Contractionary monetary policy practiced by Magufuli

Contractionary monetary policy practiced by Magufuli

Umelinganisha hali halisi ya mwenendo wa uchumi wa Tanzania au unatoa nadharia tu?
Kubana matumizi kunasaidiaje kuondoa tatizo la ukosefu wa ajira na halisi ya watanzania?
Wanaolalamika wote ni majipu , wezi sasa mnaopatapata ngoja na nynyi tule mlo MMOJA
 
Contractionary monitory policy ni nzuri sana kwasababu serikali inapopunguza matumizi ina maana na viwango vya kodi na tozo mbalimbali navyo vitashuka au kuondolewa kabisa.Eneo la kodi ni muhimu sana ktk aidha kuchochea wawekezaji wa ndani na wa nje kuwekeza kwa wingi au kuwa_discourage wawekezaji hawa kuwekeza.Matumizi makubwa ya serikali hupelekea pia viwango vya kodi kuongezeka au kuwapo kwa kodi holela na hivyo kupelekea kuwapo kwa mfumuko wa bei (inflation hike).Ila nawaomba serikali wasiishie ktk kubana matumizi tu,waimarishe miundombinu ya barabara,bandari na hasa reli ambayo ni njia ya usafirishaji ya gharama nafuu zaidi kwani inaweza kusaidia kupunguza mfumuko wa bei (inflation hike).Pia umeme wa uhakika na wa bei nafuu inaweza si tu kusaidia kushusha inflation bali pia kuchochezea uanzishwaji wa shughuli za uzalishaji au uwekezaji nchini.
Mkuu monetary policy iwe katika expansionary condition au contractionary condition haina uhusiano kabisa na kodi wala matumizi ya serikali.
 
hii ni sera nzuri ambayo inapunguza pesa nyingi kwenye uchumi ambazo hazikuwa na manufaa.hii imechangia mfumuko wa bei uliopo saivi.

MANUFAA YA CONTRACTIONARY NI;
1. Kupanda kwa thamani ya shilingi kwasababu mzunguko wa pesa unakuwa mdogo
2. Kushuka kwa bei za bidhaa kwasababu kwa sababu mzunguko wa hela ni mdogo kuliko bidhaa ( money circulation becomes low than commodities available in the economy)
3. Usawa wa kipato kwa watu, kwasababu hela zikipungua kwenye uchumi manunuzi ya bidhaa yanakuwa affordable kwa watu wote. anachotumia tajiri na mwenye kipato kidogo anaweza kukipata.
NOTE;
Ukichukua mfano kwenye mzani wa usawa ( lorenz curve) ambapo kadri muachano unavyokuwa mkubwa kutoka line ya usawa ndivyo utofauti wa kipato unavyokua mkubwa na kinyume chake ni sawa.
kinadharia umeelezea vizuri matokeo ya sera fedha inayolenga kupunguza mzunguko wa fedha.

Ingawa SIO KWELI kwamba hivi sasa Mh Raisi ndio anatekeleza sera hio. Hamna kiashiria chochote kinachoonyesha kwamba sera ya fedha kwa sasa ni contractionary.

Kinachofanywa na Mh Raisi ni kubadilisha matumizi ya fedha iliokwisha pangwa, na sio kuzuia matumizi yake. Kwahiyo mzunguko wa fedha kwa maana ya currency in circulation wala haijapungua.

Ili kutambua utekelezaji wa sera ya fedha nchini unapaswa kutazama actions za Banki Kuu kwenye masoko ya fedha na sio matendo ya wanasiasa. Isitoshe mfumuko wa bei unaotokana na kuwepo kwa hela nyingi kwenye mzunguko yaani core inflation tayari umekuwa chini sana kwenye wastani wa asilimia 2.5 kwa mwaka, kwahiyo serikali haina tija wala motive ya kutekeleza contractionary monetary policy kwa sasa. Kwa kufanya hivo, itapelekea kudumaza uchumi wetu.
 
Mkuu monetary policy iwe katika expansionary condition au contractionary condition haina uhusiano kabisa na kodi wala matumizi ya serikali.
Yes, nakubaliana na wewe, mtoa mada anaelekea kuchanganya monetary policies na fiscal policies.

Maswala ya matumizi ya serikali na kodi zake yanaangukia kwenya fiscal policies. Ndio maana nimesema hapo kwenye post yangu kwamba ili kujua utekelezaji wa sera ya fedha ni vizuri kuitazama Benki Kuu.

