Critical Thinking: Hali ngumu ya maisha, Je nini chanzo?

iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,168
2,000
Hakuna ubishi kuwa hali ya maisha imekua ngumu hapa nchini kwetu. Bila kuingiza siasa, hebu kama great thinkers tujaribu kuangalia kwa mapana kuhusu matatizo tunayokabiliana nayo kwa sasa, ambayo ndo hasa yanachangia ugumu wa maisha.


1. Mfumuko wa bei
2. Ukosefu wa ajira

Nini kifanyike?
 

Bangoo

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
5,600
1,195
Ni kweli mkuu kila mtu analalamika hasa sisi tulio na biashara, ni kutokana na kukosekana hata wanunuzi. Hali ni tete
 

Fpam

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
290
0
Watanzania tunategemea sana serikali na kutoa lawama

tumeshajua serikali ni hovyo basi tufanye kazi kwa bidii ili tuongeze hata kile kidogo tulichonacho
 

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,020
2,000
Serikali ikitowa fursa kwa wanainchi wake ni sawa imewaingizia fedha mifukoni, sasa serikali yetu inatoa fursa ambazo haizitekelezi , inqatoa fursa za kisiasa zaidi . Kwetu hapa maisha hali ya maisha ni ngumu kwa sababu fursa inazotoa serikali wewe mwanainchi inabidi ufanye kinyume chake, sasa hii ya kufanya kinyume ndio inaongeza ugumu wa maisha. kwa mfano:

1. Matibabu bure kwa akina mama wajawazito na watoto- inabidi mlengwa afanye kunyume na fursa hii vinginevyo akifuata fursa inavyosema atakufa, mjamzito inabidi anunuwe kila kitu, gloves, jik, sindano Ergometrine ya kuzuia damu zisimwagike, kadi ya klinil kumonitor maendeleo ya uja uzito,n,k na mtoto nae hivohivo.
2.Matibabu bure kwa wazee- Mzee ukienda kwenye hospitali za serikali dawa hamna , inabidi uende hospitali za private na huko inabidi ufanye kinyume cha fursa yaani ugharamikie gharama zote za matibabu yako vingenevyo utakufa.
3. Elimu ya sekondari ada kidogo kwenye shule za kata
- Sawa shule hizi za kata zinatoa elimu ya sekondari lakini hazina waalimu wa maana walioko ni wa voda fasta form four failure anamfundisha form four mwenzake, pia hazina maabara, library, nyumba za waalimu hakuna pia madarasa hayatoshi, sasa inabidi ufanye kinyume cha fursa yaani umpeleke mtoto shule za private la sivyo akibaki kwenye shule za kata atakuwa zuzu.
4.Hospitali za wilaya hazina madaktari qualified. Kwa hiyo ukiugua uende kenye hospitali hizo itabidi ufe maana watashindwa kugunduwa unaumwa nini maana ujuzi wao ni kidogo na ukiendelea kubaki huko utakufa itabidi ukodi gari kwenda kuifuata hospitali private iliko mfano kwa Dr,. Barki, kibaha picha ya ndege, fikiria unatokea Kigoma au Msoma. kufanya hivyo umefanya kinyume na fursa inavyosema.

Mambo yote hayo niliyokutajia ndugu yangu imind mwanainchi ukiyafanya basi yanaongeza ugumu wa maisha kweli kweli.

Serikali inahusikaje? serikali iliyoko madarakani inabidi ikusanye kodi ili iboreshe maeneo yote niliyoyataja ili sehemi hizo zitoe quality services na siyo quantity kama shule za kata, nini tatizo,? Tatizo ni usimamizi mbovu fedha zinazokusanywa hazifiki kwenye zilikoelekezwa wanazifisadi( syphone), ndo hizo unasikia ziko Uswiss, Mfano hai aliyekuwa katibu mkuu wizara ya fedha Ndugu GREY MGONJA alitumia fursa hii ya weakness ya usimamizi akafanikiwa kuchota hela za makusanyo ya kodi akapeleke kuweka Uswiss, na wengi tu wengine wanaendelea kufanya hivyo hadi hivi sasa, kwa mtindo huo NI LAZIMA MAISHA YAWE MAGUMU, TENA MAGUMU SANA.
 

