa hawa mafisadi maana imani inayojengwa na kiongozi mkuu inamuokoa mmoja na kumzamisha mwengine na hivyo hata wale wananchi wenye moyo mwepesi inakuwa ni rahisi kuona kuwa fulani amesemwa ni msafi na mwengine ni fisadi.

  Hilo halitakiwi kabisa hawa wananchi wanaotoka kwa mfano huko Tabora inakuwa wameshapata sababu kuwa hata fulani kasema kweli ,itakuwa tumekosa tunalolikusudia katika kuwagaragiza wafuasi wa sultani CCM mbele ya macho ya wananchi ,jamani tusichaguwe kama tunagandamiza basi iwe kwa wote mkubwa kwa mdogo ni kuwachanganya tu kwenye kapu moja hakuna msalie mtume. Wameoza wote hakuna nyangumi wala papa.

  Kama tulikuwa tunasema Serikali ya Sultani CCM inakamata dagaa ni kuiambia kazi bado hatutaki madagaa peke yao ,kuna wengine ,ikikamata mapapa tunasema itazame nyavu yako imetoboka kuna manyangumi wamechana na kuirarua na sasa wanapeta wakamate na hao ni kuiweka serikali katika hali bize na ngumu ,na si kuwapa nafasi kuwa wamefanya vyema ,Serikali iliyoko madarakani haitakiwi hata sekunde moja kuonyeshwa kuwa imefanya wema ,ni kuiponda tu ,ndio nikasema hata kama imepeleka sindano za bindamu kwenye vijiji upinzani udai kumepelekwa sindano za kudungia ng'ombe ,lazima tuende opposite direction ,mi ningefurahi sana kama Lipumba na Slaa wangesema wote ni mafisadi ,kazi yao ingekuwa kwisha ,hakuna kujiuma uma na kuonyesha kubabaika ,huu utakuwa ni udhaifu kwa viongozi wetu hawa nani asiejua kuwa Mengi anaisaidia CCM ,nani asie jua kuwa Rostam anaisadia CCM ,viongozi wetu mmeshikwa na udhaifu gani hata kufika kujibambika upande mmoja ?

  Tunataka Sultani CCM ajione hana pa kushika wafuasi wake wote wawe ni wenye kuangamizwa na kuunganishwa na ufisadi na si watenda haki ,jamani ndio pakawepo upinzani ,msifikiri upinzani ni lele mama na kulegezeana kamba ,hilo halipo ndipo mkamuona Seif Sharifu anatoka kipovu kwa kumkandia Kikwete ,si kama anataka sifa au aonekane shujaa hapana anaonyesha hisia za upinzani katika jukwaa la kisiasa na kutaka kuyazidi mawazo ya mwananchi wa kawaida na kumhamisha mwananchi katika mawazo ya Kikwete ni kiongozi bora au CCM ni Chama bora ,ni lazima umtaje mhusika kwa jina kabisa ikiwa kweli au si kweli na siasa inaruhusu hilo ,ndio ukasikia wengine wakijibu ni muongo ,hao ni CCM lakini ujumbe umeshafika na wananchi wanalainika kidogo kidogo ,kwa sababu unapozungumza inakuwa kama unapanda mbegu kwa msikilizaji na mvua za maneno ndizo zitakazoifanya mbegu ile ianze kuchipua na kuota na kushika kasi ,hivyo mbegu tunayoihitaji kupandwa ni kuwa CCM wote ni mafisadi hakuna aliebora ,vita vya wao kwa wao visitunafasishe kumtetea au kumkingia kifua mmoja wao ni kuwachanganya wote mbele ya macho ya wananchi.
   
  Last edited: May 3, 2009
 2. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mimi siamini kama mabadiliko ya kweli yatakuja kama tunaanza kupiga marungu juu ya vyama! Mpaka pale tutakapoelewa vyama ni vyombo ambavyo vinaleta watu wenye mtizamo mmoja karibu, lakini wanakuwa sio wafungwa wa kutoona mazuri nje ya chama chao hatutafika popote.

  Siasa za tanzania kwa mtizamo wangu mimi, sio wa kupinga ccm kama chama, na kusimamisha chadema ama CUF kama vyama mbadala. Ni wakati wa kusimamia agenda na maadili ya ungozi! Watu watakaoweza kushinda uchaguzi wa 2010 ni wale ambao wataacha political attacks na kuangalia zaidi hali ya watanzania kwa kupiga vita misingi mibovu ya viongozi, ufidadi na kuwapa ari watanzania kwamba mabadiliko yatawezekana.

