Hakuna ubishi kuwa hali ya maisha imekua ngumu hapa nchini kwetu. Bila kuingiza siasa, hebu kama great thinkers tujaribu kuangalia kwa mapana kuhusu matatizo tunayokabiliana nayo kwa sasa, ambayo ndo hasa yanachangia ugumu wa maisha.
1. Mfumuko wa bei
2. Ukosefu wa ajira
Nini kifanyike?
Mkuu
Ugumu wa maisha umechangiwa kwa kiasi kikubwa na kushindwa kwa sera za CCM
a) mikakati mingi isiyo na vipaumbele na mingi ikiishia katika makaratasi bila usimamizi wenye tija.
b) Serikali kupoteza dira, kukumbatia majambazi na mafisadi na kuwatelekeza raia wake, (mapato hayaendi kupunguza ukali wa maisha bali kwa mafisadi)
Mikakati isiyonavipaumbele ni kama mtu analala usingizi hajui ataota ndoto gani, si rahisi kupata maendeleo endapo hakunamikakati ya muda mrefu kuutokomeza umasikini (hakuna sera yoyote yakueleweka kukuza ajira,
viwanda ziii, kilimo ziii, mabilion ya kikwete kwa ndugu na jamaa nk)
Serikali imepoteza dira, imekuwa ya matapeli na mafisadi, imekuwa si ya kijamaa wala kibepari inaendeswa kwa nguvu ya wenye fedha na masikini hawana chao.
Kwasababu serikali imewekwa mikononi wa watawala/wanasiasa walafi, wako teyari kufanya kila liwezekanalo kuhujumu uchumi wa inchi ili watengeneze faida (mfano kubana mafuta na kuyapandisha bei watakavyo -
mtoto wa upuuzi huu ndiyo huo mfumko wa bei.)
Nini kifanyike.
a) Tupate serikali ya kweli, serikali ya watanzania (wenyenacho na wasionacho) serikali itakayoweka uzalendo kwa watu wake kwanza.
b) Tupate serikali itakayokuwa na vipaumbele vichache na vyenyetija mfano.
i) Elimu
ii) Afya
iii) Kufufua viwanda vyote na kuanzisha vingine (Kuunganisha makundi ya vijana wenye elimu zao na kuwapa mitaji kuendesha viwanada vya ubunifu nk)
c) Ipatikane serikali itakayoendesha vita ya kweli dhid ya wezi na mafisadi wote kwa sababu hii ndiyo sabau kubwa ya umasikini wetu na kushindwa kwa mipango yetu mikataba mibovu, wanyama na madini kuporwa nk.