Cosmological truth; death

Cosmological truth; death

Tatizo lako wewe unalalamika wala hutoi hoja kupinga haya tuyasemayo.

Uislamu ni Qur'aan na Hadithi,sasa nakupa ushahidi kutoka kwa viwili hivyo juu ya uwepo wa maisha ya Kaburini.

Nanukuu :

Maisha ya kaburini ni kile kipindi anachokaa mtu baada ya kufa kwake mpaka kufufuliwa kwake. Kipindi kati ya parapanda la kwanza ambalo ni amri ya kufa viumbe vyote na parapanda la pili ambalo ni amri ya kufufuliwa viumbe vyote vitakavyotakiwa vifufuke, Huitwa Barzakh. Tunajulishwa kuhusu Barzakh katika Aayah ifuatayo:

“Mpaka yanapomfikia mmoja wao mauti, husema: Mola wangu Nirudishe”,
“Ili nitende mema sasa badala ya yale niliyoyaacha. Wapi! Hii ni kauli aisemayo yeye tu. Na nyuma yao kipo kizuizi mpaka siku watapofufuliwa”. [Al-Mu-uminuwn: 99-100].

Katika kipindi hichi cha maisha ni mambo gani yanayoendelea katika nafsi ya mwenye kufa? Wengi kwa kujiliwaza katika wakati huo hufikiria kuwa watu wanakuwa mapumzikoni. Na watu ambao hawaamini siku ya mwisho huamini kuwa kifo ndio mwisho wa maisha ya watu na iliyobaki ni kuoza na kuwa chumvi chumvi zitakazotumika ardhini.

Katika kipindi cha Barzakh roho za watu wema zitakaa pahali pazuri kungojea malipo yao ya Peponi, Ama zile za watu waovu zitakuwa mahabusu zikingojea siku ya hukumu yao. Hivi ndio tunavyojifunza katika Hadiyth zifuatazo:

Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesimulia kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambae alisema: “Hakika maiti hupelekwa kaburini na hukaa kaburini bila ya khofu wala fadhaa. Baada ya hapo ataambiwa: “Ulikuwa katika nini? Atajibu: “Muhammad Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitujia na hoja zilizokuwa wazi kutoka kwa Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) na kwa hivyo tulimuamini. Ataulizwa tena “Umemuona Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala)?, Atajibu: “Si katika uwezo wa yeyote kumuona Allaah (‘Azza Wa Jalla). Kisha patawekwa uwazi utakaomuonyesha moto unaofoka. Kisha ataambiwa angalia kile ambacho Allaah Amekuokoa (Amekukinga nacho). Kisha patawekwa uwazi utakaomuwezesha kuiona Pepo na pia vyote vilivyomo ndani yake. Ataambiwa: “Hii ni sehemu yako kutokana na Uthibiti wa Iymaan uliyoishi nayo hadi kufa nayo na ambayo utafufuliwa nayo in shaa Allaah”.
Ama kuhusu mtu muovu yeye atakaa katika kaburi lake kwa khofu na fadhaa. Ataulizwa: Ulikuwa katika nini? Atajibu sijui. Kisha ataulizwa tena: Ni nani huyu? Atajibu nilisikia watu wakisema kama nilivyosema. Kisha utawekwa uwazi kwa kumuwezesha kuiona pepo ataangalia na kuona uzuri wake na vilvyomo ndani yake. Ataambiwa: Angalia kile ambacho Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Amekukosesha (Kutokana na Iymaan yako mbovu). Kisha utawekwa uwazi wa kumuwezesha kuona na ataambiwa hii ndio sehemu yako ambayo uliendesha maisha yako kwa kuwa na mashaka nayo, Na umekufa ukiwa na mashaka nayo na utafufuliwa ukiwa katika hali hiyo hiyo, in shaa Allaah”. [Ibn Maajah].

Pia tunapata Hadiyth nyingine kutoka kwa Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) amesimulia kuwa:
“Mwanamke wa kiyahudi alimwendea na kumsimulia adhabu ya kaburi, Akamwambia; Allaah Akukinge na adhabu ya kaburi. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam) akajibu; “ndio”, Adhabu ya kaburini ni jambo la kweli: ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) alisema: Sikumuona Mtume baada ya hapo kuswali Swalah yoyote bila ya kumuomba Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Amkinge na adhabu ya kaburini”. (Al-Bukhaariy na Muslim).

