CRDB ichunguzwe kunatatizo kubwa sana mahali,

CRDB ichunguzwe kunatatizo kubwa sana mahali,

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Posts
1,792
Reaction score
2,421
hii imekuwa kawaida kuwa na malalamiko ya kukosa weredi hasa siku za karibuni ilivyozidi kujitanua,
Swala la rushwa kwenye utoaji mikopo ya watumishi na wajisilia mali limekuwa la kitaifa zamani nilizani ni simiyu tu kumbe ni konection kutoka juu, hii si siri tena wafanyakazi wa uma usipotoa rushwa inafikia wanaanza hadi kukatwa makato ya mwezi lakini hawajaupata mkopo. Wakati matangazo yao yanaonesha ni kupata mkopo ndani ya masaa 48 tu bila rushwa inachukua mpaka miezi kadhaa,

pamoja na kuwepo na taasisi nyingi za kifedha, CRDB iliwavutia wakopaji kwa kuwa na viwango nafuu zaidi vya riba 18% kwa mwaka nakutokuwa na garama nyingine nyingi za ziada ukilinganisha na benki zingine na taasisi zingine za kibenki, na hiki kimewapa wafanyakazi wake kiburi cha kuomba rushwa na kuwazungusha wateja wake kwa makusudi
pamoja na hayo huduma zao za cm bank zinasuasua muda mwingi hazifanyi kazi,
 
Shida bank zote ziko ivo ivo , mtu unakaa mwezi mzima hujapata mkopo ila makato tayali, RUSHWA.
 
rushwa kwao si adui wa haki bali kisukumio haraka, usipotoa utacheleweshwa au kunyimwa kwamba huna vigezo.
 
hameni huko mbona bank zipo nyungi tu

wanariba ndogo kuliko nmb ila huduma kwa wateja sasa ni sifuri, Makato yao yako chini kila fedha yako inasamanicrdb riba ni 18 tena riba ya kushuka nmb sasa ni 20% na nmb wana bima kubwa na garama za mkopo kubwa ila sasa nmb huduma kwa wateja kwenye mikopo hakuna longolongo
 
Aisee. Poleni ila njoo uku nmb tunakopa fresh tu bila mizengwe. Ila mleta mada kwenye wiwani yangu nimeona kitu cha doubt, inaonekana kuna mahala umekwama ila unaleta mada kwa njia ya ujanja. Sijawahi kuona au kusikia popote tangazo la mkopo wa crdb ndani ya masaa48. Niliwahi kuomba mkopo kwao na hatimaye nilishalipa wote, nilikwama mpaka nikahisi natapeliwa then nkaamua kwenda kwa manager.
Meneja aliniambia wala vijana hawajakukwamisha, akavuta likitabu na kunifunulia utaratibu wao. Kweli kuna mahala niliona kwa sisi tulioko mikoani lazma mkurugenzi wa mikopo makao makuu asaini. Ems kutoka uku kwenda dar kwa njia ya posta ikitumwa leo inafika keshokutwa, alaf kama unakopa kwa dhamana ya ardhi lazma wafanye mortgage kwa afisa ardhi wa wizara ya ardhi. Alisema ata mkopo wa kawaida ukichukua siku chache ni 7 days. Na mkopo WA ardhi ndio usiseme. Iyo Biashara niliyotaka kufanya ilishakaribia mwisho yani mpaka napewa iyo 50m tayari ilishaharibika.
Nilichojifunza ni kuwa ukitaka mkopo kwenye mabenki omba mapema ila sio leo Kesho unataka hela.
Kidooogo nmb walinikopesha kwa kuonesha hati ya kimila na kadi ya GARI tu!!
Vinginevyo kama kuna jipu litumbuliwe!!
 
pole ndugu kwa upande wa NMB naona wao wako vizuri kwenye utoaji mikopo mimi leo asubuhi nilirudisha fomu yangu baada ya kusainiwa sehemu zote wilayani,asubuhi nimeipeleka mida ya mchana naangalia nakuta tayari wameishaniingizia mkopo wangu niliouomba.
 
hii imekuwa kawaida kuwa na malalamiko ya kukosa weredi hasa siku za karibuni ilivyozidi kujitanua,
Swala la rushwa kwenye utoaji mikopo ya watumishi na wajisilia mali limekuwa la kitaifa zamani nilizani ni simiyu tu kumbe ni konection kutoka juu, hii si siri tena wafanyakazi wa uma usipotoa rushwa inafikia wanaanza hadi kukatwa makato ya mwezi lakini hawajaupata mkopo. Wakati matangazo yao yanaonesha ni kupata mkopo ndani ya masaa 48 tu bila rushwa inachukua mpaka miezi kadhaa,

pamoja na kuwepo na taasisi nyingi za kifedha, CRDB iliwavutia wakopaji kwa kuwa na viwango nafuu zaidi vya riba 18% kwa mwaka nakutokuwa na garama nyingine nyingi za ziada ukilinganisha na benki zingine na taasisi zingine za kibenki, na hiki kimewapa wafanyakazi wake kiburi cha kuomba rushwa na kuwazungusha wateja wake kwa makusudi
pamoja na hayo huduma zao za cm bank zinasuasua muda mwingi hazifanyi kazi,

Kuna bwana moja anaitwa Isaya Lymo yuko kwenye mikopo anakula rushwa ile mbaya.... Tafadhali CRDB mchukulieni hatua huyu mtu
 
Hii ya kuanza kukatwa malipo ya mkopo kabla ya kupata mkopo mbona ni uzembe wa hali ya juu! Crdb bank ifanyieni kazi hii.
 
Back
Top Bottom