  Tunaposhidwa kujitoa katika hizi kuta za vyama, ccm wataendelea kushinda tu!
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Taka zilifichwa chini ya kapeti siku nyingi na wageni walikuwa wakifika ukumbini wanakuta pasafi, lakni taka zimeendelea kusokomezwa chini ya kapeti sasa zinachomoza na kutoa harufu. Ufisadi umekuwa katika mfumo wa serikali za CCM kwa miaka na kufumbiwa macho. wananchi waliipuuza hatari ya ufisadi au walifanywa na CCM wapuuze hatari hizo mpaka sasa wanaona hatari ipo mbele yao, sasa taka zinafukuka kutoka chini ya kapeti,hii ndo mbegu CCM imeipanda na ndio mbegu itakayo kisambaratisha kama ilivyosambaratika KANU kule KENYA kwa staili kama hii. Inanikumbusha zile falsafa za akina Sir Thomas Moore juu ya uhai wa mifumo au taasisi watu wanazojiundia kuwa "zipo taasisi hizo(mfano ukoloni) zikiishi na mbegu ya kujimaliza"
  Hapana ubishi kama KANU na UNIP vimemalizwa na "mbegu" ya ufisadi, na hii haitakuwa manusura kwa CCM, wamepanda mbegu ya ufisadi na ndiyo inayowamaliza, karibu "parapanda litalia".
   
 4. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mbegu hazijimalizi zenyewe, zinahitaji an organized entity inside and outside kujingoa. Hii ikiwa inamaana ndani ya CCM na nje ya CCM. Narudia kusema, siasa za party attacks ndani ya Tanzania bado hazitatufikisha popote! maana hatuna ethnic lines or class lines! Until we build those, we better stick on right agenda!
   
 5. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ili tuweze kupata mafanikio katika vita hivi lazima tuweke Utaifa mbele ya vyama vya siasa. Vinginevyo tutakuwa hatufiki popote.
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Utaifa upo ,kilichomtoa Kanga manyoya kilitokea Pemba na hadi hii leo Sultani CCM ameshatupwa baharini na kuzamishwa.

  Tatizo ni hili la viongozi wakuu huku upande wa Tanganyika kuchanganyika katika Siasa kwa kujiweka katika moja ya kambi za Sultani CCM ,na hivyo kutoeleweka pamoja na kuyumbisha msimamo wa upinzani.

  Wananchi wengi inaonekana wameshaamka katika kutaka mageuzi ya kiutawala ,ila kinachoonekana ni kwa viongozi wakuu wa upinzani kulegeza kamba pale ambapo wanahitajiwa kuvuta na kufyetua kamba hiyo ,Chadema wanaonekana kufyetua vizuri lakini baada ya muda wanaonekna kama wanasinzia na kuwapozesha wananchi ,jamani tulipofikia ni kukanyaga tu hadi kinaeleweka ,mtawala asipewe nafasi ya kupumua ,ikiwa wao wanashika kasi katika kuswagana ,upinzani uwe unaivuka kasi hiyo katika kuwavuruga ,kwa kuifanya miswagano yao kuwa si lolote zaidi ya kununua muda.
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  May 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mwiba,
  Nitazungumza kumlinda Dr.Slaa na Chadema ktk hili kwa sababu kwanza, ana ushahidi tosha dhidi ya Rostam akiwa mbunge, kiongozi wa chama na serikali hivyo sioni sababu yake kukaa kimya..Na wala hachagui upande kwani madai yake yametokea hata kabla Rostam na Mengi hawajaanza vurugu zao..lakini huyu Lipumba sijui kimemkuta nini kwanza aliunga mkono serikali inunue mitambo ya Dowans akisema kwamba hata mitambo mipya inaweza kuwa feki..Ningependa sana anionyueshe mitambo feki huwa inafanana vipi!. bado bila aibu anaendelea kutetea uozo na kukifanya chama cha CUF kupoteza ile nguvu yake ya mwaka 2000 ambayo wananchi wengi walalahoi walikuwa nyuma ya chama hiki.. sijui kuna kitu gani kimebadilika maanake sasa hivi inaonyesha kama vile CUF ni chama pandikizi..
   
