Tetesi: Corona virus: lran imekataa msaada kutoka Marekani

Mdaiwa-Sugu

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
284
910
Kiongozi mkuu wa kidini nchini Iran, Ayatollah Ali Khamenei amesema Iran haitopokea msaada wowote kutoka Marekani, katika kubadili hali ilivyo kutokana na wimbi la maambukizi ya virusi vya corona nchini mwake. Katika taarifa yake hiyo Khamenei alirejea kuizungumzia dhana ya kwamba virusi hivyo ni silaha iliyoundwa na Marekani dhidi ya maadui zake.

Katika hotuba yake iliyorushwa moja kwa moja kupitia televisheni, kiongozi huyo amesikika akisema wana maadui wengi lakini, mkubwa kuliko wote ni Marekani.. na sasa anataka kuwasaidia. Ayatollah amenukuliwa akisema ni vyema taifa hilo likajikita katika kuwasaidia wananchi wake.

Iran limekuwa eneo tete la usambaaji wa virusi vya corona, ambavyo vilianzia China mwishoni mwa mwaka uliopita. Hata hivyo usambaaji wa visa hivyo ulianza kuingia Marekani wiki iliyopita. Marekani inakabiliwa na mamia ya vifo vyenye kuhusishwa na virusi hivyo, wakati Iran vifo vyake vinapindukia watu 1000. Katika hatua hiyo ya kukataa msaada, Khamenei aligusia nadharia ya kwamba virusi hivyo viliundwa na Marekani kwa lengo la kuyadhoofisha mataifa adui kama China na Iran. Tangu Januari Khamenei amekuwa akisema virusi hivyo vinaweza kuwa silaha ya kibailojia iliyoundwa na Marekani.

Mpaka sasa watu zaidi ya 13000 wamekufa kutokana na maambukizi ya virusi vya corona huku wengine zaidi ya 300,000 wakiambukizwa virusi hivyo duniani kote.
 
Duh, mambo yanazidi kuchachamaa, Mungu atusaidie, na kama ni kweli US ndio alitengeneza hii virus, yatamkuta tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa upande wake US anamlaumu china kwa kushindwa kuudhibiti huu ugonjwa mwanzoni kabisa mpaka kupelekea kusambaa duniani kote. marekani ameenda mbali zaidi kwa kumtuhumu china kuhusika na utengenezaji wa hivi virusi.

Pamoja na mataifa haya mawili kushutumiana kila mmoja ila ipo siku ukweli utajulikana hata kwa kuchelewa.
 
Huyu Mzee ni masikini jeuri !! Msimamo wake unatesa raia wake, hizo propaganda za kirusi kutengenezwa Marekani angezipumzisha wakati huu wa dharura.

Anakataa msaada wakati raia wake wanataabika kwa ugonjwa na madaktari wameishiwa mpaka vifaa tiba huku wengi wakiambukizwa wakati wakitoa huduma.
 
Wala sio maskini jeuri yupo sawa tu kwani anae sababisha waajemi kukosa madawa ninani c huyo huyo US
Huyu Mzee ni masikini jeuri !! Msimamo wake unatesa raia wake, hizo propaganda za kirusi kutengenezwa Marekani angezipumzisha wakati huu wa dharura.

Anakataa msaada wakati raia wake wanataabika kwa ugonjwa na madaktari wameishiwa mpaka vifaa tiba huku wengi wakiambukizwa wakati wakitoa huduma.
Kama alikua anania ya Msaada IRAN Wala hawataki Msaada Wanataka Kuondolewa Vikwazo Tu Kwamuda Huu Ambao Wanakabiliwa Nagonjwa Wapate kuagiza Vifaa Tiba Mbali Mbali

Sasa kama US Kakomaa Nakumuekea Vikwazo Halafu Upande Wapili Anajifanya Kutaka Kumsaidia Anataka Kumsaidia Nanini wakati ishu ipo wazi tu aondoe vikwazo maisha yaendelee

Nlichopendelea kuhusu CORONA Haichagui kwamaana Mpaka Viongozi Wanaukwaa Kwahio Hapo Hatesi Raia Tu Mpaka Yeye Mwenyewe Ame Risk Maisha Yake Ila Uzuri Wake Nikwafaida Yataifa Lake Kwaujumla

US WAUAJI

Sent using My COVID-19
 
Ni kama unajitekesnya mwenuewe, unakataa kupokea msaada wa mtu ambaye hajatangaza kukupa msaada, yaani hawa viongozi wanajiundia agenda ili wapate hoja kwa wananchi wao.
Unahisi kama wasingetangaza Kupewa Msaada Wangeropoka US Kasema Yupo Tayari Kupeleka Msaada IRAN Halaf Wewe MYAHUDI Wa NAIROBI Unakataa Nini

Sent using My COVID-19
 
Huyu Mzee ni masikini jeuri !! Msimamo wake unatesa raia wake, hizo propaganda za kirusi kutengenezwa Marekani angezipumzisha wakati huu wa dharura.