Pia tuangalie katika Hadiyth ifuatayo inatueleza nini juu ya maisha ya Kaburini.

Bara’a bin ‘Aazib amesimulia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam) akisema:
“Malaika wawili watamjia (maiti), Watamkalisha na kumuuliza: Ni nani Bwana wako? Atajibu: Allaah pekee Ndiye Bwana wangu. Kisha watamuuliza tena, Ni nani huyo aliyeletwa kwenu? Atajibu: Alikuwa ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam). Watamuuliza tena; Amekuleteeni habari gani? Nimesoma kitabu cha Allaah nikaamini kutokana nacho na nikaithibitisha ‘Iymaan hiyo (katika matendo)”.
Na pia tuangalie Kauli Yake Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Asemavyo katika Kitabu Chake kuwa:
“Allaah Huwatia imara wenye kuamini kwa kauli ya imara katika maisha ya dunia na katika Aakhirah. Na Allaah Huwaacha kupotea hao wenye kudhulumu. Na Allaah Hufanya Apendavyo”[Ibraahiym: 27]
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam) akasema:
“Mtangazaji (mwenye kunadi) atatangaza (atanadi) kutoka mbinguni: Hakika mja Wangu amesema ukweli. Mtengeeni sehemu Peponi na mvisheni mavazi ya Peponi, Na mfungulieni mlango wa Peponi. Kisha utafunguliwa. Akasema Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam) na hewa ya Peponi na harufu yake nzuri ya manukato itamjia na Pepo itakurubishwa kwake kiasi cha upeo wa macho. Ama kwa kafiri asiyeamini, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam) alitaja kifo chake na akasema: Roho yake itarudishwa katika kiwiliwili chake na Malaika wawili watamjia, Watamkalisha na kumuuliza: Ni nani Bwana (Mola) wako? Atajibu: Haa! Haa! Sijui! Watamuuliza tena: Ni ipi dini yako? Atajibu: Haa! Haa! Sijui! Kisha watamuuliza ni nani huyo aliyeletwa kwenu? Atajibu Haa! Haa! Sijui! Kisha mwenye kunadi atanadi kutoka mbinguni: Hakika amesema uongo, Kwa hiyo mkunjulieni kitanda cha motoni. Akasema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam) Kisha joto lake na upepo wa moto utamjia na kaburi lake litakuwa jembamba sana kwake mpaka mbavu zake mbili zitapishana.
Kisha atakabidhiwa kwa Malaika kipofu na kiziwi mwenye pande (rungu) la chuma, Kama mlima ungelipigwa na chuma hicho ungelikuwa vumbi. Atampiga kwa chuma hicho kwa kipigo ambacho kitasikika kwa kila aliye mashariki na magharibi ispokuwa viumbe wa aina mbili (Majini na Watu) hawatasikia. Atakuwa vumbi na kisha roho itarudishwa tena kwake.” (Ahmad na Abu Daawuwd).

Hivi kusadiki kwa jambo au kuwepo kwa jambo mpaka wewe ulione kwa macho au ? Mbona bado uko nyuma sana kielimu ?

Sijasema mpaka ulione. What I said ni kwamab hata icho kitabu chako unachosoma cha dini akijasema kaburini kuna Adhabu wala maisha. Toa aya yako hapa tuione as a theory atleast tuanze kuijadili. Wewe umetoa wapi hii kauli kaburini kuna adhabu na maisha? Utaniambia hadithi za mtume, BS ,kwenda zako.
 
Halafu umenifanya nipitie post zako ili nijue Level yako ya elimu Na kufikiri. Maana Sio kwa mavi mavi haya unayoandika.

Mayahudi waarabu sijui nini that is all you know eeenh ? Napenda sana kudebate na critical thinker as a part of learning. But wewe kwako sijifunzi kitu, unapoteza muda na ukapige Ramli this is not your level

Safi sana. Ila siamini katika Ramli,sasa unaniweka katika kundi gani ?

Lakini waambie walimu wako wakufundishe namna ya kujenga hoja na usiwe unakimbia maswali,tangu tuanze mjadala hujajibu swali langu zaidi ya lile linalo husu Hadithi.

