CRDB Bank na kinachoendelea?

ndenga

JF-Expert Member
Dec 20, 2010
1,795
1,310
Ni nini kimeisibu benk yetu hii pendwa,

Napenda kutoa angalizo kwa Benki Yetu iliyokuwa pendwa ya CRDB. Benki hii imejijengea mtandoa mpana na hata kwenye faida katika soko la banki nchini imekuwa ikifanya vizuri sana kwa takribana zaidi ya milongo miwili iliyopita.

Ila kilichosababisha niliete angalizo hili, ni kwa tabia ya hivi karibuni ambayo benk hii imekuwa ikipoteza network ya system zao za ATM and simbanking kwa muda mrefu na bila kutoa maelezo ya kinachoendelea. Kwa takriban mwezi mzima wa tano na Huu wa sita benki hii imekuwa ikipotea hewezani kiasi kwamba wateja wake wanashindwa kupata huduma zote za kibenki, hii inajumuisha huduma za ATM na SimBanking

Naomba wahusika wakisoma hapa watoe maelezo, maana kwa kadri siku zinanyoenda hii bank naona inaendelea kupotea kabisa kwenye kutoa huduma nzuri za kibenki.

Kwa mfano leo huduma ya Simbank na ATM hazipo hewani tangu saa saba mchana na hakuna majibu na sitegemei kama watatoa maelezo yoyote katika hili.

Jamani tubadilike CRDB
 
Kesho tutawaona wakiitisha Press Conference na waandishi wa habari!!
 
Hawa jamaa wanakera sana..Hakuna maelezo... Hata kwenye ATM zao kwa siku za hivi karibuni wamekuwa wakiweka note za 5000 tu.. elfu kumi hakuna
 
Kuna ATM ilikuwa pale ABLA APARTMENT inaweza ikakaa hata wiki mbili bila kuweka pesa...Mitaa ya Sinza ndio kabisa
 
Sitasahau walichonifanyia hao crdb kwenye tu-hela twangu twa mboga... Nimeshahama kwa sasa niko na mafukara wenzangu NMB
 
Siku zote kama huduma ikipotea tupate maelezo, waige Tanesco...Lakini ikizidi inabidi tujiulize
 
Mimi nilikuwa na mpango wakufungua acc/ kumbe wana matatizo hayo? Mbona mmenitisha sana sasa naogopa.
 
Kuna shida na hivi account kuu za taasisi za serikali imehamishiwa BOT.
 
Tuwe wakweli mimi sio mshabiki wa crdb plc wala Md wao. Siku zote ni amini baada ya Kimei ukweli wa crdb plc utajulikana.
Ukitaka juwa crdb plc chini ya Kimei ipo shida angalia mchezo wanafanya kwenye soko la hisa. Tangu wameingia soko la hisa wao wanacheza na tsh350-450 sina kumbukumbu ikiwa wamewahi fika hisa 500-700 tangu wapo sokon. Pia angalia hisa ya nmb imeshuka sana ipo 1800 na imewah kupanda mpaka ~3600.
Njoo kwenye ghawio ndio utachoka tzs 5 sijuw kumi wakati nmb plc mpaka ~116. Sasa ajabu nyingine jamaa kwenye soko hisa zake ndio kama hvyo ila ajabu faida anatangaza unajiuliza wanakokotoaje p&l yao.
Kingine angalia uwekezaji wao. Wao wanafungua matawi kwenye nchi ambazo ni high risk kama kongo, burundi na unawasikia wanajivunia uwekezaji wao.
Huyo ndio crdb plc chini ya Md Kimei. Ila pia ths tm wanakazi nzito kuficha mambo yao chini ya serikal ya Magufuli.
 
Nilienda kwenye ATM ya Barclays (VISA) kutoa hela ikagoma na hapo mfukoni nina buku 4 tu dah, majanga.
 
Yaani, nlitaka kuhamisha hela kwa simbanking ili ninunue umeme hola.....
 
Ni kweli, sio simbanking na atm pekee bali hata ndani ya bank ni tatizo, one week ago kwa ck 3 ilikuwa tatizo kubwa
 
Tuwe wakweli mimi sio mshabiki wa crdb plc wala Md wao. Siku zote ni amini baada ya Kimei ukweli wa crdb plc utajulikana.
Ukitaka juwa crdb plc chini ya Kimei ipo shida angalia mchezo wanafanya kwenye soko la hisa. Tangu wameingia soko la hisa wao wanacheza na tsh350-450 sina kumbukumbu ikiwa wamewahi fika hisa 500-700 tangu wapo sokon. Pia angalia hisa ya nmb imeshuka sana ipo 1800 na imewah kupanda mpaka ~3600.
Njoo kwenye ghawio ndio utachoka tzs 5 sijuw kumi wakati nmb plc mpaka ~116. Sasa ajabu nyingine jamaa kwenye soko hisa zake ndio kama hvyo ila ajabu faida anatangaza unajiuliza wanakokotoaje p&l yao.
Kingine angalia uwekezaji wao. Wao wanafungua matawi kwenye nchi ambazo ni high risk kama kongo, burundi na unawasikia wanajivunia uwekezaji wao.
Huyo ndio crdb plc chini ya Md Kimei. Ila pia ths tm wanakazi nzito kuficha mambo yao chini ya serikal ya Magufuli.

Mkuu nakubaliana na wewe. Kwenye soko la hisa hawa jamaa mwenendo wao sio mzuri. Mimi ni mteja wao kwenye maeneo mengi lakini naona kuna vitu haviko clear sana. Sijui Kimei anacheza mchezo gani. Mimi mwenyewe hapa bado najiuliza maswali mengi....and I may decide otherwise !!
 
Back
Top Bottom