Huduma ya CRDB Simbanking ni ovyo na imejaa kero

Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
26,117
34,077
Habarini za asubuhi Wadau,

Kwa wateja wa CRDB kuna hii huduma ya SIMBANKING, yaani ufanyaji mihamala kwa njia ya simu. Kwa sasa huduma hii kwa CRDB ni hovyo sana na usiiamini tena huduma hii

Natumia huduma ya Cardless kwasababu sins ATM Card nasubiri kutoka kwao, sasa tangu juzi natoa pesa kwa njia ya simbanking kuna namba za siri wanapaswa kukupa sehemu ya kwanza na ya pili.

Sasa upumbavu unakuja pale unapotoa hela utashangaa wanakuletea namba ya sehemu ya kwanza tu au ya sehemu ya pili tu (ni mara ya 5 sasa na huwa nawafuata dirishani).

Hapa nipo stand nasubiri kusafiri nikajaribu tena huduma hiyo holaa, nikajaribu kutoa kwa Wakala wanasema CRDB mtandao haupo.

Ukimpigia mhudumu anakuambia update Simbanking App na bado inakataa.

KERO nyingine kubwa ni kwamba ukijaribu kuwapigia ndio kabisa hawapokei simu.

Crdb kama mpo huko ninyi mmekuwa kero, mna matangazo mengi ya huduma ila hakuna chochote.
 
Utakuwa umepatwa tu na bahati mbaya ya kutosha , kwa kawaida huwa haisumbui sana.
Tumia app yao ipo smart kuliko app zote za bank nilizotumia hapa Tanzania.
 
Utakuwa umepatwa tu na bahati mbaya ya kutosha , kwa kawaida huwa haisumbui sana.
Tumia app yao ipo smart kuliko app zote za bank nilizotumia hapa Tanzania.
Mkuu tangu juzi natumia App yao na nimeiupdate jana usiku, nimeona App haimalizi muamala wa kutoa pesa nikaamua kutoa kwa njia ya kawaida *150*03# still imegoma
 
Mkuu tangu juzi natumia App yao na nimeiupdate jana usiku, nimeona App haimalizi muamala wa kutoa pesa nikaamua kutoa kwa njia ya kawaida *150*03# still imegoma
Mi natumia app tena hii waliyo update majuzi ambayo unaweza i customize ukatumia fingerprint badala ya pin.
Asubuhi hii nimefanya muamala wa sampuli hiyo hiyo yako kupitia app na imemaliza.
Inawezekana kuna shida la mtandao hapo ulipo huwa inatokea.
 
Inatokea mara mojamoja..ila ukipiga simu huduma wa wateja wanakutumia namba zilizomiss..japo mpaka simu ipokelewe ni kasheshe.

SimBanking app iko poa in my opinion.
 
sjajua lately shida ni nini ila imeanza kusumbua since last week. otp haziji..otp inakuja after one hr. opt kuwa na two factor authentication via mail. yani zile otp zije kwenye email.
 
Inatokea mara mojamoja..ila ukipiga simu huduma wa wateja wanakutumia namba zilizomiss..japo mpaka simu ipokelewe ni kasheshe.

SimBanking app iko poa in my opinion.
Umejaribu kutumia ndani ya wiki mbili zilizopita?
 
Back
Top Bottom