Ndachuwa

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
5,964
2,000
What are policy makers (Government and BoT) doing to make our shilling stable?

1. "If a factor increases the demand for domestic goods relatively to foreign goods, the domestic currency will appreciate; if a factor decreases the relative demand for domestic goods, the domestic currency will depreciate". Is there any positive initiative being done such as AGOA and like? What Ministry of Trade doing to address this?

2. "In the long run, a rise in a Country's price level (relatively to the foreign price level) causes its currency to depreciate, and a fall in the country's relative price level causes its currency to appreciate". What is government doing to reduce rocketing of food prices?

3. "Increasing trade barriers causes a country's currency to appreciate in the long run" Do we really need to continue importing sub-standard goods from china such as plastic shoes, artificial flowers, low quality electrical goods? What is the role of Ministry of Industry and SIDO in supporting small scale industries such as for shoes?

4. "Increased demand for a country's exports causes its currency to appreciate in the long run; conversely, increased demand of imports causes the domestic currency to depreciate".When our leaders will show the way for example wearing suits made from Sungflag produce? Or Stocking their refirgerators with Dodoma wine instead of South Africa wine?

5."In the long run, as the country becomes more productive relative to other countries, its currency appreciates". Has anybody linked the depreciation of our shilling to the effect of factories closed after being privatised?

Source:Mishkin & Eakins, 7e

 

mayenga

JF-Expert Member
Sep 6, 2009
4,073
2,000
Haya maswali tangu tuko darasa la tatu tunaulizwa kwenye somo la uraia,kila siku makongamano na masemina yanatoa masuluhisho,watu wamepata shahada,stashada,shahada za uzamiri na uzamivu kwa kuyaandikia haya.Kuna tafiti nyingi zimejaa vumbi hazifanyiwi kazi,wanaosoma hawana jipya zaidi ya kucopy na kupaste.Karne hii hatuna haija ya kuzidi kuulizana mambo haya.Swali la msingi lingekuwa tumeyafanyia nini masuluhisho yaliyopo.Hakuna jipya chini ya jua.
 

sifongo

JF-Expert Member
Jun 5, 2011
4,810
2,000
Watanzania tunategemea sana serikali na kutoa lawama

tumeshajua serikali ni hovyo basi tufanye kazi kwa bidii ili tuongeze hata kile kidogo tulichonacho
Ni kweli Mkuu ukiangalia sana tunalalamikia serikali, mwanzo nilizani si sahihi lakini kwa upande mwingine SERIKALI inachangia, mfano SERIKALI ndio huwa inatoa tenda kubwa kubwa ambazo kama tukizipata mimi na wewe walio pembeni yetu watafaidika katika ajira hata kama ni za muda mfupi, lakini kwa hali ilivyo upataji wa hizo tenda kwa MTANZANIA wa kawaida ni ishu maana hongo inayotembea huko ni balaa.......
malalamiko kwa serikali hayawezi kukoma mpaka watakapodhibiti mianya ya rushwa, kazi tunafanya sana ila hailingani na kipato.
 

iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,168
2,000
Ni kweli Mkuu ukiangalia sana tunalalamikia serikali, mwanzo nilizani si sahihi lakini kwa upande mwingine SERIKALI inachangia, mfano SERIKALI ndio huwa inatoa tenda kubwa kubwa ambazo kama tukizipata mimi na wewe walio pembeni yetu watafaidika katika ajira hata kama ni za muda mfupi, lakini kwa hali ilivyo upataji wa hizo tenda kwa MTANZANIA wa kawaida ni ishu maana hongo inayotembea huko ni balaa.......
malalamiko kwa serikali hayawezi kukoma mpaka watakapodhibiti mianya ya rushwa, kazi tunafanya sana ila hailingani na kipato.
Kabla hatujalalamikia serikali, Je sisi tunatimiza wajibu wetu? Kwa mfano kulipa kodi stahili, kufanya kazi kwa bidii n.k? Hata nakubaliana na Fpam kuwa Wa TZ wamezidi kulalamika haka kwa vitu visivyo vya msingi.

