CRDB na fees zao...!?

Leo nilikuwa naperuzi account yangu ya CRDB through internet banking na nikashtuka kidogo na fees zao. Nimekutana na kitu kama ifuatavyo:

Monthly maintenance fee ........Tshs. 1,000
Card fee June ........................Tshs. 4,000 (hii transaction ya tarehe 9 July)
Card fee June ........................Tshs. 4,000 (hii transaction ya tarehe 13 July)
Withholding Tax .....................Tshs. 63.39

Nilikuwa sijanotice hivi vitax kwa muda na nashangaa kama huu ni utaratibu mpya. Kama wanamfanyia kila mteja namna hii, basi wanatengeneza faida ya hatari sana

...Ongeza na hizi:

-Maintenance fee 700/= ( nina hakika hii wameishapandisha!)
- Withdrawal fee 500/= ( pia nadhani imeishapanda!)
- Visa ATM Charges 2000/-
- Mimi binafsi nina cheki ya shs 30,000/- ambayo huingia kila Ijumaa kwenye Account yangu na inapoingia tu jamaa wanachukua 1,500 kama Commission na mimi kubaki na 28,400/= kwa maana hiyo katika 120,000/= ya kila mwezi jamaa wanavuta 6,000/= zangu kama commission yao mbali na makato yote hayo mengine!! Dah. Naanza kufikiria sana kuhusu kuweka hela zangu chini ya Godoro!

-
 
Hata mie nilikuta makato ya 4000 mara mbili eti ni card fee...Nilitaka kuwafuata kuuliza kuhusu hili suala. Ila kama ni gharama za visa card, kulikuwa na sababu gani ya msingi ya kukata mara mbili??

...Mimi Hii ya June Card Fee wamenikata mara tatu yaani 4,000/= x 3 = 12,000/= ! Jamani hapa sasa ninadhani tunapaswa ku-MULIKA MWIIZI!!
 
...Mimi Hii ya June Card Fee wamenikata mara tatu yaani 4,000/= x 3 = 12,000/= ! Jamani hapa sasa ninadhani tunapaswa ku-MULIKA MWIIZI!!


Kama ni hivyo basi kuna tatizo kubwa.....


Hawa jamaa wameshazoea kwamba watu wengi hawaangalii bank statements zao. Ndo maana vijana wengi wanaofanya kazi kwenye mabenki hawasiti kuanza mchezo wa kujichukulia kidogo kidogo kutoka kwenye accounts za watenja wao!!
 
Mimi nilitaka kwenda kumfungulia mwanangu JUNIOR ACCOUNT CRDB, mbona mmeanza kunitisha jamani? Nimfungulie bank gani tena?

mnunulie hisa ama umnulie fixed asset inayo appriciate value kuliko benki za hapa kwetu Tz wamezidi wizi!
 
Mkuu usijisumbue tu kuwapigia, hakuna kilichokosewa hapo!
Hiyo buku kama alivyosema mdau hapo juu ni fee ya internet banking, mi nilishawahi kuwauliza wakaniambia hivyo. Halafu hizo buku nne nne ni gharam ya card yao (8000 kwa mwaka), sema tu wamekata in two instalments. Hiyo 63.39 ni kodi ya TRA

Inamaana hiyo buku unakatwa hata kama hautumii huduma ya internate
 
...Mimi Hii ya June Card Fee wamenikata mara tatu yaani 4,000/= x 3 = 12,000/= ! Jamani hapa sasa ninadhani tunapaswa ku-MULIKA MWIIZI!!

You see? hapa kuna tatizo aisee. Inawezekana utaratibu wa buku 4 hauna lengo la kutimiza ile 8,000/= Fee ya mwaka kama imevyokuwa suggested na wadau wengine. CRDB wameanza tabia mbovu aisee. Siku hizi wanacharge 1% ya kila amount ya US$ unazowithdrawal
 
mnunulie hisa ama umnulie fixed asset inayo appriciate value kuliko benki za hapa kwetu Tz wamezidi wizi!

I wish ningweza kufanya hivy Shine, tatizo ni hela za kudunduiza, yaani zinapatikana mdog mdogo so ni km nataka kumwekea akiba akifikia umri wa kusoma at least kuna chochote cha kumsaidia.
 
Inamaana hiyo buku unakatwa hata kama hautumii huduma ya internate

Kama hutumii wakati ume-subsribe utakatwa tu, ila kama hautumii kwa maana kwamba huja-subscribe basi hautakatwa
 
...Ongeza na hizi:

-Maintenance fee 700/= ( nina hakika hii wameishapandisha!)
- Withdrawal fee 500/= ( pia nadhani imeishapanda!)
- Visa ATM Charges 2000/-QUOTE]

Withdrawal fee nadhani ni Tshs. 1,000/= (not so sure) maana sijawithdrawal physically muda mrefu sasa. Yaani gharama za hawa watu zimeanza kuwa juu na kama alivyosema mdau mmoja, inawezekana kuna ujanja flani umeingizwa.
 
Back
Top Bottom