Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,222
- 10,730
They see me rollin'
They hatin'
Patrollin' and tryna catch me ridin' dirty
Tryna catch me ridin' dirty
Kwa wale wahenga haya mashairi yanawarudisha mbali sana, miaka ya 2006, ambapo mashairi haya yalikuwa ni kama wimbo wa dunia haswa sehemu za disco, aliyeimba wimbo huu wengi wanamfahamu kwa jina la Chamillionaire, nyota ambaye alitupatia dude zito sana kwa jina la “Ridin’ (Dirty)” dude ambalo lilikuwa likipigwa basi ndio tutajua utimamu wa DJ kwenye kuchezea deck vizuri.
Ukweli ni kuwa wimbo wa “Ridin’ (Dirty)” ulipata mafanikio makubwa sana ndani ya Marekani pamoja na dunia kwa ujumla, Chamillionaire alipata show nyingi sana ndani ya Marekani, pamoja na nchi za Karibea.
Bwana mdogo alipata deals za pesa ambazo zilimfungua akili ya biashara mapema sana mzee baba na kutazama upande wa pili, upande wa kuwekeza pesa kwenye biashara zaidi haswa teknolojia.
Michongo na simu ambazo Chamillionaire alipigiwa zilimfanya aanze kushtuka mapema isije kuwa kama ya MC Hammer ya kufilisika.
Chamillionaire alichagua upande tofauti. Katika mahojiano ya 2015, alikiri wazi kwamba “hanywi pombe wala havuti sigara wala bangi,” msimamo uliompa nidhamu ya kuweka malengo ya kifedha nje ya muziki wake.
Uchumi wa Chamillionaire haukujengwa kwa hisia tu bali kwa maamuzi magumu; ukichangiwa sana na akili kubwa na mikakati yenye ubunifu ndani yake. Tangu mapema aliingia kwenye biashara ya magari kupitia kampuni yake ya Fly Rydes Kustom Toy’z, Chamillionaire hakutumia magari yake kutembelea mtaani kuonesha jeuri ya pesa bali aliumiza kichwa na kuamua kugeuza magari hayo kuwa mali zinazozalisha pesa na faida.
Alitengeneza mifumo na connection na kuanza kuazimisha magari hayo kwa wasanii wengine wakati wa kurekodi picha mjongeo za nyimbo zao. Huo ndio upekee wake: badala ya matumizi aligeuza nafasi ya biashara; badala ya anasa, akatengeneza mapato.
Kama alivyonukuliwa: “Tutafanya video na kukodisha aina zote za magari… badala ya watu kupoteza pesa, waje wakodishe kwangu kwa bei nafuu.”
Aliwahi kuhojiwa na kituo kimoja cha Redio kuwa cheni na vito vya thamani anavyovaa vina gharama kiasi gani, Chamillionaire alicheka na kuwaambia kuwa, vitu vyote hivi sio vyangu, nimeviazima kwa ajili ya kufanyia video kisha ninarudisha, kiukweli vina gharama kubwa sana ila thamani yake ni bora kuigeuza katika biashara.
Chamillionaire hakuishia tu kwenye biashara ya magari, alikuwa miongoni mwa wawekezaji wa mwanzo wa Maker Studios, na baadaye kuuzwa kwa The Walt Disney Company mwaka 2014 kwa dola milioni 500. Uamuzi wa Disney kununua Maker Studios ulimfanya mwamba kuwa moja ya marapa waliokwenda sambamba na gari la mshahara.
Chamillionaire akatuliza kichwa na kuona upepo wa kuwekeza kwenye teknolojia ya magari (self driving car) kupitia Cruise Automation. Baada ya kuonekana ni moja ya teknolojia bora ya magari, Kampuni ya General Motors ilinunua Cruise mwaka 2016 kwa thamani iliyoripotiwa kuzidi dola bilioni moja—mauzo haya yalimpa bwana mdogo jina la King Rapper of Timings, kwani ni kama malaika wake alikuwa akimsanua mapema kuwa aweke pesa sehemu fulani ili baadaye apige mpunga mwingi.
Chamillionaire ni mtu wa ajabu sana, alikuwa ana uthubutu wa kipekee sana, kwani muda mfupi tena aliwekeza pesa kwenye teknolojia ya usalama wa majumbani kupitia Ring (zamani Doorbot), kipaza sauti-cha-mlangoni kilichogeuka na kuwa moja ya teknolojia bora sana ya “smart home.”
Kampuni ya Amazon ilinunua Ring mwaka 2018 kwa takribani dola bilioni moja— hii ikawa ni sehemu nyingine ya matunda bora ya uwekezaji mzuri wa Chamillionaire.
Kwa nini simulizi yake ni muhimu kwa wasanii wa leo? Kwa sababu historia ya muziki ina vitabu vizito vinavyoeleza namna vipaji vilivyogeuzwa hadithi za umasikini kutokana na mikataba mibovu, matumizi mabaya ya kupita kiasi, na kutojifunza misingi ya biashara mapema katika maisha.
Donald S. Passman, katika kitabu chake cha All You Need to Know About the Music Business, anabainisha kwa lugha nyepesi jinsi mikataba, “royalties,” na mapato ya “streaming” vinaweza kumkandamiza msanii asiye na uelewa; ni “biblia yenye lugha nyepesi” kwa yeyote anayetaka kuepuka mitego.
Mwisho wa siku, Ridin’ (Dirty) ni kumbukumbu ya ushindi wa muziki; mafanikio ya Chamillionaire ni ushahidi wa ushindi wa akili na utimamu wa maisha. Katika tasnia ambako majina mengi husikika kwa mwaka mmoja kisha kutoweka.
Chamillionaire ameandika sura ya pekee—msanii aliyebadili midundo kuwa hisa, “hooks” kuwa haki miliki, na mistari kuwa mtaji. Hiyo ndiyo tofauti ya hadithi ya kuongelewa wiki moja na urithi wa kuishi vizazi.