Mnamo mwezi wa pili (tarehe siikumbuki) nilienda kutoa pesa Tawi la CRDB Chanika Mwisho kiasi cha milioni mbili. Basi baada ya kukaa foleni kwa muda mlefu nikafika dilishani, huku nje madalali wananisubiri nikalipie kiwanja kata ya Yondwe.
Kilichonikuta sitosahau. Kwanza yule dada anayenihudumia alikuw amenuna sana pale kidirishani; namkumbuka alikua mweusi, akanipatia 5000 tupu kiasi cha milioni mbili, mzigo huo. Nikamwambia anipe 10000 akakataa.
Basi nikaona uvivu kuhesabu, kumbe dada kanipiga 20000 kwenye ile pesa; kufika kule kwa mtendaji, 20000 haipo.
Hawa wahudumu wa benki sio waaminifu, mnisamehe jamani kwa uandishi wangu mbovu. Si mnajua shule zetu kayumba?
Sent using
Jamii Forums mobile app