Ingawa kunawakati serikali inaweza kutekeleza fiscal policies zinazolenga kusuport monetary policy nchini.
 
Huyu Mkurupukaji Mkuu ndio anataka kuigeuza nchi yetu kuwa ni lab ya majaribio ya sera za zimamoto na ukurupukaji! Yaani Magufuli anajiona kama yuko pale UDSM Lab ya idara ya Chemia anachanganya madawa kwenye CH 101! Hii haiwezekani kabisa tutarudi nyuma miaka 10!
Nahisi hii nadharia inatekelezeka kwenye vitabu na siyo kihalisia!
hiyo sio leo wala kesho. btw, hiyo ni nadharia tu. nadharia nyingi za uchumi (ikiwemo hiyo) hazifanyi kazi kwa muda mfupi
Nyie watanzania watatu ni weupe kabisa alooooo
 
Huyu Mkurupukaji Mkuu ndio anataka kuigeuza nchi yetu kuwa ni lab ya majaribio ya sera za zimamoto na ukurupukaji! Yaani Magufuli anajiona kama yuko pale UDSM Lab ya idara ya Chemia anachanganya madawa kwenye CH 101! Hii haiwezekani kabisa tutarudi nyuma miaka 10!
leta hoja kuonesha kwanini tutarudi nyuma miaka 10 siyo ngonjera. Hili ni jukwaa la Gt
 
Kujaribu kutumia nadharia za kiuchumi kuelezea suala hili ni upotoshaji. Ikumbukwe wakati wa kampeni mwaka jana Magufuli aliahidi mambo kadhaa, kubwa likiwa kutoa elimu ya msingi na sekondari bure kuanzia Jan, 2016. Januari hii ni katikati ya mwaka wa fedha 2015/16 hivyo hakuna bajeti mpya kwa ajili ya haya matumizi mapya. Alichofanya JPM ni kupunguza matumizi kwenye maeneo ambayo siyo muhimu kwake kisiasa kama safari za nje, warsha, sherehe, chai ya maofisini, semina n.k. na fedha inayookolewa iende kwenye haya matumizi mapya. Hii pia imeenda sambamba na kujitahidi kuongeza makusanyo ya kodi pamoja na kwamba hajabuni vyanzo vipya vya mapato. Hivyo hapa hakuna kubana matumizi worthy of the name; simple and clear!
 
actually heading yako imekosewa tayari na content pia, Magufuli hana mkono kwenye Monetary Policy. Monetary Policy inafanywa na Banki Kuu labda uniambie ameathiri kwenye fiscal policy ambayo inahusisha gvt. spending and gvt. revenue (Tax)
 
Niliwahi kusema kwamba ili kuondoa umasikini inabidi somo la uchumi lianze kufundishwa form one.ili tuongeze vijana wengi wenye uelewa na uchumi.

Kwa uzoefuwangu mada kama hizi hapa Jf watu wanapitaga tu.
 
actually heading yako imekosewa tayari na content pia, Magufuli hana mkono kwenye Monetary Policy. Monetary Policy inafanywa na Banki Kuu labda uniambie ameathiri kwenye fiscal policy ambayo inahusisha gvt. spending and gvt. revenue (Tax)
1.What is the difference between monetary policy and fiscal policy
 
1.What is the difference between monetary policy and fiscal policy
Monetary policy kwa lugha yetu inamaana ni sera ya fedha, kwa maana ya matendo ya banki kuu katika kuongeza au kupunguza ujazi wa fedha au money supply.

Kwahiyo hii sera ya fedha inaweza kuwa contractionary pale ambapo benki kuu ina nia ya dhati ya kupunguza ujazi wa fedha sokoni, ili kuleta uwiano katika uhitaji wa fedha na shughuli za uzalishaji.

Kwakuwa sote tunaju kwamba kma fedha zitakuwa nyingi zaidi ya shughuli za uchumi basi hii husababisha kuwepo kwa mfumuko wa bei au inflation.

Sasa kinyume cha contrationary monetary policy ndio tunaona expansionary monetary policy, ambapo hapa sasa banki kuu inakuwa na nia ya kuongeza fedha kwenye uchumi kwa makusudi kabisa.