Mfano, Juzi tu hapa katika sherehe za uzinduzi wa Jiji la Arusha, watu wamelalamikia matumizi ya Tsh 140m kwa ajili ya sherehe hizo. Je kama harusi ya kawaida tu kwa sasa ina cost hadi Tsh 30m itakuwa, shughuli ya kiserikali?

Pia ni kwa njia kama hizi ndo fedha huweza kurudishwa kwa watu na kupunguza ugumu wa maisha; kwa mfano hapo kuna mpambaji amepata kidogo, walinzi (Mgambo), printers kuchapa Tshirts etc. Hawa nao wataenda kununua mchele kwa mangi, kulipa tuition ya watoto, kujenga banda etc.
Hata kama waliopata hizo tenda, wamepata kwa kujuana, lakini ni watanzania....mwisho wa siku inaongeza mzunguko wa fedha.

Mara nyingi vitu kama hivi vinaonaonekana kama matumizi mabaya ya fedha lakini kwa mawazo yangu nafikiri vinachangia kurudisha pesa mtaani.
 

KEIKEI

Member
Jun 17, 2009
24
0
Sababu ulizoainisha, ukosefu wa ajira na mfumko wa bei ndio za msingi kwa ugumu tunaokabiliana nao kwa sasa. Bahati mbaya hatuoni mikakati ya madhubiti ya kisera kukabiliana na hizi chamgamoto. Sana sana tunaishia kupewa takwimu zakupika!
 

Baba V

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
19,500
2,000
Labda sijakuelewa mleta mada uliposema BILA KUINGIZA SIASA, kwani sidhani kama tunaweza kujadili haya mambo bila kugusa siasa za nchi yetu, vinginevyo tutakua tumeamua kujadili huku tuki ignore kwa makusudi sehemu muhimu ya mjadala, ambapo hatutafikia suluhisho muafaka
 

Fursa Pesa

JF-Expert Member
May 30, 2012
3,345
2,000
Kwa mtazamo nilionao yawezekana yafuatayo yanachangia kwa kiasi kikubwa;
1.Utashi wa watawala kushindwa kuamua juu ya namna ipi itumike kuwajaza watu pesa mifukoni.
2.Utashi wa wananchi kushindwa kuamua juu ya namna gani wao wenyewe wanapaswa kuishi kwa maana ya mtu mmojax2
au jamii nzima.
3.Sera,mashinikizo na misukosuko kutoka nje.
4.Ile hali ya kutokuwa na uthubutu katika jambo fulani (kukata tamaa ya maisha).
 

adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
11,209
2,000
Hakuna ubishi kuwa hali ya maisha imekua ngumu hapa nchini kwetu. Bila kuingiza siasa, hebu kama great thinkers tujaribu kuangalia kwa mapana kuhusu matatizo tunayokabiliana nayo kwa sasa, ambayo ndo hasa yanachangia ugumu wa maisha.


1. Mfumuko wa bei
2. Ukosefu wa ajira

Nini kifanyike?

Mkuu

Ugumu wa maisha umechangiwa kwa kiasi kikubwa na kushindwa kwa sera za CCM

a) mikakati mingi isiyo na vipaumbele na mingi ikiishia katika makaratasi bila usimamizi wenye tija.

b) Serikali kupoteza dira, kukumbatia majambazi na mafisadi na kuwatelekeza raia wake, (mapato hayaendi kupunguza ukali wa maisha bali kwa mafisadi)

Mikakati isiyonavipaumbele ni kama mtu analala usingizi hajui ataota ndoto gani, si rahisi kupata maendeleo endapo hakunamikakati ya muda mrefu kuutokomeza umasikini (hakuna sera yoyote yakueleweka kukuza ajira, viwanda ziii, kilimo ziii, mabilion ya kikwete kwa ndugu na jamaa nk)

Serikali imepoteza dira, imekuwa ya matapeli na mafisadi, imekuwa si ya kijamaa wala kibepari inaendeswa kwa nguvu ya wenye fedha na masikini hawana chao.
Kwasababu serikali imewekwa mikononi wa watawala/wanasiasa walafi, wako teyari kufanya kila liwezekanalo kuhujumu uchumi wa inchi ili watengeneze faida (mfano kubana mafuta na kuyapandisha bei watakavyo - mtoto wa upuuzi huu ndiyo huo mfumko wa bei.)