 8. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #8
  May 4, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu Mkandala,
  Tupo pamoja na ikumbukwe kuwa hoja iliyopo mbele ya watanzania ni kuchagua uongozi makini ambao utalitoa taifa hapa lilipo.Nafasi ya vyama itashughulikiwa huko mbele ya safari baada ya kuwatambua na kuondoa viongozi wenye fikra za kifisadi.
   
 9. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
   
 10. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #10
  May 4, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Yote hayo mliyoyasema yana mshiko ,lakini unaposema umlinde,unamlinda kwa yaliyopita ,kama msimamo wake ungelikuwa ni kuswaga tu moja kwa moja asingeliingia katika kundi la pamoja na Lipumba au Zitto ndio hapo nikasema itabidi wajisahihishe ,kwa ufupi wote hapo mwanzo walianza vizuri kabisa lakini haya yanayotokea hivi sasa ndio yanayonishangaza na kuwaona wanapoteza muelekeo na kuwapoteza au kuwazubaisha wananchi na kuwafanya mazezeta.

  Tafadhalini sana msinijie na lugha ya kusema bora fulani ,hilo sitokubaliana nalo na ninayo haki hiyo. Ninapolaumu wakuu ni lazima wao waelewe kosa lao katika siasa za upinzani vinginevyo watakuwa ndumila kuwili au waoga kwa kiasi fulani ,na watakuwa wanawadanganya wananchi kwa maneno wanayoyaendea kinyume.

  Ikiwa mtafuatilia siasa za ulaya za kati kuna vyama vidogo sana na mara nyingi hutokea muungano wa vyama hivi ili kuweza kuunda serikali ,kwa kweli vyama hivi vinaweza kuzusha sababu ndogo tu na ikawa ndio sababu ya kuitisha uchaguzi mpya ,hii hutokana na misimamo yao ya kuikosoa serikali na huwa hawaungani na serikali au kuipa sapoti wao ni kutafuta au kwa lugha ya kwetu husaka habari na sababu na kuzifanyia kazi kikweli kweli bila ya kuhurumiana ,maana ndio unapoonekana upinzani wa kweli ,hizi kesi tulizonazo ambazo zinakatisha mwaka wa tatu ,kesi kama hizi zingezuka huko basi leo hii pasingekuwepo na Kikwete wala kingunge ,serikali nzima nje.

  nafikiri ipo haja kutafuta elimu ya kwenda na aina ya kesi hizi katika harakati za upinzani kupitia vyama hivi vya Ulaya njia na mikakati ya kuilazimisha serikali kufuata sheria na kuwajibika au kuwajibishwa ,najua kuwa upinzani tuna wabunge wachache sana ,chukulia wale waliojiuzulu hadi leo tunakwenda nao bungeni.

  Hivyo wakuu wetu ni lazima wawe na mshikamano katika kujipanga ili kupambana kikweli kweli na sio kuonekana wakivamia upande mmoja wa kambi za chama tawala ,Lipuma alifanya kosa kubwa sana katika uamuzi wa kusema mitambo inunuliwe,nafikiri angeweza kusema mitambo ingeweza kununuliwa lakini sio katika serikali tulio nayo ,kwani serikali tuliyonayo imejaa ukiritimba hivyo hata kuinunua itakuwa ni kutilia maji ukiritimba wa serikali iliyopo madarakani ,very simple jawabu na hivyo hivyo kwa Slaa kuwa kusema Mengi amefanya jambo la ushujaa ,(Sikumbuki vizuri alichosema) lakini angeweza kusema kuwa Mengi asitumie zana zetu katika kujikosha kwani hawa tumeshawataja wote na yeye tunawasiwasi ni mmoja wao ,hivyo Mengi atuwachie wenyewe tupambane nao hadi watakapojua kama meli hutembea baharini.

  jamani upinzani ni kupiga tu na kubomoa kila kinachochomoza kutaka kuuteka upinzani ,hizi tunazoziona ni hila za kutupotezea muda na kuwacha kuikurupusha CCM na viongozi wake walio madarakani ,tunaona sasa jamii yote imehamishiwa kusikiliza na kungojea hatma ya mibweko kutoka katika midomo ya mafisadi ,they keep opposition busy on their business while the aim of the opposition is to keep them (Government) busy & disturbing their movement ,hivyo ni lazima tuwe wabunifu katika kutibua harakati za serikali inapojaribu kujiweka sawa ,iwe tunabomu mepya na kuyarudia kimadai yaliopita na huku tunajijenga kwa wananchi kwa kuitelekeza serikali kuwa haifanyi kitu ,serikali iliyokuwepo imeshikwa na butwaa haijui la kufanya ,utendaji wake umepotea ,utekelezaji ni jambo la kinadharia ,kila mmoja anajifanyia kivyake vyake hakuna anaemsikiliza mwenzake wote ni maDC wote ni marasi wate ni mahakimu kama haitoshi wote ni mafisadi ,huko ndio kuponda na kuswaga.

  Kiongozi Mkuu wa upinzani anasema lakini Mengi kafanya jambo la kiume lakini mitambo bora ilivyosema serikali tuinunue , What kinds of administration we have here ? Kuyasema hayo ni kuwapa wao uongozi ,fikirieni vizuri muone athari za kuunga uunga mikono na miguu.
   
 11. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Date::5/4/2009
  Ufisadi papa, nyangumi wawagonganisha CUF na Chadema
  Zaina Malongo na Salim Said
  MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ametetea msimamo wake wa kuikosoa kauli ya Mwenyekiti Mtendaji wa Kmpuni za IPP Reginald Mengi kuwa inawatoa watanzania katika lengo la vita dhidi ya ufisadi nchini.


  Lakini Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemtuhumu Profesa Lipumba kwamba anaisaliti vita hiyo dhidi ya mafisadi


  Juzi, Prof Lipumba alisema Mengi anajipendekeza kwa Rais Jakaya Kikwete kwa bei rahisi kwa kuwa yupo madarakani kwa sasa na kwamba ataanza kumponda baada ya Rais huyo kuacha madaraka.


  Kufuatia kauli hiyo, maofisa wa Chadema walikerwa na kuamua kujitokeza katika vyombo vya habari jana wakimtetea Mengi kwa madai kwamba msimamo wa Mengi ni sahihi.


  Mkurugenzi wa masuala ya bunge wa Chama hicho , John Mrema aliwambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa chama chake kinasikitika kwa kitendo cha Profesa Lipumba kumwambia Mengi anajipendekeza kwa Rais Jakaya Kikwete.


  Mrema alifafanua kuwa, Profesa Lipumba ndio muasisi wa vita dhidi ya ufisadi nchini hususan katika sakata la ununuzi wa Rada na Ndege ya rais Mstaafu Benjamin Mkapa lakini sasa amekuwa msaliti wa misimamo yake aliyokuwa akiitangaza kwa wananchi.


  "Tunasikitika sana, profesa Lipumba namheshimu , lakini ametusaliti katika vita hii, kwa sababu yeye ndiye muasisi na aliyekuwa mstari wa mbele kuhusu kupinga ununuzi wa rada na ndege ya rais. Leo hii ameshindwa kusimamia misimamo na matamko yake aliyokuwa akiyatoa kwa wananchi" alisema Mrema.


  Akijibu tuhuma hizo profesa Lipumba alisema, Chadema hawakumuelewa kwa kuwa kauli yake iko wazi sana kuhusu kasoro za Mengi katika sakata la mafisadi papa.


  "Kama Chadema wameamua kumuunga mkono Mengi hata kama amekosea, hiyo ni hiari yao wenyewe, lakini kauli yake ni mbaya na inatutoa katika lengo la vita dhidi ya ufisadi" alisema Profesa Lipumba


  Profesa Lipumba aliliambia Mwananchi Ofisini kwake Buguruni jijini hapa kuwa, hajabadilisha wala kuusaliti misimamo kuhusu vita dhidi ya ufisadi nchini, lakini vita hiyo lazima ilenge katika kung'oa mzizi ambao mfumo mbovu wa serikali.
   
 12. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kulikuwa na muhimu gani wa kurudisha malumbano kwenye magazeti! Wapinzani wanahitaji njia za kuongea wao kwa wao kuimarisha!
   
 13. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  chadema walimuunga vipi mkono mengi?
   
 14. Nyumbu

  Nyumbu Senior Member

  #14
  May 5, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 141
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kila chama kina itikadi yake na misimamo yake. Hata kwenye suala la ufisadi, kila chama kina approach yake inayoamini ndio sahihi. Haya sio malumbano, ni kukomaa kwa mfumo wa vyama vingi.
   
Loading...