sangujoseph
Senior Member
- Nov 30, 2015
- 164
- 184
By Sangu Joseph
Tukiwa tunaendelea kuchukua tahadhari ya kupambana na Corona kuna tatizo moja kubwa nimeliona ambalo linaendelea kushamili sana ambalo linahatarisha umoja wetu kama Watanzania (Kunyanyapaa)
Hili ni tatizo kubwa sana kwa sasa licha ya mwanzoni nililishuhudia kufanyika katika baadhi ya Vyombo vya usafiri (Daladala ) lakini sasa nimeona limeenda mbali zaidi mpaka kwenye vituo vya Afya na kwenye makazi yetu watu wananyanyapaana kisa Corona.
Nakumbuka hata hivi karibuni April 23, 2020 Waziri wa Afya Ummy Mwalimu aliwataka wahudumu wa Afya wasiwatenge wenye Corona, lakini pia April 22 Rais Magufuli alieleza kisa kimoja cha kunyanyapaa kilichotokea Dodoma jimboni Kwa Spika Ndugai ( Wakati akizungumza na Viongozi wa Vyombo vya ulinzi na usalama).
Tatizo kubwa la uwepo wa Corona kwetu Tanzania imepelekea kunyanyapaana wenyewe kwa wenyewe licha ya kuchukua tahadhari ya Corona kwa mujibu wa Wataalam. ( Yaani mbeba kinyesi anaweza akakumbatiwa na kupandishwa Daladala lakini wewe unayekohoa au kupata mafua ukashushwa kwenye Daladala)
Kunyanyapaana wakati huu wa Corona ni hatari sana baada ya huu ugonjwa kuisha maana itajenga uhasama baina yetu Sisi Watanzania na kubomoa umoja wetu ambao ulijengwa kwa muda mrefu.
Rai yangu kwa viongozi wa Dini mnanafasi ya kuwakutanisha waumini pamoja kupitia ibada msaidie kuhubiri upendo na kukemea vitendo hivi.
Wito wangu kwa Serikali isaidie kuweka watu maalum (Volunteer) wapite kwenye maeneo ambayo mikusanyiko haijapigwa marufuku ili kutoa elimu juu ya kutonyanyapaana sababu ya Corona.
- Sangu Joseph
- #KijanaaMzalendo
- 0712861292
.
#IloveTZ
Sent using Jamii Forums mobile app