COSAFA Cup, leo 18 Mei 2015: Tanzania vs Swaziland

COSAFA Cup, leo 18 Mei 2015: Tanzania vs Swaziland

hivi ni kweli wakuu unampa vipi john boko acheze 90 minutes? kwa hali hii sidhani hata chan tutaweza toboa ni hali mbaya sana tuko nayo kwa sasa
 
Tatizo wachezaji wamezoea ligi ya kununua mechi na ubishoo wa kwenye Mwanaspoti na Championi.Hivi kweli kufungwa na Swaziland iliyoko kwenye namba 175 kwenye rank ya FIFA utadai tunacheza mpira? Turudi zetu tuendelee na mdumange wetu.
 
Kichwa cha mwendawazimu hichoo ati, wala usishangae . Ka nchi kadoooooogo hako nako kanatutoa jasho , AIBU YAO AIBU YETU WATZ
 
mhhh hali yetu ni mbaya saaana ila ukiwasikia viongozi wetu wa TFF na mipango yao utasema wana stars wanakwenda kombe la dunia urusi
 
Mashabiki wa Taifa Stars hawajawahi kuonja furaha ya ushindi tangia wazaliwe, na kunahatari wakafa na huzuni mioyoni mwao.
Poleni sana,najua inawauma sana ila ndiyo ukweli wenyewe..
 
mi huwa nasema hatuna wachezaji hawa akina msuva huwa mechi zinaponunuliwa ndo wanaambiwa team husika hhakikishen flan na flan ndo anawafunga so huwa kila kitu kinajulikana before

hapo kwenye red mh
 
Kichwa cha mwendawazimu hichoo ati, wala usishangae . Ka nchi kadoooooogo hako nako kanatutoa jasho , AIBU YAO AIBU YETU WATZ

Benchi la ufundi nalo ni matatizo,sisi tupo nyuma ya king'amuzi cha Azam tunaona matatizo,wao wapo live uwanjani wanaona poa tu.
 
Kichwa cha mwendawazimu hichoo ati, wala usishangae . Ka nchi kadoooooogo hako nako kanatutoa jasho , AIBU YAO AIBU YETU WATZ


Hapo kwenye kijani,
mimi sihusiki kabisa mkuu.
 
Hatuna viongozi ktk mpira tanzania. Neno uongozi ukiondoa herufi ya mwisho "zi" unabaki na "uong.....o. Ndio tulio nao ktk soka hapa tza. Shame
 
Mashabiki wa Taifa Stars hawajawahi kuonja furaha ya ushindi tangia wazaliwe, na kunahatari wakafa na huzuni mioyoni mwao.
Poleni sana,najua inawauma sana ila ndiyo ukweli wenyewe..

Furaha yangu ya kuwa mshabiki wa Yanga,Barca,Bayern M imekufa ghafla leo.Naamini Stand United ingeshinda leo sio hao majanga.
 
Viongozi hawa wa soka , sijui wao hawana mioyo kama sisi , wansfikiri sie tuna mioyo ya chuma hatuumizwi na matokeo mabovu kila mara ama wao wanafurahi timu yetu inavyofungwa fungwa hivi hata na vitimu vidogo?
 
Back
Top Bottom