Lakini mimi nimejifunza mambo kadhaa toka kwako ni kuwa hata kwenye Saynsi kuna story zisizo weza kuthibitishwa kwa misingi ya Sayansi yenyewe. Pili nimejifunza ya kuwa unatumia hisia kujua ukweli wa jambo,kitu ambacho hakitoshelezi. Tatu nimejifunza ya kuwa,mnaposhindwa hojanaleta tuhuma.

Nipo ....
 
Unaweza kuthibitisha kua nilipuliziwa roho

Naweza kukuthibitishia hilo. Soma hapa chini kwa mazingatio :

7. Ambaye ametengeneza vizuri umbo la kila kitu; na akaanzisha kumuumba mtu kwa udongo.
8. Na kisha akajaalia uzao wake utokane na kizazi cha maji madhaifu.
9. Kisha akamtengeneza, na akampulizia roho yake, na akakujaalieni kusikia na kuona, na nyoyo za kufahamu. Ni uchache mnavyo shukuru.
10. Nao husema: Tutapo kwisha potea chini ya ardhi, ni kweli tutarudishwa katika umbo jipya? Bali wao wanakanusha kwamba watakutana na Mola wao Mlezi.
11. Sema: Atakufisheni Malaika wa mauti aliye wakilishwa juu yenu; kisha mtarejeshwa kwa Mola wenu Mlezi. (as Sajdah : 7-11)

Huo mimi ushahidi wangu,sasa wewe naomba unithibitishie ya kuwa sisi hatukupuliziwa roho ?

Nipo ....
 
Sijasema mpaka ulione. What I said ni kwamab hata icho kitabu chako unachosoma cha dini akijasema kaburini kuna Adhabu wala maisha. Toa aya yako hapa tuione as a theory atleast tuanze kuijadili. Wewe umetoa wapi hii kauli kaburini kuna adhabu na maisha? Utaniambia hadithi za mtume, BS ,kwenda zako.

Inaonekana hujui hata aya ni nini ? Soma hayp maelezo humo kuna aya na kuna hadithi za mtume amani ya Allah iwe juu yake.
 
Inaonekana hujui hata aya ni nini ? Soma hayp maelezo humo kuna aya na kuna hadithi za mtume amani ya Allah iwe juu yake.

Zuri unapenda sana mabishano ya kwenye kahawa. Honestly have no time for that.
 
Naweza kukuthibitishia hilo. Soma hapa chini kwa mazingatio :

7. Ambaye ametengeneza vizuri umbo la kila kitu; na akaanzisha kumuumba mtu kwa udongo.
8. Na kisha akajaalia uzao wake utokane na kizazi cha maji madhaifu.
9. Kisha akamtengeneza, na akampulizia roho yake, na akakujaalieni kusikia na kuona, na nyoyo za kufahamu. Ni uchache mnavyo shukuru.
10. Nao husema: Tutapo kwisha potea chini ya ardhi, ni kweli tutarudishwa katika umbo jipya? Bali wao wanakanusha kwamba watakutana na Mola wao Mlezi.
11. Sema: Atakufisheni Malaika wa mauti aliye wakilishwa juu yenu; kisha mtarejeshwa kwa Mola wenu Mlezi. (as Sajdah : 7-11)

Huo mimi ushahidi wangu,sasa wewe naomba unithibitishie ya kuwa sisi hatukupuliziwa roho ?

Nipo ....

Huyu jamaa bhana haelewi kabisa. Halafu anapenda sana kutoa version of his distorted mind.
That is what you have been encrypted. Use your mind boy, stop tell us what they have taught you. Tell us what you think, unlock that part please.

Mimi I can’t debate with this boy.
 
Hili ni funzo kwenu pia muache kusoma mambo nusu na muwaambie wakubwa zenu wakiwafundisha wawe wanawapa misingi kwanza ya elimu husika kisha ndio wawafundishe na msiwe mnaleta story za Kisayansi ambazo mnashindwa kuzitetea mnapoulizwa maswali.

Tuko pamoja ....
 
