Country Music

Country Music

AnyWayZ

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2022
Posts
4,885
Reaction score
8,482
Kwetu Tanzania tunazo Zilipendwa za akina Les Wanyika na Wengine wengi, lakini hao wote bado ni wa juzi tu

Marekan wanayo "Country Music" hii ni ya kitambo zaidi.
Ni tamu
Ina maadili pia
Ina hisia kali.
Na waimbaji wake ni watu wenye fikra pana na chanya katika Maisha

Binafsi nampenda sana Kenny Rogers aliyeimba The Gambler, Coward of the County, Lucille na nyingine nyiiingi.

Lakini naukubali zaidi wimbo wa Don Williams "I believe in you"

Upo Wimbo unaitwa "Remember when" uloimbwa na Alan Jackson, huu wimbo ni sehemu kubwa ya kumbukumbu za maisha yang ya utoto, ujana na nataman niishi uzee wangu katika njia hiyohiyo kwa maana ndiyo Furaha yangu.

Unafahamu nini kuhusu Country Music?
Unamfahamu nani kwa undani?

Umewahi kujifunza nini kupitia wimbo gan?

Nataman kujua zaidi kupitia ninyi ebu funguka.

View attachment 2275442View attachment 2275443View attachment 2275441
Screenshot_20220628-143414_1.jpg
 
Unaonekana wa long sema kuna hii genre ya country-pop huwa naipenda sana ya vijana wapya

Kwa country zaman kuna hii ya John Denver- Take me home, country roads... nikiwa narudi nyumban mkoan huwa inanipa hisia kali sana...

Music 🎶 una nguvu ya kubadili hisia kwa haraka, waliimba hata hawa band ya country
Lady Antebellum- what a song can do
 
Unaonekana wa long sema kuna hii genre ya country-pop huwa naipenda sana ya vijana wapya

Kwa country zaman kuna hii ya John Denver- Take me home, country roads... nikiwa narudi nyumban mkoan huwa inanipa hisia kali sana...

Music [emoji445] una nguvu ya kubadili hisia kwa haraka, waliimba hata hawa band ya country
Lady Antebellum- what a song can do
Yeah hawa wa kisasa pia wakali aga nawasikiliza wapo makin sana, Lakin naona dunia haiwapi sikio sana, unadhan kwanini?
 
Country sio zilipendwa ni aina muziki ambayo had sasa bado ipo na kuna wanamziki wa kizazi hiki wanaimba country music kama Brett Young, Brad Paisley, Carrie Underwood, Kacey Musgraves, Keith Urban, Katie Armiger, Kelsea Ballerini, Gabby Barrett, Tucker Beathard nk
 
Dolly Parton ~Coat Of Many Colours My Mother Made For Me
Mambo Ya Nguo Kuweka Viraka Yalianza Kitambo
Huo wimbo ni true story yake mwenyewe na aliwahi kuieleza kwenye tv interview moja miaka mingi kidogo nyuma.

Yeye ametoka kwenye familia masikini sana na wazazi hawakuwa hata na uwezo wa kuwanunulia nguo, kwa hivyo mama yake akipita kwa mafundi vyerehani na kuomba vipande vya vitambaa ndiyo akiwashonea makoti ya baridi.

Alipokuwa akilivaa basi watoto wenzake shule wakimcheka sana, na aliporudi nyumbani kumueleza mama yake ndiyo akamwambia kuwa Jesus aliwahi kuvaa a coat of many colours. Na yeye aliamini kabisa lakini alipokwenda shule kuwaambia wenzake bado walikuwa wanamcheka.

Alikuja kuelewa baada ya kuwa mtu mzima maana ya ile hadithi ya mama yake ilikuwa ni kumpa moyo kuliko kumwambia kuwa familia haikuwa na uwezo wa kuwanunulia nguo.
 
Ana Vocal Kali Sana Akiiimba Sambamba Na Kenny Rogers
You Got Night!!!
 
Country sio zilipendwa ni aina muziki ambayo had sasa bado ipo na kuna wanamziki wa kizazi hiki wanaimba country music kama Brett Young, Brad Paisley, Carrie Underwood, Kacey Musgraves, Keith Urban, Katie Armiger, Kelsea Ballerini, Gabby Barrett, Tucker Beathard nk
Hivi Lionel Richie tunamueka genre ipi ya Musik maana aga naona anaswagg za aina mbalimbali sana
 
Country ni mziki wa shamba. Ukiendelea kuusikiliza utakuwa hushiki pesa. .
Mziki wa matajiri unaujua 😃 unaitwa claasical music such as Opera

Hata mie namkubali sana sana Allan Jackson, Don Willium and Kenny Rogers my three favorite country musicians. Ila mdogo wangu anayenifuata yuko too deep ananiambiaga hao bado sana😃
😃😃
 
"Alipokuwa akilivaa basi watoto wenzake shule wakimcheka sana, na aliporudi nyumbani kumueleza mama yake ndiyo akamwambia kuwa Jesus aliwahi kuvaa a coat of many colours"

Jamii ya hawa watu wengi huwa na Iman ya Kikristo? Maana hata nyimbo zao zinakua na Points za Imani.
 
Country ni mziki wa shamba. Ukiendelea kuusikiliza utakuwa hushiki pesa. .
Mziki wa matajiri unaujua [emoji2] unaitwa claasical music such as Opera

Hata mie namkubali sana sana Allan Jackson, Don Willium and Kenny Rogers my three favorite country musicians. Ila mdogo wangu anayenifuata yuko too deep ananiambiaga hao bado sana[emoji2]
[emoji2][emoji2]
Duuuh, Anamaanisha wapo wakali zaid? Eb elezo kidogo juu ya hiyo Classical mkuu
 
Kwetu Tanzania tunazo Zilipendwa za akina Les Wanyika na Wengine wengi, lakini hao wote bado ni wa juzi tu

Marekan wanayo "Country Music" hii ni ya kitambo zaidi.
Ni tamu
Ina maadili pia
Ina hisia kali.
Na waimbaji wake ni watu wenye fikra pana na chanya katika Maisha

Binafsi nampenda sana Kenny Rogers aliyeimba The Gambler, Coward of the County, Lucille na nyingine nyiiingi.

Lakini naukubali zaidi wimbo wa Don Williams "I believe in you"

Upo Wimbo unaitwa "Remember when" uloimbwa na Alan Jackson, huu wimbo ni sehemu kubwa ya kumbukumbu za maisha yang ya utoto, ujana na nataman niishi uzee wangu katika njia hiyohiyo kwa maana ndiyo Furaha yangu.

Unafahamu nini kuhusu Country Music?
Unamfahamu nani kwa undani?

Umewahi kujifunza nini kupitia wimbo gan?

Nataman kujua zaidi kupitia ninyi ebu funguka.

View attachment 2275442View attachment 2275443View attachment 2275441View attachment 2275444
Country ni muziki unaoimbwa na watu wa kusini mwa marekani,,
Ni genre kama ilivyo pop, hip hop, jazz and zingine
Hata sasa hv still bado kuna watu wanaimba Country wengi tu kama brett young
 
Siri ni nini naona country music inaimbwa na watu ambao umri umeenda hivi
Me nadhan ni mtazamo tu wa vijana kutoendana na lifestyle ya Country, Japo wapo waloimba tangu ujana mpaka wakazeeka na wapo vijana wa sasa wanaimba.
 
Back
Top Bottom