Nini kifanyike.

a) Tupate serikali ya kweli, serikali ya watanzania (wenyenacho na wasionacho) serikali itakayoweka uzalendo kwa watu wake kwanza.

b) Tupate serikali itakayokuwa na vipaumbele vichache na vyenyetija mfano.

i) Elimu

ii) Afya

iii) Kufufua viwanda vyote na kuanzisha vingine (Kuunganisha makundi ya vijana wenye elimu zao na kuwapa mitaji kuendesha viwanada vya ubunifu nk)

c) Ipatikane serikali itakayoendesha vita ya kweli dhid ya wezi na mafisadi wote kwa sababu hii ndiyo sabau kubwa ya umasikini wetu na kushindwa kwa mipango yetu mikataba mibovu, wanyama na madini kuporwa nk.
 

MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
7,932
2,000
Maisha magumu ni karibu kila nchi, ktk global
Hivyo kwa vile sisi ni subset wa global hili ni vigumu kuepuka ugumu wake kwa sababu. Wanaoleta mzunguko wa fwedha nchini wanamatatizo hivyo wamepunguza kuzileta kama vile kwenye utalii nk, na in return hata bidhaa hazinunuliki.

Nivigumu kuepuka hili janga kama nchi inazungurusha fedha tu za ndani ama mapato ya ndani tu, mfano unanunua mahindi mbeya unayauza shinyanga, hii ni kuzungurusha tu. Ni sawa na unakopa fwedha kwa Juma unalipa deni kwa George. unakopa kwa Donald unalipa kwa Juma.

Badala yake tunahitaji kuingiza fwedha kutoka nje ya nchi, ili uchumi uwe endelevu, na kwa vile tunategemea kuingiza kwa utalii na watalii wenyewe wamepata matatizo na kuingia mitini inabidi tubuni njia zingine za haraka kupata kunusuru na kuyafanya maisha ahueni.
Ktk mkoba wangu hapa nina ona njia nyepesi zaku-implement promptly ni A na B nazo ni.

A.Tufanye kilimo cha mass production cha mazao ya chakula na tuki export kwa nchi jirani, uwezo tunao, mashamba yapo ya kutosha, maji kila kona hadi ziwa malawi lipo.
B. Wawa rahisishie watanzania walio nje masharti na ikiwezekana wawazeshe kwa namna moja ama nyingine, ili wapate kuleta fwedha za kigeni nchini, mfano wa kuwawezesha ni
1. Wawape uraia wabongo wote
2.mfano serikali wanaweza kuwa na ka mgodi kao ka dhahabu harafu wanakuwa wananitumia mie mtanzania niliopo hapa nawauzia hapa ulaya kwa soko la kiulaya na si kwa soko la kiafrika kwa makubaliano ya kimahakama. Hii mbinu ndo wachina na serikali yao imewatoa sana.

/BR
 

blueray

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
2,218
0
Hakuna ubishi kuwa hali ya maisha imekua ngumu hapa nchini kwetu. Bila kuingiza siasa, hebu kama great thinkers tujaribu kuangalia kwa mapana kuhusu matatizo tunayokabiliana nayo kwa sasa, ambayo ndo hasa yanachangia ugumu wa maisha.


1. Mfumuko wa bei
2. Ukosefu wa ajira

Nini kifanyike?
Duh! Mkuu unataka kutuambia siasa haihusiki na ugumu wa maisha ya watanzania! Hii kweli ni great thinking!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom