DaudiAiko
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 362
- 302
Wanabodi,
Tofauti na muonekano wa wengi, nina dhubutu kusema kwamba miradi ya kimkakati ya serikali, ina mchango mdogo sana kwenye kukuza uchumi wa nchi na kuleta maendeleo ya kudumu. Sio jambo ngeni Kwa nchi ya Tanzania kuhusishwa na umasikini duniani na kwasababu hiyo ni vyema kwa jambo hili kupata suluhu. Miradi inayofanywa na serikali ya sasa inaweza kuonekana ya tija sana lakini Kwa sababu nitakazo elezea, utagundua kwamba miradi hii ni ya kawaida sana. Madarasa ya wanafunzi, vituo vya afya, Barabara, miradi ya maji, n.k. inatatua changamoto zinazotokana na umasikini lakini haitupi mwanga wowote wala kutatua changamoto ya jinsi ya kututoa kwenye umasikini huo.
Kabla sija nyooshewa kidole na kushikwa shati, nitauliza Swali. Je Tanzania ya dunia ya Kwanza ipo na aina ipi ya miradi itatuwezesha kufikia malengo haya?. Shughuli za kutuletea maendeleo ya kudumu na kutimiza ndoto ya kuwa nchi ya dunia ya Kwanza zitahitaji serikali yenye udhubutu na ambayo inaweza kuwa entrepreneurial. Mradi wa ATCL ambao haujafanikiwa bado, SGR ambayo itawezesha nchi za jirani kutumia bandari ya Dar Es Salaam, kampuni ya TTCL ni mifano michache ya miradi yenye tija ambayo inaweza kuleta maendeleo ya kudumu na kubadilisha maisha ya watanzania. Tofauti na mifano niliotoa, miradi mingi ya maendeleo nchini ni short-term na hailengi kukuza uchumi wa nchi in the long run.
Nchi zilizoendelea zimeweza kukamata masoko ya bidhaa na huduma mbalimbali duniani na kuzitumia kama njia ya kujiingizia Kipato ngeni na kukuza uchumi wao. Mfano, ligi ya Uingereza inaingiza kipato cha paundi bilioni 7.6 serikali ya Uingereza kila mwaka, Kipato cha kampuni ya Microsoft mwaka 2024 tu ni Dola za kimarekani bilioni 245. Makampuni kama Mitsubishi, Toyota na Sony yaliyopo Japan, Hyundai na Samsung yaliyopo Korea Kusini. Nchi zilizoendelea hazijaendelea kiuchumi tu ila ni viongozi katika tafiti zinazoleta bidhaa na huduma mpya. Kwa mara nyingi pia, zimeweza kubuni teknolojia mbalimbali ambazo zimegusa maisha ya mamilioni ya watu walio sehemu tofauti duniani.
Ni vyema kuwa na malengo ya siku moja kuwa nchi ya dunia ya Kwanza na kwasababu hiyo hatutakiwi kutegemea mapato kutoka Kwenye kodi tu. Serikali ya Tanzania inaweza kuwa muwekezaji mkubwa kwenye sekta binafsi na kuchochea ubunifu wa teknolojia, bidhaa na huduma mbalimbali. Ubunifu huu ukitumiwa katika kukamata masoko ya bidhaa na huduma mbalimbali hapa nchini na hata nje ya nchi basi makampuni ya kitanzania yatafanya vizuri kwenye masoko haya. Serikali inaweza kuanzisha makampuni au kuwekeza kwenye makampuni mbalimbali ya kitanzania yanayo onyesha potential ya kuwa makampuni makubwa. Tuelewe kwamba uwezo wa kuongeza kipato na kukua kiuchumi unategemea sana jinsi ambavyo makampuni makubwa ya kitanzania yanavyofanya katika masoko ya dunia. Haya ndiyo maendeleo ya kweli na miradi ya kimkakati itakayo tufikisha pahali.
Tusidanganywe na tunachokiona kwenye runinga au kwenye mitandao ya jamii. Serikali hii bado haijaonyesha dira ya Tanzania ya miaka kumi au ishirini ijayo. Kodi za wananchi zinazotumika kila mwaka kufanya shughuli za kila siku bila kuwa na mipango mingine zimeifanya serikali hii kuwa serikali ya "Business as usual". Mpaka ifikie hatua ambayo serikali inachukua risks tutabaki pale pale