Coronapocalypse

Coronapocalypse

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
97,070
Reaction score
136,458
Gumzo la dunia hivi sasa ni kirusi cha Corona.

Kirusi hiki kimeleta kizaizai na sokomoko kila pembe ya dunia.

Nchini Marekani kuna sintofahamu kubwa.

Hakuna ajuaye mwisho wa huyu kirusi.

Hali hiyo imepelekea kutokea kitu kinachoitwa ‘panic buying’.

Sasa hivi ukienda kwenye maduka-masoko [supermarket] mengi kuna baadhi ya bidhaa kuzipta ni mbinde.

Bidhaa hizo ni kama karatasi za chooni, taulo za karatasi, jeli za kusafishia mikono, na kadhalika.

Rafu za maduka-masoko mengi zipo tupu. Hiyo ni kwa sababu watu wengi wanazinunua hizo bidhaa kwa wingi kuliko ilivyo kawaida. Jambo linalopelekea kuwepo na uhaba wa hizo bidhaa kwa sasa.

Hebu ona hizo rafu hapo chini. Ni kutoka duka-soko la Publix.

8A5F51F1-662B-46D8-A661-6CBC69CC57AC.jpeg
F887BB79-E723-4E74-A0C2-98A7DD529844.jpeg
E697D103-1666-4F97-AD1E-C20ACFAFBC0E.jpeg
9B559E56-A957-41F4-8B2F-BC99ED61C24F.jpeg

Sielewi kwa nini watu wanakimbilia sana kuzinunua hizo bidhaa na kuzihodhi majumbani mwao.

Kwangu jambo lenye mantiki zaidi na bora ni kujiwekea akiba ya pesa kuliko kutumia pesa na kununua vitu ambavyo kama itatokea umeugua na hicho kirusi, havitakusaidia kupata nafuu.

Badala ya kununua dawa, watu wananua makaratasi ya chooni!

Halafu Wamarekani wana tabia ya ku-panic sana.

Corona siyo kiama. Lakini jinsi watu wanavyofanya mambo hivi sasa, utadhani kiama ndo kimefika.

Sielewi. Na wala siogopi.

I ain’t never scared 💪🏿
 
Mkuu rudi kwnza huku ikungulyababeshi ili mambo yakipoa urudi huko
 
Asilimia kubwa ya wanaopata hayo mafua ya Corona wanapona.

Pia, unaweza kuwa na hayo mafua na wala usijue na yenyewe yakaisha hivyo hivyo.

Panic iliyopo haiendani kabisa na athari zake.
Ngoja tuendelee kuona hali inavyoenda, ila kwa kuwa wapo wanaopeteza maisha pia ni muhimu kuchukua tahadhari.
 
Atii huogopi hii ugonjwa ,hii ni ugonjwa hatari sana hasa kwa Africa. Labda ni kiki unatafuta

Sent using Jamii Forums mobile app
Nenda kamsome Betty Mkwasa Facebook na Insta,Kuna watu wameugua 3 weeks ugonjwa unaofanana na huo, Betty aliugua,Mkwasa kwenye kambi na wachezaji kadhaa,hiyo ilijuwa Desemba 2019, Hospital zilishindwa kujua wanaumwa nini?
Au Facebook kamsome Onni Sigala utapata majibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja tuendelee kuona hali inavyoenda, ila kwa kuwa wapo wanaopeteza maisha pia ni muhimu kuchukua tahadhari.

Kuchukua tahadhari nakukubali.

Lakini panic iliyopo haiendani na uhalisia wa hatari yake.
 
Jaribu kufikiri kuanzia usafiri kama daladala,mwendo kasi ,huduma za jamii kama shule ,hospital zitaendeshwaje wagonjwa wakiwa wengi,then hospital zinahesabika wahudumu wa afya wanahesabika,Tz tuko wangapi ...hizo mask zenyewe ni mtihani,ukiona wenzetu wameshindwa jua ni hatari,omba Mungu aepushe mbali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nenda kamsome Betty Mkwasa Facebook na Insta,Kuna watu wameugua 3 weeks ugonjwa unaofanana na huo, Betty aliugua,Mkwasa kwenye kambi na wachezaji kadhaa,hiyo ilijuwa Desemba 2019, Hospital zilishindwa kujua wanaumwa nini?
Au Facebook kamsome Onni Sigala utapata majibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao sio wataalam wa afya ,duniani kote watu wanahangaika usiku na mchana kutafuta ufumbuzi ila bado,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asilimia kubwa ya wanaopata hayo mafua ya Corona wanapona.

Pia, unaweza kuwa na hayo mafua na wala usijue na yenyewe yakaisha hivyo hivyo.

Panic iliyopo haiendani kabisa na athari zake.
Kuna uzi niliwaambia watu hili jambo kuwa waathirika wengi wana recover jamaa wakanicheka kinyama.
 
Hata mimi kwa upande wangu naona panick imekua kubwa mno naweza kusema kua panick iliyopo kwenye corona ni kubwa kuliko iliyokuwepo kwenye ebola wakati ebola ilikua karibu nasi zaid kuliko hiyo corona.
Nadhani mitandao ya kijamii inachangia zaidi katika hili hasa kwakua nchi waathirika zinajiweza kiuchumi na kipropaganda pia janga likiwa kubwa kwao basi na kwetu ni hivo hivo vivyo hivyo likiwa dogo kwao na kwetu tutaona ni janga dogo.

Na wanaopata pata corona katika nchi zetu izi wengi utaskia ni msafiri kutoka eidha ulaya,asia au amerca ndo amekuja na hiyo corona. Na uku kwetu usambaaji wake sio wa kasi kama zilivo nchi kama italy,markani na china. Nchi nyingi za Africa ukiskia mtu kasadikika ana corona basi ni huyohuyo nchi nzima.

NB: Tahadhari ni muhimu lakini hatupaswi kupanick kwa wakati huu na kuchukua maamuzi yasiyo sahihi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom