Asilimia 80 ya Watanzania waliopata virusi vya Corona hawakufika hospitalini

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Wizara ya afya nchini Tanzania kupitia ofisi ya mpango wa taifa hilo wa chanjo imesema tangu kuingia kwa janga la Corona nchini humo mwishoni mwa mwaka 2019, asilimia 80 ya watanzania waliopata virusi vya Corona hawakufika hospitali huku asilimia tano ya walioambukizwa walifikishwa kwenye vyumba vya wagongwa mahututi ICU.

Pamoja na mambo mengine wizara hiyo inasema ukosefu wa elimu ya kutosha kwa wananchi umechangia suala hilo, huku mpaka sasa mwamko wa chanjo ukisuasua katika maeno mengi ikiwepo mikoa ya kanda ya ziwa.

Meneja wa taifa wa mpango wa chanjo kutoka wizara ya afya nchini Tanzania Dr. Florian Tinuga, ameyasema hayo wakati akitoa mafunzo maalumu kwa waandishi wa habari kuhusu kuripoti habari zinazohusu Corona, akibainisha kuwa kundi la waandishi wa habari ni muhimu kupatiwa elimu mahususi hasa katika kipindi hiki kunaposhuhudiwa taarifa mbali mbali alizoziita kuwa ni za upotoshaji kuhusu janga la Corona.

Ukosefu wa elimu sahihi ni kati ya sababu za watu kutofika hospitalini
Akitoa ripoti kuhusu utekelezaji wa kitaifa wa chanjo ya Corona Tanzania mpaka kufikia tarehe 15 mwezi wa Disemba, Dr. Tinuga amesema takwimu zinaonesha asilimia 80 ya Watanzania waliombukizwa virusi vya Corona hawakufika hospitali, kutokana na sababu mbali mbali miongoni ikiwa ni ukosefu wa elimu sahihi.

Tanzania inatarajia kuzindua mpango wa pili wa chanjo kitaifa kuanzia Disemba 22, 2021.

Aidha waandishi wa habari walipotaka kujua kwanini Tanzania haitoai takwimu za mwenendo wa ugonjwa wa Corona.

Tanzania iliyo na idadi ya watu karibu milioni 60 imeweka malengo ya kufikisha asilimia 70 ya Watanzania watakaochanjwa chanjo ya Corona, huku zoezi hilo likionekana kusuasua katika meneo mengi.

Mkoa wa Ruvuma unaongoza miongoni mwa wlaiopata chanjo

Kulingana na takwimu za wizara ya afya kupitia mpango wa Taifa wa Chanjo, Mkoa wa Ruvuma ulio kusini mwa Tanzania unaongoza kwa asilimia 4.6 ya watu waliopata chanjo ya Corona huku mkoa wa Manyara ulio kaskazini mwa Tanzania ukishika nafasi ya mwisho miongoni mwa mikoa 31 ya Tanzania ukiwa na asilimia 0.8 ya watu waliopata chanjo hiyo.

Katika mafunzo hayo mwenyekiti wa jukwaa la wahariri nchini Tanzania Deodatusi Balile amewataka waandishi wa habari kuzingatia weledi na taaluma yao katika kuripoti habari za Corona.


DW
 
Walifika sababu hawakupata Elimu ?, Na wale waliobanwa na kukosa pumzi na kufika kukuta mitungi haitoshi walikosa elimu ya Bahati ?

Na Elimu ipi kama Muhimbili waliweka Sauna..., sasa si mtu bora atumie nyungu yake kuliko kufunga safari ? Tuache Siasa kuna blunder wizara ya afya ilifanya kulingana na umuhimu / kazi yake..., ila sio mbaya kama wengi hawakufika hospitali (sababu kama hizo asilimia tano zilifanya hospitali zikazidiwa je wangefika asilimia 20)
 
Asilimia 80 imepatikana wapi. Kwa pilot study ipi?
Unazungumziaje kundi usilolijua na kulipa ugonjwa.
Kwa upimaji unaosuasua huwezi kujua wagonjwa ni wangapi. Mtu yupo Naliendele mpaka sampuli itumwe Dar au Dodoma au Mwanza ndio apate majibu.
Elimu ipi inatakiwa ya kujikinga au kupima?
Ugonjwa upo watu wajikinge.
 
Walioshawishi watu wasichanje wangeuwawa tu kutokana na kifungu penal code 367 ya mwaka 1981
Kwani nao pia ni wauwaji tu
 
Kitendo cha kwenda kupimwa alafu uambiwe una covid19 ugonjwa unaongezeka mara 2,ni heri ubakie home ujipige nyungu na paracetamol huku unajipa moyo kuwa hizi ni homa ndogondogo tu!
Usipopima ukimwi unaweza ukaishia nao hata miaka 100.ila ukipima tu unaanza kuumwa
 
Back
Top Bottom