Mnamo mwezi wa pili (tarehe siikumbuki) nilienda kutoa pesa Tawi la CRDB Chanika Mwisho kiasi cha milioni mbili. Basi baada ya kukaa foleni kwa muda mlefu nikafika dirishani, huku nje madalali wananisubiri nikalipie kiwanja kata ya Yondwe.
Kilichonikuta sitosahau. Kwanza yule dada anayenihudumia alikuwa amenuna sana pale kidirishani; namkumbuka alikua mweusi, akanipatia 5,000 tupu kiasi cha milioni mbili, mzigo huo. Nikamwambia anipe 10,000 akakataa.
Basi nikaona uvivu kuhesabu, kumbe dada kanipiga 20,000 kwenye ile pesa; kufika kule kwa mtendaji, 20,000 haipo.
Hawa wahudumu wa benki sio waaminifu,
Sent using
Jamii Forums mobile app