CRDB Kitengo cha Refunds Acheni wizi

Vipi mkuu, walikurudishia. I have the same problem nimekutumia sms inbox
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi mkuu, walikurudishia. I have the same problem nimekutumia sms inbox

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimesoma hii thread mwanzo mwisho. Pia nimewahi kupambana Sana na CRDB kupata refunds zangu ....same same scenario Kama mtoa mada alivyozungumzia mwanzo. Kwa kweli ni shida na inachukua muda kupata refunds zako tofauti na benki zingine.
Tatizo nililoliona kwenye hii thread ni kwamba imevamiwa na watu wasio na uelewa na PayPal refund inavyofanya kazi kwa nchi Kama Tanzania. Kwa hiyo wapo mahususi kupinga kwamba CRDB hakuna tatizo .......tatizo lipo kwa wateja ( nawaonea huruma kwa uelewa finyu na hawataki kujiongeza kufuatilia kuelewa tatizo).
Mwisho kabisa ukisoma mtiririko wa wachangiaji wengine wa mwishoni mwishoni utaelewa wanafanana fanana na wafanyakazi wa CRDB. Wao wanajifanya ni wakarimu na wanasisitiza mtoa mada na wengine wenye tatizo Kama Hilo wawasiliane kupitia contact centre yao ( Sasa najiuliza hawajasoma vizuri thread kujua kwamba hii contact centre haipo efficient ama? Au wameshaboresha?)
Kuna jamaaa anaitwa undertaker .......ukisoma post zake utacheka na kumuonea huruma kwa jinsi anavyojizalilisha kwa kuwa na uelewa finyu. Huku akijigamba yeye ni mfanyakazi wa benki. Kama huyu ni staff wa CRDB naombeni niwape pole. Mpigeni msasa Tena kwenye Mambo matatu; ajifunze refund process mahususi inayo involve pay pal, customer care na flexibility ya kujifunza. Bila hivyo atazidi kuwaangusha.
Mwisho kabisa na kwa Nia njema kabisa wafunisheni wafanyakazi wenu wasichangie chochote kwenye social media, wawepo watu maalum wa kujibu Mambo ya kwenye mitandao baada ya kupitia kwa umakini na kuelewa mada inayozungumzwa. Kila mtu akijibu yeye anavyojua HESHIMA ya taasisi kuharibika kwa muda mfupi ni rahisi Sana, maana lazima watatofautiana na wengine watatumia lugha chafu zitakazowakwaza wateja. Na mwisho wajuvi wa Mambo wanaweza kutafisiri kwamba benki Mnafanya trolling/ spinning makusudi.

NIHITIMISHE KWA KUSEMA TATIZO LIPO KWENYE REFUND ZA PAY PAL, CUSTOMER SERVICE PIA INAHITAJI MABORESHO, MUDA MNAOUTUMIA KURUDISHA HELA KWENYE ACCOUNT NI MREFU KULINGANISHA NA WASHINDANI WENU.

NINI KIFANYIKE?
FUATULIA PROCESS MWANZO MWISHO KUBAINI SHIDA IPO WAPI? MAANA PAYPAL WAKI REFUND HELA INATAKIWA KU HIT ACCOUNT MOJA KWA MOJA MOJA.

MBILI, BORESHA CHANNELS ZENU ZA MAWASILIANO. SIO MTU AFUATILIE JAMBO MOJA HADI MARA NANE NA KUPEWA JIBU LILE LILE KWAMBA TATIZO LAKO LINAFANYIWA KAZI.
 
Kifupi PayPal kwa Tanzania tunaruhusiwa tu kulipia sio kupokea pesa kupitia PayPal .Tanzania haijaruhusu Hilo .tumepiga kelele Sana humu kuwa turuhisiwe watanzania kupokea pesa kupitia PayPal Lakini Serikali haitaki inataka tuwe tinalipia tu.Maajabu ya dunia

Kupokea pesa iwe refund or whatever from PayPal hairuhusiwi.Mnawalaumu.bure CRDB
 
Umejibu kiprofessional sio ki-"return of undertaker"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…