Naweza kukuthibitishia hilo. Soma hapa chini kwa mazingatio :

7. Ambaye ametengeneza vizuri umbo la kila kitu; na akaanzisha kumuumba mtu kwa udongo.
8. Na kisha akajaalia uzao wake utokane na kizazi cha maji madhaifu.
9. Kisha akamtengeneza, na akampulizia roho yake, na akakujaalieni kusikia na kuona, na nyoyo za kufahamu. Ni uchache mnavyo shukuru.
10. Nao husema: Tutapo kwisha potea chini ya ardhi, ni kweli tutarudishwa katika umbo jipya? Bali wao wanakanusha kwamba watakutana na Mola wao Mlezi.
11. Sema: Atakufisheni Malaika wa mauti aliye wakilishwa juu yenu; kisha mtarejeshwa kwa Mola wenu Mlezi. (as Sajdah : 7-11)

Huo mimi ushahidi wangu,sasa wewe naomba unithibitishie ya kuwa sisi hatukupuliziwa roho ?

Nipo ....

Nakusubiria unipe uthibitisho!
 
Mwalimu mzuri Siku zote hatoi majibu bila kuonesha njia jibu kalipata vipi.
pamoja na kutoa majibu na njia lakini si kuna watu wanafeli?? je mwalimu huyo ikiwa ni mwenye uwezo wote wa kuwafanya wanafunzi wote wa faulu pasipo kufelisha ikatokea mwalimu huyo amefelisha robo ya darasa utaona si sahihi kwa wazazi kumlaumu mwalimu huyo??

Hayo inayo ita ni mahubiri ni Darasa kwako mwanafunzi, kama kunaambacho hujakielewa hapo kiseme, kama kuna unacho kipinga kipinge kwa hoja usikimbie mada kwa kuita facts ni 'mahubiri'.
Darasa unalolinadi nilishaona wanafunzi kutoka darasa hilo wote waki score zero, sasa kuna umuhimu gani mimi kwenda darasa hilo?? elimu inayotolewa darasani humo ni full hoax, mtu anafundishwa kua nyoka na binadamu walizungumza nae anakubali tu. Darasa linatoa elimu ya kizushi kua jua huzama matopeni, dunia ni bapa , mara jua huzunguka dunia WTF??? Labda mimi ndio niwe mwalimu wenu wa hilo darasa.
Nirudi kwenye swali ambalo nimeshalijibu....ila majibu umeyapuuza na kuita mahubiri ...
nimeyapuuza kwasababu si majibu
Mwalimu Kabla ya kutoa mtihani huwa darasa lake analijua vyema na wanafunzi wake anawajua vizuri vilaza anawajua

vilaza utawajuaje bila kuwapa mtihani wa majaribio??? utajuaje huyu kilaza na huyu si kilaza bila kuwapima kwa mtihani?

Unaweza ukaniambia nini lengo la mtihani mashuleni??

Wakali wa kuweka banda anawajua. Je ni sawa mwalim asitoe mtihani na badala yake achapishe matokeo vilaza awawekee "o" na Wakali wa darasa awawekee "100", Je mwalim huyu atakuwa katenda haki? Je alichofanya ni Sahihi?
Kwanza mwalimu huyu anauwezo wote na ujuzi wote pamoja na upendo wote? ikiwa kama kimoja kati ya hivyo hana basi haitakua sahihi kuhoji mapungufu yake.

Pili nataka nikuambie kua

mwalimu hana uhakika na wanafunzi wake na ndio maana anatoa mitihani ili kupata uhakika. Kwasababu hao vilaza wako katika hali ya kujifunza na kuna muda wanaweza kuwa juu zaidi ya hapo walipo sasa hapa ili mwalimu atambue kua huyu kapanda daraja yule kashuka inambidi atumie mtihani kama njia ya kujua
Jibu ni hapana
Je Mungu Mmoja, mpenda haki akafanya kama mwalimu huyo itakuwa ni Sahihi?
Jibu ni hapana
nimekuuliza na huyo mwalimu anakua na uwezo wa kuingia akilini mwa mwanafunzi kujua anachokiwaza huyo mwanafunzi?? Mungu huyu unayemfananisha na huyo mwalimu ndiye huyu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote???

