Mwali, huyu Ray Charles hakuwa mwimbaji wa COUNTRY MUSIC. Yeye alikuwa zaidi kwenye JAZZ, R&B etc.....
Mie pia ni mpenzi mzuri sana wa Country music. Don Williams nikianzia, Kenny Rogers, Dolly Parton nk hadi hizi New SH*t za sasa ambazo kila sehemu zimevamia na kuharibu muziki. Kwa wapenzi wa Old School, mpitieni pia Reba Mcentire na huyu dada Wynona JUDD (mama pia ni Actor mzuri tu).
1.
Reba McEntire - Starting Over Again - YouTube Reba Mcentire (Starting over again).
2.
Wynonna Judd - It's Never Easy To Say Goodbye - YouTube
Sasa tuje kwa Don Williams, OMG. Unaanzia Senorita, Gyps Woman, You are my best friend, kwa kweli zipo nyingi sana.
Ninazopenda kwa sasa na kwa sababu zimepigwa na jamaa wengine na kupigwa vizuri sana ni hizi hapa chini;
3. Huyu mama ni Mwimbaji mzuri sana wa Gospel na hapa anachukua wimbo wa Don Williams na kuubadilisha na kuanza kumwimbia mtu wa pili (Mwanaume) maana yeye ni Mwanamke. Wimbo safi sana na ukiweza basi utafute kwenye Youtube wimbo wa Don Williams ..
I`m just a Country Boy Don Williams.mpg - YouTube
4. Wimbo wa Don Williams, it must be love :
Don Williams - It Must Be Love - YouTube
Baadaye akaja mwimbaji maarufu kwa sasa na mpenzi pia wa Don Williams na akauimba tena...
Ila nikiri kuwa katika mambo yaliyonishangaza ni kumuona Don Williams akiwa Zimbabwe a kufanya Concert kama mbili au tatu hivi. Nilipata bahati ya kununua DVD Concert yake ambayo nafikiri Ebay waweza kuibahatisha mara moja moja. Yeye pia alishangaa sana kukuta nyimbo zake zinapendwa sana Africa na alikuwa anafikisha sehemu anaacha kuimba na watu wanaimba hiyo sehemu. Poa zaidi walipomuomba aimbe SENORITA na wakamsaidia kuimba kwa furaha. Enzi hizo BLACK and WHITE in Zim walikwua kitu kimoja. Ukiweza kuipitia hii Video ya mwisho, poa sana.
I can't stop loving you - Ray Charles...
(you'd fall in love with who ever you are dancing with, lol)