Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,131
- 35,173
Kuna mambo kadhaa ya kufahamu kwa kina kabla ya kujadili hili.
Kwanza tuukubali ukweli huu kuwa, kusambaa kwa Corona duniani ndio kuliko pelekea kusimama kwa shughuli za utalii hapa Tanzania. Sio mtu, watu au mamlaka fulani iliyoamuru kusitisha shughuli za utalii hapa Tanzania.
Watalii wenyewe na mazingira yanayozunguka utalii ndio yaliyopelekea kusimama kwa utalii hapa Tanzania. Hivyo tusijidanganye kuwa kuna mtu au mamlaka fulani inaweza kuamuru utalii urejee na watalii ghafla wakamiminika kuja nchini.
Pili, utalii ni jambo la ziada&gharama (anasa?) katika maisha ya mtu. Sio jambo la lazima, dharula au kufa na kupona kwa mtalii kuja kufanya utalii hapa Tanzania. Hivyo tusiwe na matumaini ya haraka haraka au kuwa na matumaini makubwa ya kutaka kuona utalii unarejea kama awali. Tujipe muda zaidi, tujipange upya na tuwe na subira.
Tatu, Corona imebadilisha kila kitu duniani kwa muda mfupi sana. Hivyo tukubali au tukatae, mambo hayataweza kurejea tena kama awali, lazima yatabadilika, na kwa vyovyote vile hayawezi kuwa chanya sana kwa upande wetu tulioathiriwa. Tunapaswa kujipanga upya, tena kwa namna tofauti.
Mwisho tunapaswa kufahamu kuwa, kuzorota ghafla kwa shughuli za utalii hapa Tanzania kumeleta hasara kubwa sana, hakuna namna ya kuweza kufidia kirahisi. Wapo ambao wameshafirisika, wengine wamepunguza mitaji yao kwa kuhamisha kwenye biashara zingine. Hivyo sekta nzima kwa sasa imechoka na imezungukwa na woga mwingi.
NINI SASA KIFANYIKE ILI KUREJESHA HALI YA MAMBO KATIKA SEKTA YA UTALII HAPA TANZANIA?
1. Tujikite zaidi kwenye uhalisia wa hali ngumu ya mambo ilivyo kuliko kujikita kwenye taswira tamu ya kisiasa yenye matumaini hewa.
2. Wadau wa utalii wasikilizwe, maoni yao yaheshimiwe na changamoto zao zitatuliwe kwa haraka na mamlaka husika.
3. Serikali ipunguze au kuziondoa kabisa baadhi ya kodi na tozo mbalimbali katika sekta nzima ya utalii. (Kumbuka utalii ndio sekta yenye mnyororo mrefu zaidi wa thamani (chain of value) huku ikiwa sekta mtambuka na yenye kutuingizia pesa nyingi za kigeni, hivyo utalii ni Economic catalyst hata kama serikali itakosa kodi katika sekta ya utalii)
4. Serikali ije na mpango mkakati mpya wa utalii katikati ya janga la Corona. Corona imebadilisha mambo mengi hivyo mipango na mikakati yetu ni vyema ikabadilika kulingana na hayo mabadiliko.
5. Tuimarishe Diplomasia ya kimataifa kwa kulinda ndimi zetu na twende sambamba na ulimwengu unavyotaka. (Vivutio vya utalii sio vitu pekee vinavyoweza kumvutia mtalii kuja Tanzania, mtalii ni mtu sensitive sana na anayependa kulindwa privacy yake na kuheshimiwa utaifa wake, tusije kumtumia mtalii kama ngao ya kuhalalisha siasa zetu, tuheshimu utaifa wake na nchi inayotokea. Zile lugha za kuwaita mabeberu, kuwanyoshea kidole kuwa wao wanatuletea Corona au nchi zao zimeshindwa kudhibiti Corona au wanakimbia Corona kwao, wamekuja kufuata nyungu kwetu nk. tuziepuke kabisa. Pia tusipende sana kuwapiga picha watalii wanapo wasili nchini au katika maeneo ya utalii ili kuziweka kwenye vyombo vya habari au mitandao ya kijamii. Kifupi kabisa tusimchanganye mtalii na mambo mengine ya kwao au ya kwetu)
Mimi ni mdau katika sekta ya utalii hapa Tanzania, ujio wa Corona duniani umeniathiri sana katika shughuli zangu. Hayo niliyoandika ni maoni yangu kulingana na upeo wangu katika sekta hiyo.