Kwanini basi Mwalimu akifanya hayo ni kosa lakini hayo makosa ya Mwalimu unataka yawe ni sahihi kwa Mungu Mmoja kufanya?
sasa jiulize ikiwa kama tu mwalimu asiyekua na uwezo wote ujuzi wote na upendo wote akifelisha wanafunzi kizembe kazi yake inakua matatani, inakuaje mungu mwenye sifa ya ujuzi wote, upendo wote na uweza wa yote kuumba ulimwengu wenye mabaya wakati alikua na uwezo wa kuumba ulimwengu usioruhusu mabaya asishtumiwe kwa ujinga huu?
Mungu mmoja kukuuliza kila ulilofanya na wewe kukiri ndiyo mfumo wa Mahakama zote, iweje mfumo huyo tuukubali, lakini mfumo huo huo ukitimilizwa na Mungu Mmoja unakuwa ni makosa?
mahakama haina uwezo wote na ujuzi wote na ndio maana hata wafungwa waliohukumiwa na mahakama sio wote wenye makosa.

mahakama yenye kuhukumu watu kwa mgongo wa rushwa unataka kuifananisha na mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na muweza wa yote??

Mahakama tumeona mara nyingi imekiri kua "mtuhumiwa aliyeishi gerezani miaka mingi leo hii mahakama imemkuta hana hatia" unataka kuniambia uwezo wa mungu nao ni wakubabaisha kama ilivyo mahakama zetu???
Atheists mnaikubali kweli ikiwa upande wenu, lakini kweli hiyohiyo ikihama upande mwingine munaikana... Mna nini nyinyi?
Haya ita na haya ni mahubiri maana hoja zikiisha kinacho fuata ni 'character assassination '
haya sio mahubiri ila ni ngonjera.[/QUOTE]
 
Kweli, dini zinatoa tafsiri potofu kuhusu kifo.

Unaambiwa ndani ya kabuli kuna nge, nyoka etc,na kuna malaika ana bonge la rungu la kuwazibua wafu ili akili zikae sawa.. Then unaanza kutililika full infor ulizokuwa unafanya duniani.

Kifo sio hukumu.

Binafsi sikumbuki mara ya mwisho kuhofia kifo.
I always preach and believe death is eminent; if I find a noble cause to die let me nobly die.
 
Uthibitisho upi huo ? Huo ndio uthibitisho wangu,sasa labda wewe upinge kwamba huo si uthibitisho na utoe sababu za kielimu.

Tuendelee....
Hayo mahubiri nataka uthibitisho
 
Hujakanusha kielimu. Kwanza kilichoandikwa umekielewa ?
Hoja za kielimu hukanushwa kielimu

Kukanusha hoja yako kielimu ni kutoitendea haki elimu

Hoja yako inaujinga ndani yake hivyo haipaswi kukanushwa kielimu
 
What is your proof that it is a trusted book ?
You denied a lot of things. books, angles, prophets etc, but all this the source is denying the existence of ONE GOD, so if I can prove to you the Quran is the book of ONE GOD, you will rise this n that which also I will clarify for you, but since denying the book is not the disease which you suffer from but the symptoms of the disease, then lets don't waste each other time on the symptoms while the root of problems left untouched ... lets talk about the root first ... lets talk about ONE GOD
Since your the one who dined the existence of ONE GOD then enlight us WHY SO ...
 
Hoja za kielimu hukanushwa kielimu

Kukanusha hoja yako kielimu ni kutoitendea haki elimu

Hoja yako inaujinga ndani yake hivyo haipaswi kukanushwa kielimu

Kurudi katika asili ndio elimu yenyewe hiyo na mimi nimerudi kwenye asili ns shahidi ulioutaka nimekupa.

Sasa sababu najua huna hoja ya kielimu siku yoyote ukiujua ukweli nistue.
 
pamoja na kutoa majibu na njia lakini si kuna watu wanafeli?? je mwalimu huyo ikiwa ni mwenye uwezo wote wa kuwafanya wanafunzi wote wa faulu pasipo kufelisha ikatokea mwalimu huyo amefelisha robo ya darasa utaona si sahihi kwa wazazi kumlaumu mwalimu huyo??
Unacho fanya hapa ni kama kulazimisha penalti ...
Kwanza mwalimu yoyote akitaka darasa lote lifaulu anaweza fanya hivyo, just anawapa wote 100 ya 100, je atakuwa amefanya sahihi? Kwa muktadha wa tunacho zungumza hapa mwalim tumemuweka kama mfano kwenye tendo la MUNGU MMOJA kuwatahini waja wake na kisha kuwapa malipo kulingana na ufaulu ... unapo sema mwalim anayo uwezo wa kuwafanya wafaulu lakini kawafelisha ... nadhani unamaanisha kuwa MUNGU MMOJA anao uwezo wa kuwafaulisha waja wake wote kwanini basi awafelishe ni kuwaadhibu ... hoja hii nime ijibu huko juu kwenye hayo unayo ita 'mahubiri' na 'ngonjera' tafadhali rudia tena ... lakini kama unang'ang'ania kuwa MUNGU MMOJA anawafelisha makusudi waja wake LETA USHAHIDI WAKO, KAMA HUNA TUFUNGE HICHI KIPINGILI,

Darasa unalolinadi nilishaona wanafunzi kutoka darasa hilo wote waki score zero, sasa kuna umuhimu gani mimi kwenda darasa hilo?? elimu inayotolewa darasani humo ni full hoax, mtu anafundishwa kua nyoka na binadamu walizungumza nae anakubali tu. Darasa linatoa elimu ya kizushi kua jua huzama matopeni, dunia ni bapa , mara jua huzunguka dunia WTF??? Labda mimi ndio niwe mwalimu wenu wa hilo darasa.
Mambo munayo yakana wakanaji wa MUNGU MMOJA ni mengi mno, lakini yote hayo msingi wake ni mmoja tu, KUKATAA UWEPO WA MUNGU MMOJA, hivyo hayo mengine mnayo yakana ni matokeo ya kulikana tendo zima la UUMBWAJI, na MUUMBAJI MWENYEWE.
Unaonaje basi tukaacha kushughulikia dalili za ugonjwa na tukaelekeza nguvu kutibu ugonjwa wenyewe wa kumkana MUUMBA? LETS TALK ABOUT GOD.
Tuambie kwanini, hoja moja baada ya nyingine KWANINI unadai hakuna MUUMBA?
Tukiifunga hii vizuri tutatizama vitabu, mitume, malaika n.k

nimeyapuuza kwasababu si majibu
Majibu yanapuuzwa kwa hoja, si kwakusema tu nimeyapuuza ... unawanyima haki wafuasi wako ambo wangetegemea wewe ungejibu hoja hizo ... unawaacha njia panda wafuasi wako ... hivyo rudi na jibu hoja hizo.

vilaza utawajuaje bila kuwapa mtihani wa majaribio??? utajuaje huyu kilaza na huyu si kilaza bila kuwapima kwa mtihani?
Na hicho ndicho tunacho sema wafuasi wa MUNGU MMOJA, kwanini uhukumiwe tu bila kupewa mtihani, na ulipwe stahiki yako hiyo standard ya sheria ya maumbile .... mahakamani lazima ukiri kosa, uhukumiwe au ukanushe na utoe hoja zako. MUNGU MMOJA angehukumu tu bila kukutahini na kisha kukuhoji si mngesema MUNGU MMOJA mbona hafuati kanuni za maumbile mbona ni dikteta, mbona anatumia mabavu ...nk ndiyo maana, unapewa mtihani, jibu utakavyo jibu, matokeo yatasema wewe unstahiki wapi.

Unaweza ukaniambia nini lengo la mtihani mashuleni??
Yapo mengi sijui wewe ni lipi unalo taka kulijengea hoja, litoe tu tulijadili.

Kwanza mwalimu huyu anauwezo wote na ujuzi wote pamoja na upendo wote? ikiwa kama kimoja kati ya hivyo hana basi haitakua sahihi kuhoji mapungufu yake.
MUNGU MMOJA NI MKAMILIFU PASINA MAPUNGUFU YOYOTE.