Ilihali, fiscal policies hizi sera za mapato na matumizi kwa serikali kuu. Ambazo zinaweza pia kulenga matumizi ya serikali kwenye uchumi ikiwa ni pamoja na matumizi ya kimaendeleo au development expenditures, lakini pia sera za ukusanyaji wa kodi nchin.
 
Yaani wewe umekopi ukabandika theory hapa. Bahati mbaya umeshindwa kulinganisha na hali halisi ya mazingira yetu. Nchi zetu developing countries zipo immune na hizi theories kwa sababu Mfumo wetu haueleweki. Lakini Magufuli hajapunguza pesa kwenye mzunguko bali amefanya value for money. Yaani anataka pesa zitumike ipasavyo kwa kuondoa rushwa.
Nakubaliana na wewe, Dogo anakarii, economic growth inhuishwa na vitu vingi sana. sio tu kubana matumizi. basi kama kubana matumizi ndio every thing katika ukuaji wa uchumi kila nchi ingefanya hivyo na zote ziwe sawa kimaendeleo.
 
hii ni sera nzuri ambayo inapunguza pesa nyingi kwenye uchumi ambazo hazikuwa na manufaa.hii imechangia mfumuko wa bei uliopo saivi.

MANUFAA YA CONTRACTIONARY NI;
1. Kupanda kwa thamani ya shilingi kwasababu mzunguko wa pesa unakuwa mdogo
2. Kushuka kwa bei za bidhaa kwasababu kwa sababu mzunguko wa hela ni mdogo kuliko bidhaa ( money circulation becomes low than commodities available in the economy)
3. Usawa wa kipato kwa watu, kwasababu hela zikipungua kwenye uchumi manunuzi ya bidhaa yanakuwa affordable kwa watu wote. anachotumia tajiri na mwenye kipato kidogo anaweza kukipata.
NOTE;
Ukichukua mfano kwenye mzani wa usawa ( lorenz curve) ambapo kadri muachano unavyokuwa mkubwa kutoka line ya usawa ndivyo utofauti wa kipato unavyokua mkubwa na kinyume chake ni sawa.
Hapo sasa ndio umesema nini?Ulisoma posti yako kabla ya kutuma?
 
Kama hizo ndizo maana za fiscal and monetary policies basi sioni tatizo la heading ya hii mada,maybe a very tiny technical error but contextually was on point. Nasema hivyo kwasababu benki kuu haiwezi tu kuamua kama iingize kiasi kikubwa cha pesa au ipunguze kiasi kikubwa cha pesa ktk uchumi,benki kuu hulazimika tu kufanya hivyo kufuatia matakwa ya kisera ya kiuchumi ya serikali husika.Kwa mfano utawala wa King kikwete ulikazia zaidi ktk kukuza micro economy, hii ina maana pesa nyingi sana zilikuwa zinahitajika ktk uchumi.So both monitory and fiscal policies are influenced by the government, the central bank simply follows the orders from the government.
Monetary policy kwa lugha yetu inamaana ni sera ya fedha, kwa maana ya matendo ya banki kuu katika kuongeza au kupunguza ujazi wa fedha au money supply.

Kwahiyo hii sera ya fedha inaweza kuwa contractionary pale ambapo benki kuu ina nia ya dhati ya kupunguza ujazi wa fedha sokoni, ili kuleta uwiano katika uhitaji wa fedha na shughuli za uzalishaji.

Kwakuwa sote tunaju kwamba kma fedha zitakuwa nyingi zaidi ya shughuli za uchumi basi hii husababisha kuwepo kwa mfumuko wa bei au inflation.

Sasa kinyume cha contrationary monetary policy ndio tunaona expansionary monetary policy, ambapo hapa sasa banki kuu inakuwa na nia ya kuongeza fedha kwenye uchumi kwa makusudi kabisa.

Ilihali, fiscal policies hizi sera za mapato na matumizi kwa serikali kuu. Ambazo zinaweza pia kulenga matumizi ya serikali kwenye uchumi ikiwa ni pamoja na matumizi ya kimaendeleo au development expenditures, lakini pia sera za ukusanyaji wa kodi nchin.
 
Nyie watanzania watatu ni weupe kabisa alooooo
subiri uone kama kuna litakalotokea zaidi ya shilingi kuimarika, tena itaimarika kwa shida kwa kuwa mnategemea imports. wacha kukariri vitabu. kawaulize wachumi wa ulimwengu; how long are short-run, long-run periods?
 
Back
Top Bottom