EasyFit
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 1,269
- 1,082
Tumekuwa tukihesabu miezi wiki siku hatimaye masaa kutimia muda wa siku 90 waliopewa wanaodaiwa magamba ndani ya CCM wajipime na kujiondoa wenyewe ikibidi watalazimishwa kuondoka lakini hadi kufikia count 0hrs hakuna ayejiondoa au aliyewalazimisha kuondoka.
Je nini hatima ya wanaotakiwa kuondoka na wanaotaka wenzao kuondoka na hatima ya chama kwa ujumla.
Maoni yangu inawezekana kwa vile waliambiwa wajipime wenyewe labda wamejipima na kuona hakuna sababu ya wao kuondoka.
Vile vile kwa upande mwingine wanaowataka wenzao kuondoka labda nao wamejipima wakaona hawana sababu za msingi kuwataka wenzao kuondoka.
Nini mawazo yako.