Covid - mfumo wetu wa kupima Korona hauwafai watalii...

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,586
4,271
Kwa Muda sasa nimekuwa nafuatilia mfumo wetu wa kupima covid (PCR) nikaona unawafaa watu ambao hawana haraka au hawana tatizo la muda kitu ambacho sio rafiki kabisa kwa utalii
1. Tulitangaziwa kuwa majibu kwa Dar/ Arusha mikoa yenye Lab yatatoka Ndani ya saa 24 kitu ambacho, ukiuliza lab wanatoa majibu ndani ya saa 24 kuanzia pale wameyapokea Sample hivyo logistic au muda gani sample inatumia kuwafikia haiwahusu hivyo kiuhalisia, majibu hayatoki ndani ya saa 24 ( watalii wangejulishwa tu ni saa 48) ili wasiteseke kupiga simu mara kumi kumi wakifuatilia matokeo na pengine kuachwa na ndege
2. Ukitoka nje ya mikoa husika, majibu yanatoka ndani ya saa 72 hii ina maana siku moja + ya kusafirisha na siku moja + ya kuchakata
3. Hakuna huduma ya Express; Hivi ina ingia akilini, mtalii atoke Mahale, Ruaha, Nyerere Np, Katavi nk halafu umuambie aje Dar/Arusha akae masaa 48 akisubiri Majibu ya Covid??
4. Napendekeza iwepo huduma ya Express ( MASAA SITA TU MTU ANAPATA MAJIBU kwa kulipia ziada mfano mara mbili ya bei. Mbona wenzetu wanayo, tunashindwa wapi?
5. Hivi unawezaje kufikiri tutapanua utalii mikoa ya kusini ( Mahale, Ruaha, Katavi na Nyerere NK wakati hatuja weka mfumo WOWOWOTE wa kupima au pengine hata hiyo express ili watalii wakifika dar saa 11h00 wapime na kupata matokeo yatakayo wawezesha kuondoka na ndege ya jioni
6. Hakuna mfumo wa kupokea maombi ya watu/ wageni wenye shida ya express test result (Kila mtu ni boss kuanzia hospitali hadi Lab) yaani tunafukuza watalii wenyewe!!!
7. Wenzetu Kenya wana weka centre za kuchukua sample kwenye park zao simple tu kwa kama shs 10mil za kitanzania, sisi gharama ya kuweka centre tuna kadiria 40mil. Makampuni ya watalii yapo taabani serikali inasubiri eti waandae Centres?? yaani ni sawa na kusubiri kukamua ngombe ambaye hujampa majani na majani yenyewe hakuna/kampuni nyingi zimejifunga kwa kushindwa kujiendesha watatoa wapi hela ya kuchangia?
8. Inaniuma sana jinsi vijana wengi walivyo jaa mitaani bila ajira kwenye Utalii na hakuna jitihada za kutia matumaini ili kuokoa jahazi zaidi ya kusikia tozo zinapandishwa. Hivi huwa hatuma wataalamu wa masoko wa kushauri?
9. Hadi Leo Serengeti Np tuna centre moja tu ya kuchukua sample? Masaimara ( Kenya) ambayo ni kama robo ya serengeti wana centre zaidi ya 10; Tuna hangaika kukimbizana na wamachinga walipe kodi wakati tunaweza kuimarisha mfumo wa utalii tuka kusanya pesa kiurahisi
 
Back
Top Bottom