CRDB kwenye huduma ya simbanking hamko serious

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,580
7,944
Kama kuna CRDB bank employees ujumbe huu naomba muufikishe kwa mabosi wenu.
Network yenu haieleweki, wiki iliyopita network kwangu ilizingua ndani ya siku kama 3 hivi kila nikijaribu bilabila, ikatulia kwa siku kadhaa leo najaribu tena niweze kurekebisha maisha yangu network hamna.

Yaani hata kutazama salio mpaka niende bank zama hizi.
-Na ma ATM yenu yanasumbua sana hasa tarehe za mshahara.
-Makato makubwa kwa huduma ya kuhamisha fedha kwenda kwenye mitandao ya simu.
 
Wana maneno yao yana nikela eti siku nzima wana rekebisha mitambo!!
 
Kama kuna CRDB bank employees ujumbe huu naomba muufikishe kwa mabosi wenu.
Network yenu haieleweki, wiki iliyopita network kwangu ilizingua ndani ya siku kama 3 hivi kila nikijaribu bilabila, ikatulia kwa siku kadhaa leo najaribu tena niweze kurekebisha maisha yangu network hamna.

Yaani hata kutazama salio mpaka niende bank zama hizi.
-Na ma ATM yenu yanasumbua sana hasa tarehe za mshahara.
-Makato makubwa kwa huduma ya kuhamisha fedha kwenda kwenye mitandao ya simu.
Hiyo bank ina slogan yao eti "the bank that listens" they should change to "the bank that LISTENED" hapo wala hawatakusikiliza ndg.
 
Wana jamvi mimi yamenikuta. Niko Kigoma ugenini, nikajifanya kutoa hela CRDB kwenda mpesa ili niitoe kilaini. yaliyonikuta ni balaa. Kwanza ilitoka halafu ikakataa kuja Mpesa, nikawasiliana nikaaambiwa ipo hewani na itarudi benki ndani ya saa 24. Sasa masaa 24 yamepita naambiwa nisubiri masaa mengine 24. Naomba ushauri jinsi ya kufungua madai maana hapa nimeshapata damage kubwa balaa. Tahadhari iwe kwako pia. Asante.
 
CRDB online banking nao wana mambo yao flaniflani ya ajabu. Kuna vijimakato vingi visivyo na maelezo ya kuridhisha.
 
unapofanya miamala ya kielectronic uwe na tahadhali kubwa hasa maeneo ambayo netwok iko chini au inayosua sua
 
Wana jamvi mimi yamenikuta. Niko Kigoma ugenini, nikajifanya kutoa hela CRDB kwenda mpesa ili niitoe kilaini. yaliyonikuta ni balaa. Kwanza ilitoka halafu ikakataa kuja Mpesa, nikawasiliana nikaaambiwa ipo hewani na itarudi benki ndani ya saa 24. Sasa masaa 24 yamepita naambiwa nisubiri masaa mengine 24. Naomba ushauri jinsi ya kufungua madai maana hapa nimeshapata damage kubwa balaa. Tahadhari iwe kwako pia. Asante.
Mi yalinikuta hayo, nikaambiwa niandike barua, afu nisubiri ka wiki 2 ivi, afu ndo ilikua hela ya nauli nipo stendi.
 
Niko Kigoma ugenini, nilijifanya kutumia huduma tajwa hapo juu, yamenikuta makubwa na nimepata damage kubwa sana kibiashara na kimaisha hapa ugenini. Hela ilitoka crdb lakini ikashindwa kuingia kwenye MPesa. wakasema itafanikiwa ndani ya saa 24, haikuwezekana, sasa wana sema nisubiri saa 24 zingine.

Nipeni mwongozo wa kudai damage.
 
Mimi mbona hua inafanya kazi vizuri tu. Hizo ni hitilafu za mifumo ya kompyuta na si kweli kuwa utapoteza fedha yako,itarudi tu. Isipokua hilo la kwamba umepata hasara kwa kufeli kwa huduma ya SIM Banking hapo nenda kawadai wala usianzie kwa wakili nenda tu kaongee nao wakibisha ndo nenda upate ushauri wa wanasheria.

Ila uwe unaweza kuthibitisha hyo hasara bila shaka
 
Back
Top Bottom