CRDB mnazingua sana na ATM zenu!

CONSTRUCTIVE THOUGHT

JF-Expert Member
Jul 10, 2015
1,158
417
Kimsingi nimechoka kuwavumilia CRDB katika huduma yenu ya Automatic Teller Machine (ATM) ambayo imekuwa ni jambo la kawada kwa Benki hii kukata mtandao katika ATM kuanzia mida ya saa kumi na mbili hadi saa mbili na nusu usiku (18:00pm - 20:30pm) hasa katika Jiji la Mwanza.

Ukataji huu wa Mtandao (Network) katika ATM za CRDB umekuwa ukifanyika si chini ya siku tano kwa Wiki bila kuangalia ni siku za kazi au za mapumziko.

Sio jambo geni kwa ATM kupeteza mtandao (Network) hata katika ATM za Mabenki mengine, lakini kwa CRDB ni jambo ambalo lipo kwenye mpangilio wa kazi (sababu ni kuanzia muda mmoja kila siku ya kukata Mtandao). Yawezekana kuna sababu za kiufundi (financial planning strategies) katika utendaji.

Hivyo, kama ni sehemu ya utaratibu wa kazi, kwanini msitaarifu wateja wenu kuwa kuanzia mida ya saa kumi na mbili hadi saa mbili na nusu hakuna huduma za ATM? Kwa kufanya hivyo, mtakuwa waungwana sana kuliko kukaa kimya katika jambo ambalo linaleta usumbufu, hasira na hasara kwa wateja.

Binafsi nimechoshwa na tabia hii (kukata mtandao / Network) katika ATM za CRDB kwani imenisababishia:
1. Kuchelewa na hata kupata hasara katika Biashara zangu kwasababu ya kushindwa kuchukuwa pesa kwa wakati napo ziitaji kwaajili ya kununulia mzigo wa Biashara.
2. Kuhairisha Safari sababu nimeshindwa kutoa pesa za nauli katika ATM za CRDB.
3. Kumchelewesha mgonjwa (Mjamzito) Hospital kwa ajili ya kujifungua sababu nilishindwa kutoa pesa kwenye ATM kwa ajili ya nauli ya Tax.
4. Kuonekana muongo mbele ya mama mkwe na familia nzima baada ya kutoa ahadi wanisubili nifate pesa, sikurudi sababu nilishindwa kutoa pesa katika ATM za CRDB.
5. Na leo nalala njaa kwasababu nimeshindwa kutoa pesa mtandao unazingua.

Sioni sababu ya kuendelea kuwa Mteja wa hii Benki, kesho hasubui naanza kubeba kila kilicho changu (pesa zote) kutoka Benki hii naenda kuanza maisha mapya katika Benki nyingine, siwezi kuteseka wakati pesa ninayo.

Samahani sana kama takuwa (CRDB) nimewakwaza!!!
 
Mi huwa nashangaa Benki za bongo kama hao CRDB wana andika nje ya ATM zao et service ni 24 hours, wakat hata masaa 12 tu kufanya kazi bila shda huwa ni mara chache na nyingi usiku mnene znakuwa hazina kitu.
Nchi zetu za dunia ya 3 hatukp siriaz kabsa.
 
yaani ATM ziinazingua weekend, mwisho wa mwezi, sikukuu... Namba za simu zilizowekwa hazipokelewi baada ya saa 12 jioni na bado wanakumbia ni 24hrs. Simbank nayo inazngua yaani taabu tu asee
 
Back
Top Bottom