Anakataa msaada wakati raia wake wanataabika kwa ugonjwa na madaktari wameishiwa mpaka vifaa tiba huku wengi wakiambukizwa wakati wakitoa huduma.
Mkuu uko sahihi kabisa, lakini hawa wamarekani hawatoagi misaada kwa nia njema

Nawaunga mkono Iran kwenye hili.
 
Unahisi kama wasingetangaza Kupewa Msaada Wangeropoka US Kasema Yupo Tayari Kupeleka Msaada IRAN Halaf Wewe MYAHUDI Wa NAIROBI Unakataa Nini

Sent using My COVID-19
Trump alisema yuko tayari kusaidia wananchi wa Iran kuhusu hili janga mwezi huu mapema kabla hata ugonjwa hausambaa sana America ewe shia wa Kilosa.
 
Huyu Mzee ni masikini jeuri !! Msimamo wake unatesa raia wake, hizo propaganda za kirusi kutengenezwa Marekani angezipumzisha wakati huu wa dharura.

Anakataa msaada wakati raia wake wanataabika kwa ugonjwa na madaktari wameishiwa mpaka vifaa tiba huku wengi wakiambukizwa wakati wakitoa huduma.
Khamenei ana hofu kwamba anaweza kupewa drugs ambazo zitafanya the virus to remain in Iran permanently. Hawana imani na chochote US atakachotaka ku-offer. Wanahisi lazima ni mtego.
 
Trump alisema yuko tayari kusaidia wananchi wa Iran kuhusu hili janga mwezi huu mapema kabla hata ugonjwa hausambaa sana America ewe shia wa Kilosa.
Kwann asiwasaidie maswahiba zake mpaka wana kufa kama panya na anganganie kuisaidia Iran?
Eti kuwasaidia raia wa Iran angekuwa anawapenda angekuwa kila siku ana fanya kila mbinu kulidhoofisha taifa lao?
 
Huyu Mzee ni masikini jeuri !! Msimamo wake unatesa raia wake, hizo propaganda za kirusi kutengenezwa Marekani angezipumzisha wakati huu wa dharura.

Anakataa msaada wakati raia wake wanataabika kwa ugonjwa na madaktari wameishiwa mpaka vifaa tiba huku wengi wakiambukizwa wakati wakitoa huduma.
Mi naona ni sawa tu alivyokataa... Watu wanaomba waondolewe vikwazo vya kibiashara... Ili wanunue vifaa tiba, unakataa... Halafu leo hii eti uwaletee msaada, huo ni unafiki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwann asiwasaidie maswahiba zake mpaka wana kufa kama panya na anganganie kuisaidia Iran?
Eti kuwasaidia raia wa Iran angekuwa anawapenda angekuwa kila siku ana fanya kila mbinu kulidhoofisha taifa lao?
Mashia sijui mnaumwaga nini, embu rudia kusoma nilichoandika na usome ulichoandika wewe tena.

Trump alisema yuko tayari kusaidia wananchi wa Iran kuhusu hili janga mwezi huu mapema kabla hata ugonjwa hausambaa sana America ewe shia wa Kilosa.
 
Huyu Mzee ni masikini jeuri !! Msimamo wake unatesa raia wake, hizo propaganda za kirusi kutengenezwa Marekani angezipumzisha wakati huu wa dharura.

Anakataa msaada wakati raia wake wanataabika kwa ugonjwa na madaktari wameishiwa mpaka vifaa tiba huku wengi wakiambukizwa wakati wakitoa huduma.
Shida inayojitokeza hapa ni hofu kuu ya lran dhidi ya marekani anahisi hata huo msaada atakaopewa unaweza kuwa mtego wa kuwamaliza. Iran hana imani kabisa na US
 
Screenshot_20200322-224124.png
 
ukisoma thread utaona kwamba wamekataa baada ya marekani kutaka kuwasaidia. Siku nyingine uache kucheza yope unavosoma thread.

Back
Top Bottom