Pili nataka nikuambie kua

mwalimu hana uhakika na wanafunzi wake na ndio maana anatoa mitihani ili kupata uhakika. Kwasababu hao vilaza wako katika hali ya kujifunza na kuna muda wanaweza kuwa juu zaidi ya hapo walipo sasa hapa ili mwalimu atambue kua huyu kapanda daraja yule kashuka inambidi atumie mtihani kama njia ya kujua
nimekuuliza na huyo mwalimu anakua na uwezo wa kuingia akilini mwa mwanafunzi kujua anachokiwaza huyo mwanafunzi??
Kwenye 'mahubiri' na 'ngonjera' nilishajibu hili, nilipo kupa darasa fupi la kiumbe kinacho itwa 'time' au 'muda' na tabia zake, rudia hapo juu soma tena.

Mungu huyu unayemfananisha na huyo mwalimu ndiye huyu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote???
NAOMBA NIKUSAHIHISHE SIJAMFANANISHA MUNGU MMOJA NA MWALIMU.
ILI UWEZE KUELEWA, NIMETIZAMA 'HALI' au 'SITUATIONAL' ya TENDO LA MWALIMU NA WANAFUNZI NA HABARI YA MITIHANI, NIKALINGANISHA NA TENDO LA MUNGU MMOJA NA WAJA WAKE NA MITIHANI. NILICHO FANANISHA HAPO NI VITENDO VIWILI NA SIYO WATENDAJI WA VITENDO HIVYO.

sasa jiulize ikiwa kama tu mwalimu asiyekua na uwezo wote ujuzi wote na upendo wote akifelisha wanafunzi kizembe kazi yake inakua matatani, inakuaje mungu mwenye sifa ya ujuzi wote, upendo wote na uweza wa yote kuumba ulimwengu wenye mabaya wakati alikua na uwezo wa kuumba ulimwengu usioruhusu mabaya asishtumiwe kwa ujinga huu?
Tafadhali rudi tena kwenye kile ulicho kiita 'mahubiri' na 'ngonjera' nimejibu hoja hii.

mahakama haina uwezo wote na ujuzi wote na ndio maana hata wafungwa waliohukumiwa na mahakama sio wote wenye makosa.
MUNGU MMOJA KAEPUKANA NA MAPUNGUFU HAYO.

mahakama yenye kuhukumu watu kwa mgongo wa rushwa unataka kuifananisha na mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na muweza wa yote??
REJEA HOJA YA MWALIM HAPO JUU

Mahakama tumeona mara nyingi imekiri kua "mtuhumiwa aliyeishi gerezani miaka mingi leo hii mahakama imemkuta hana hatia" unataka kuniambia uwezo wa mungu nao ni wakubabaisha kama ilivyo mahakama zetu???
REJEA HOJA YA MWALIM HAPO JUU.

haya sio mahubiri ila ni ngonjera.
[/QUOTE]
Si mahubiri ni ngonjera unataka kuanzisha uzi mwingine wa sifa za mahubiri na ngonjera, kwani hizi hoja umesha jibu zote ... tulia dawa ikuingie acha kuruka ruka, jibu hoja hapo juu moja baada ya nyingine maetheist wenzako wanakutegemea usiwaangushe.
 
Niko hapa kujibu hoja zilizojengeka katika mifumo inayokubalika ki mantiki na kimsimamo. mpaka saizi sijaona hoja yeyote uliyoweza kuitoa, kama unahisi umeitoa ila haijajibiwa jaribu kuichunguza kama imefit katika vigezo hivyo
 
Kurudi katika asili ndio elimu yenyewe hiyo na mimi nimerudi kwenye asili ns shahidi ulioutaka nimekupa.
ushahidi gani ulionipa?? Ukiambiwa ulete ushahidi utapeleka hizo ngonjera kama ushahidi?

Nikikwambia unipe ushahidi unaosema kuto kula nguruwe ni haram kwa muislam hapo ukinipa aya kutoka kwenye kuran utakua sahihi. Hata mimi kama kuna mtu anabisha kua kuna habari zimeandikwa kwenye vitabu kua jua huzama matopeni nitampa ushahidi wa hayo maandishi ajiridhishe.

Sasa sababu najua huna hoja ya kielimu siku yoyote ukiujua ukweli nistue.
ukweli hata ukiletewa utauelewa kua ni ukweli pasipo akili?

Nilishawahi kukupa fact ya ukweli kua jua si kiumbe hai vipi ulielewa?

Na kama hukuelewa unafikiri utaweza kuyaelewa mambo mengine unayodai nikustue??
 
Back
Top Bottom