Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,768
- 49,940
Wengi tumeambiwa kuhusiana na ugonjwa wa Corona. Na wengi tunaamini kuwa sasa tunauelewa.
Tunapojihadhari na ugonjwa huu, mategemeo yetu makubwa ni serikali na wataalam wa afya, ambao tunadhani kuwa wana ufahamu zaidi kuliko sisi tusio watu wa fani ya tiba.
Jambo moja tunalotakiwa kujua ni kuwa mpaka sasa, kwenye ugonjwa huu, wote ni layman. Na inawezekana, mtu asiye mtaalam wa tiba, kama anajishughulisha kuufahamu ugonjwa huu kwa kupitoa maandiko mbalimbali ya wataalam wa huko ambako upo, akawa na uelewa mkubwa zaidi kuwazidi wasemaji wa serikali au madaktari wetu.
Watu wasiitegemee sana serikali wala madaktari bali wajitahidi kuujua ukweli kuhusiana na ugonjwa huu. Mpaka sasa kuna madudu mengi tayari yamefanywa na serikali, ambayo kwa watu wanaouelewa ugonjwa huu, wasingefanya. Labda tu tumekingwa kwa neema ya Mungu tu lakini siyo kutokana na umakini wa Serikali.
1) Siku za karibuni serikali iliruhusu watalii toka China wakati nchi nyingine zimepiga marufuku ndege kutua nchini mwao kutokea China, achilia mbali kupokea watalii wa Kichina
2) Karibuni tena, pale JKN airport kuna watu wagonjwa ambao dalili zilionekana kushabihiana na zile za Corona, walipimwa na kuonekana negative, wakaruhusiwa kuingia mitaani. Ukweli ni kwamba siyo wagonjwa wote au watu wenye coronavirus, virusi hivyo huonekana kwenye vipimo. Inaonekana watu hawa wa serikali bado hawajaujua huu ugonjwa.
Tafiti za karibuni kabisa zinaonesha mambo yafuatayo:
1) Kirusi cha Corona kinaambukizwa zaidi kwa kushika sehemu aliyoishika mwathirika kuliko kwa njia ya kukohoa.
2) Kirusi cha Corona siyo airborn bali ni huenea kwa droplets za mate. Wale wanaoongea mpaka wanatema mate, kama ameathirika, ni wasambazaji wazuri
3) Kirusi cha Corona, kwa mfano muathirika akishika kwenye meza au akakoholea kwenye meza kinaweza kuishi hapo kwa siku kadhaa, hakuna anayejua kina uwezo wa kukaa siku ngapi. Kwa hiyo kwenye milango, ngazi, viti, meza, hata simu zetu - vyote vinaweza kueneza kwa kasi zaidi kuliko kushikana na kukohoa
4) Kirusi cha corona, kimeonekana kina uwezo wa kujificha na kisionekane kwenye vipimo. Inaaminika ni katika hatua zake fulani tu, ndiyo huonekana kiurahisi. Baadhi ya wagonjwa waliotibiwa, na kupimwa na kuonekana negative, baadaye walionekana wana uwezo wa kuendelea kuambukiza, wengine baadaye walionekana tena positive, na wengine walikufa baada ya kuruhusiwa na kutajwa kuwa wamepona.
Hiki kirusi siyo cha mzaha, kama ambavyo serikali yetu imekuwa ikichukulia.
Kenya tayari, DRC tayari, Rwanda tayari, Botswana tayari - Hatupo salama kama tunavyofikiria. Chukua tahadhari binafsi kuliko kuitegemea sana Serikali.
Serikali yetu inafahamika. Ni nyepesi sana kushugulikia mambo yanayotishia kupokonywa utawala na madaraka lakini siyo kwenye mambo ya msingi yanayohusu uhai, usalama na maisha ya wananchi wote.
Ikitokea ugonjwa huu ukaingia nchini mwetu, mzazi chukua hatua zako binafsi kama vile kumzuia mwanao kwenda shule kuliko kusubiri mpaka Serikali itangaze.
Kama una uwezo wa kuepuka usafiri wa umma, epuka kuanzia sasa kuliko kusubiri siku Serikali itakapotangaza. Watatangaza pale ambao tayari hali imekwishakuwa mbaya. Kama siyo lazima sana kusafiri, acha kusafiri kuanzia sasa, hii ni pamoja na safari za ndani.
Can you get coronavirus twice?