COVID-19 : Naibu Waziri wa Afya aipongeza JamiiForums kwa elimu iliyotukuka

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
72,865
2,000
UELIMISHAJI UMMA KUHUSU - CORONAVIRUS_ NAIBU WAZIRI AIPONGEZA JAMIIFORUMS - Naibu ( 536 X 640 ).jpg


Dr Faustine Ndungulile ambaye ni Naibu Waziri wa Afya ameipongeza na kuishukuru Jf kwa uchambuzi makini na kuelimisha Jamii kuhusu Ugonjwa wa Corona .

Hii ni heshima kubwa sana kwa Wanachama wote wa JF

Wito: Tuendelee kuelimisha wananchi wenzetu namna bora ya kujikinga na Corona .

Mungu ibariki JF

======

UELIMISHAJI UMMA KUHUSU #CORONAVIRUS: NAIBU WAZIRI AIPONGEZA JAMIIFORUMS

Naibu Waziri wa Afya nchini Tanzania, Dkt. Faustine Ndugulile kupitia Instagram ameandika “Nawapongeza sana JamiiForums kwa kutoa elimu sahihi kwa Umma juu ya Ugonjwa wa Corona kupitia Mitandao ya Kijamii”.

Amesema, “Kuna upotoshaji mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ugonjwa wa Corona (Covid19). Hali inayopelekea kujenga hofu na unyanyapaa kuhusu ugonjwa huu katika jamii.”

#JFCOVID19_Updates
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
9,143
2,000
Asante na pongezi JamiiForums kwa mchango wetu ambao unatambulika ktk kusambaza na kupashana habari nyingi za kina zilizo sahihi ikiwemo hizi za gonjwa la CoVid - 19 linalosababishwa na virusi vya coronavirus.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom