Moja kwa moja kwenye mada.
Kama ilivyokuwa imetegemewa Kenya tayari wameshakata pumzi. Kinachosubiriwa sasa ni tamko rasmi tu la bwana Kenyatta.
Tayari waziri wao wa afya Mutahi Kagwe amekwishakiri kuwa Corona sasa hivi huko Kenya iko kila mahali. Heri hawa wanao ujasiri wa kuutamka ukweli kama ulivyo. Si ajabu kuwa hata sisi hali si tofauti sana na hiyo.
Bila shaka ni kwa sababu kama hizo ndiyo maana madereva tokea Kenya au Tanzania haijali wapi wanakopimwa, matokeo kwao ni Corona tu kwa kwenda mbele.
Jana katika ITV habari (2000) palikuwa na dereva tokea Tanzania kazuiliwa kuingia DRC kutokana na kukutwa na Corona. Mabishano baina ya dereva huyo na maafisa wa DRC kwenye camera yalikuwa ya kudhalilisha haswa.
Dereva yule alirejeshwa Rwanda bila staha yoyote. Haieleweki kama Rwanda walimpokea vipi, yuko kwenye matibabu, au yuko njiani kurejea nyumbani?
Dereva yule alikuwa akikataa kibongo bongo tu kuwa yeye hana Corona japo vipimo vimeonyesha hivyo.
Kenya kama sisi wamekuwa wakijikanyaga sana kwenye kupambana na huu ugonjwa. Kwa ujumla Kenya na sisi yawezekana hatuna cha mno cha kuchekana. Hali yetu pia haiwezi kuwa na la kupongezwa asilani.
Ikizingatiwa Rwanda na Uganda wanahitaji kufika fukweni kunako bandari, hapo napo patawapa changamoto za kutosha kweli kweli.
Kushoto au kulia, suala hili lilihitaji protocol moja vinginevyo hapa tulipo haya maambukizi kupungua au kuondoka itakuwa ni ndoto tu za alinacha.
Covid-19 cases explode in Mathare - VIDEO
Bandugu tuchukue tahadhari, Corona bado inasambaa.