Covid-19 imetikisa biashara ya Utalii duniani

Covid-19 imetikisa biashara ya Utalii duniani

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,353
Wakati majira ya kiangazi yanakaribia nchi nyingi zinazotegemea utalii kama sehemu ya mapato ya ndani zimeanza kufikiria mbinu za kuongoza biashara bila kupoteza kabisa soko.

Cyprus
Wanaruhusu watalii wanaoingia na cheti cha maabara kilichotolewa ndani ya siku nne mpaka msafiri anapoingia. Cheti hicho kithibitishe kuwa mgeni hana maambukizi ya corona.

Serikali pia imetenga majengo ya kukarantine wageni watakao patikana na maambukizi katika kipimo kitakachofanyika Airport. Mizigo yote itapuliziwa dawa za kuuwa wadudu ( disinfectant).

Wageni watakao ruhusiwa kuingia Cyprus kwa utalii ni wale ru wanaotoka katika nchi zenye rekodi nzuri ya kupambana na corona. Nchi za Scandinavia. Umoja wa Falme za Kiarabu, Ugiriki na Israel.

Ureno
Hutaingia hotelini mpaka zipite saa 24 tangu mgeni aliyetoka amekabidhi chumba hotelini.

Hakuna kuota jua ufukweni mwa bahari kwenye vitanda vya jumuia.

Ukiwa unatafuta hoteli mtandaoni utaona daraja la usafi wa hoteli.
 
Acha tu mkuu imetupiga sana kwetu nadhani ni Zero kwasasa mapato ya utalii.
Ninaangalia hatua zilizochukuliwa na nchi nyingine ili wasikose soko. Ugiriki wamesema baa hazitafunguliwa wala disco. Hapa unajiuliza maana ya holiday ni nini kama hakuna bar wala disco?
 
erikali pia imetenga majengo ya kukarantine wageni watakao patikana na maambukizi katika kipimo kitakachofanyika Airport.
Sidhani kama kuna mtu wa ku-take all that trouble kisa KUTEMBEA maana hata unakokwenda utaambikizwa pamoja na kupima kwenu kuwa uko salama! WHY ALL THAT TROUBLE!... labda kwa vile ni wazungu maana nimeshangaa USA wanaghabika eti hawajaend beach na kuruhusu tu kidogo, eh! wamejazana!
 
Sidhani kama kuna mtu wa ku-take all that trouble kisa KUTEMBEA maana hata unakokwenda utaambikizwa pamoja na kupima kwenu kuwa uko salama! WHY ALL THAT TROUBLE!... labda kwa vile ni wazungu maana nimeshangaa USA wanaghabika eti hawajaend beach na kuruhusu tu kidogo, eh! wamejazana!
Kwa wazungu holiday inasaidia mental health wellbeing. Wao hawasafiri kwenda nyumbani Kigoma, mama anaishi kwenye council flat hapo hapo mjini.
 
Tanzania: Hakuna lockdown kwa watalii Wala kupimwa Wala karantini wako huru muda wote watakaokuwepo hapa.
 
Kuna article nimesoma mahala eti Tanzania imefungua utalii katikati ya janga la corona kuokoa uchumi unaoenda kuanguka.
 
Kuna article nimesoma mahala eti Tanzania imefungua utalii katikati ya janga la corona kuokoa uchumi unaoenda kuanguka.
Hayo mheshimiwa rais ameyasema tena hawatapimwa wala hakuna karantine
 
Wat skunks ndugu wa CCM Wachina
Nipo kwenye Biashara hii inayohusu watalii kwa muda sasa, kabla hata ya kuja hua wanaulizia kujua hali ikitokea majibu wameyakosa mtandaoni..

Nami kwa kulinda kazi yangu nawajibu ukweli...narudia tena kwa mwenendo wetu tukae tutulie..labda iishe worldwide

sent from Samsung Galaxy A30
 
Back
Top Bottom