CRDB DODOMA BRANCH hii sio haki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CRDB DODOMA BRANCH hii sio haki

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by SOKON 1, Jul 2, 2011.

 1. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,115
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  CRDB dodoma branch haiwezekani maelfu ya wanafunzi dodoma kuhudumiwa kupitia dirisha mojo uku wale ambao sio wanafunzi kuhudumiwa kupitia madirisha sita kwani huku ni kupotezeana muda kwani ukienda madirisha mengine wanakataa.
  My take:
  CRDB bado tuko safarini kama leo hii mnawatenga kumbuka kesho watakapo maliza masomo yako kuja kuwa wateja wenu itakuwa ngumu kwa kukumbuka mateso waliyowapata wakati mlipokuwa mmewagawanya kimatabaka. Ila kwa kuwa fair nusu ingekuwa wanafunzi na yanayobaki wengine.
  Nawasilisha
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Aaaaaaa,nilipokua dodoma nilijuuuuuta,sina hamu na huduma za kibenki dodoma hasa wanapokuwepo wanafunzi,kama unaharaka unaweza kupanda basi hadi moro........yaani mteja hugeuka mtumwa...halafu huyo mama meneja wa benki kama hajui kinachoendelea anasema wanafunzi huwa wanakuwepo kwa msimu hivyo hakuna haja ya kuongeza TAWI,hivi hawajui kama mji unapanuka huooooo.loh
   
 3. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,115
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  sema kweli wanakera wanakuwa kama hawana macho ila wameamua kutufanya watoto ila siku zote ili kumbakisha mteja ama kuongeza wateja ni jinsi gani ulivyomuhudumia mwanzo ila sisi sote waelewa lakini kwa hili sio haki kutojali mda wa mtu wakati mistari mengine watu wachache.
   
 4. Ikumbilo

  Ikumbilo JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 455
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wewe unemwandikia Mkurugenzi wao Dr.Kimei angelipatia ufumbuzi suala lako. Unajua kuna mameneja wengine wanadharau sana wanafunzi utafikiri nao hawakuwa wanafunzi.
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Wazo zuri sanaaaaaaaa......
   
 6. Ikumbilo

  Ikumbilo JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 455
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mie nakumbuka jamaa alinisaidia sana wakati CRDB tawi fulani walikuwa wananizingua. Baadaye aliwauliza kuhusu huyo mteja ndipo jamaa walinitafuta kweli, simu zilipigwa kila wakati. Nilipofika walinihudumia kama sio yule nilikuwa nazungushwa.
   
 7. samito

  samito JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 621
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  lakin wanafunz benk yenu si ipo udom? mi naona ni poa tu, mana wanafunz smtime mnapenda kuja mjin bila sabb za msing na ku2sababishia wengine jam isiyokuwa na mana, CRDB dodoma nawaunga mkono kwa kuwawekea dirisha moja, hii inawasaidia wao binafsi kupunguza matumizi hasa safar za mjini, mana inawa discourage ku acces acont zao pind wawapo mjin. big up.
   
 8. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  We mbinafsi kweli. Mteja ni mteja tu. Maana hiyo policy haipo kwenye bank ya CRDB ni maamuzi ya manager husika kudiscriminate unfairly and unlawfully. Kila mtu ana uhuru wa kutumia kipato chake vyovyote aonavyo inafaa. Halafu uelewa wako wa wanafunzi ni mdogo sana. Unahisi kama wanafunzi ni watoto ambao wanatakiwa kupangiwa nini wanafanya kwa muda gani.


  Asilimia kubwa ya wanafunzi waliopo vyuoni wamefikia umri wa utu uzima (18 years) na wengine unaweza kukuta ni babu au bibi zako. Pia wengine wana kipato kuliko hata wewe na wengine wana familia zao. Hivyo si watu ambao unawapangia kuwa sasa hivi ni muda wa kulala, sasa hivi ni muda wa kwenda tuition, sasa hivi nenda prep, sasa hivi hakuna kutoka chuo. Kwa maana hiyo huwezi kuwadiscourage kwenda mjini kwa kuwaweka kwenye foleni muda mrefu.

  CRDB top management sijui kama wanashare vision na wafanyakazi wa huku mikoani. Maana hii benki wanafanya ubunifu mwingi sana kuwa market leaders lakini wanakwamishwa sana na wafanyakazi ambao akili zao nimelala, wanaowaza kizamani bila kujua biashara ya benki ina ushindani sana kwa sasa.
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Sidhan kama hilo tawi la udom ni kwa ajili yao......ameshakuwa mteja wao basi ahudumiwe kana wengine.......kwa waliofika UDSM,mwanafunzi anaweza kuhudumiwa campus,mabibo au mlimani city au tawi lolote lile,je hao wa udom wakija town kuna makosa,sasa na makao makuu yanakuja taratibu mji wa dodoma utaweza kuwahudumia wakazi wa dodoma na wageni........,maana hata mitaa ya dodoma kwa sasa unaikuta imefurika watu,jamaniii
   
 10. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hivi hapo dodoma kuna benki moja? Kwanini msihame? Halafu huyo mama anayesema wanafunzi ni wa msimu alitakiwa atengeneza mfumo ambao ungemonitor demand yake na kuwa na wahudumu wengi kwenye peak na wachache kwenye low peak. Hapa haijalishi mwanafunzi au mtu wa kawaida wote wanahitaji huduma sawa. Mie nina kadi yangu toka uanafunzi inamaana nikienda hapo wataniita mwanafunzi?
   
 11. T

  TumainiEl JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 2,894
  Likes Received: 1,649
  Trophy Points: 280
  Amieni NBC MPATE HUDUMA BORA! Watanzania achane Lawama.
   
 12. T

  The Priest JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 1,026
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  ada wanalipia crdb bana....
   
 13. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #13
  Jul 2, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,115
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  dodoma kuna vyuo vingi ukiacha udom je na hao wengine waende wapi?
   
 14. m

  mob JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2013
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  mkuu hawa jamaa walinikera sana kuna cku nimezunguka benki zao zote tatu hapa dodoma yaani dodoma branch, chamwino na udom nakaambulia kupoteza mafuta ikanibidi nihamie DTB ambayo haina foleni wewe ni kwenda kudeposit fast na ikikuta ndani kuna foleni unaenda kwenye meza ya maulizo anakuongoza mdada hadi kwenye ATM zao unaweka fedha palepale CRDB nimebakiza kutumia ATM zao tu kupitia master card ya DTB
   
 15. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2013
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,556
  Likes Received: 1,313
  Trophy Points: 280
  Dhambi hii ya utengano ndio inawatesa airtel na Vodacom hadi leo. Mwanzo waliwadharau watumiaji wa mtandao wa tigo wakauita mtandao wa wanafunzi wakasahau mwanafunzi akimaliza anakua mfanyakazi na haachii line yake.

  CRDB wasipoangalia itawakumba. NMB wanalijua hilo pia namna gani wanafunzi wanawakimbia pindi wanapomaliza masomo.
   
Loading...