Connection walizopewa wageni.. Ndio zinazoitesa Tanganyika

Connection walizopewa wageni.. Ndio zinazoitesa Tanganyika

Hii ni pesa wanayojitolea kwa hiyari, si kodi inayokatwa na kuliwa na wajanja wachache. Kila anayeamini hiyo tonetone ni upigaji ana hiyari ya kutochanga.
Unaruhusiwa kufanya kampeni kwa umma ili watu wasichange.
Ni jukumu langu kuwatoa watu upumbavuni na uzwazwani......Kwakweli manyumbu ni mazwazwa
 
Nauleta mjadala huu unaogusa kiini cha unyonyaji na usaliti wa kiuchumi hapa Tanganyika, ambapo rasilimali za umma zimegeuzwa kuwa mali ya watu wachache na washirika wao wa kigeni.
Nitachambua yale ya msingi.. Mtanisaidia mengine

1. Ufisadi na Connection za Kiwaki
Mifumo ya kiuchumi imetekwa na mtandao wa kifisadi unaowapa wageni upendeleo wa wazi kupitia mikataba ya siri na ya kinyonyaji.

Ufisadi huu mkubwa unafanywa na viongozi wasio na uzalendo, ambao wanapokea rushwa nono na asilimia za hisa za siri (kickbacks) ili kupitisha sheria zinazolinda maslahi ya makampuni ya kigeni. Matokeo yake, wazawa wanabaki kuwa watazamaji maskini kwenye nchi yao, huku mabilioni ya fedha yakitoroshwa kwenda nje ya nchi kila uchao.

2. Utamaduni wa Kula kwa Urefu wa Kamba
Msemo wa "kula kwa urefu wa kamba yako" umetumika vibaya kama leseni ya kuhalalisha wizi wa mali ya umma na ubadhirifu wa kodi za wananchi. Viongozi na maafisa wa serikali waliopewa dhamana ya kulinda rasilimali wamejilimbikizia mamlaka makubwa, wakila hadi kamba yenyewe na kuacha mifuko ya nchi ikiwa mitupu.

Mtindo huu wa maisha ya kifahari ya viongozi unagharimiwa na umaskini wa Watanzania wa kawaida, ambao wananyimwa huduma bora za afya, elimu, na miundombinu.

3. Kupitia Upya Mikataba na Kukata Kamba
Ili kujinasua kwenye mtego huu, Tanganyika lazima ifanye mageuzi makubwa kwa kupitia upya na kuvunja mikataba yote ya kifisadi katika sekta za kimkakati kama madini, bandari, na nishati.
Ni lazima kuwepo na sheria kali za uwazi zinazomfanya kila kiongozi anayesaini mkataba mbovu kuwajibishwa kibinafsi na kufungwa jela. Kukata kamba hizi za kifisadi kutazuia wageni kupata upendeleo wa kipekee na kurudisha umiliki wa rasilimali mikononi mwa umma.

4. Kufunga Mianya ya Upigaji Serikalini

Ni lazima kuimarisha taasisi za udhibiti na uchunguzi (kama TAKUKURU na Ofisi ya CAG) kwa kuzipa meno na uhuru kamili wa kuwakamata na kuwashtaki "mafisadi papa" bila kuingiliwa kisiasa.

Upigaji wa fedha za umma kupitia manunuzi ya serikali, safari za nje hewa, na miradi ya kitapeli unapaswa kudhibitiwa kwa mifumo ya kidijitali isiyoruhusu mianya ya rushwa. Viongozi wote lazima walazimike kutangaza mali zao hadharani, na mali zinazopatikana kwa njia za kifisadi zitaifishwe mara moja.

5. Kujenga Uchumi na Mitaji ya Wazawa
Nchi haiwezi kuendelea ikiwa sekta zote kubwa zinamilikiwa na wageni; ni lazima serikali iwekeze kwa makusudi kukuza mitaji na uwezo wa wajasiriamali wa ndani.
Kupitia benki za maendeleo za kizalendo, wazawa wapewe mikopo ya riba nafuu na upendeleo wa kisheria wa kuendesha biashara kuu nchini.
Hii itabadilisha mfumo uliopo, ili badala ya wageni kupewa "connection," wazawa ndio wawe wamiliki wakuu wa uchumi wa Tanganyika.

6. Katiba Mpya na Uzalendo wa Kweli
Mwisho, mabadiliko ya kweli yanahitaji Katiba Mpya itakayopunguza madaraka makubwa ya viongozi na kuweka mifumo imara ya uwajibikaji inayomilikiwa na wananchi.
Elimu ya uzalendo lazima irejeshwe ili kujenga kizazi kipya cha viongozi wanaochukia rushwa na wanaoweka maslahi ya taifa mbele ya matumbo yao.
Ni kupitia mapinduzi haya ya kisheria na kifikra pekee ndipo Tanganyika itakapoacha kuwatajirisha wageni na kuanza kuwanufaisha wananchi wake

Mungu Ibariki Tanganyika💖View attachment 3634351
Msipoipigania Nchi yenu kwa maneno, na silaha tegemeeni kufanywa watumwa mara kumi zaidi ya sasa.

Bandari, mbuga, Tanzanite, gas, carbon, maji, madini tofauti yote, makaa ya mawe na kila kitu vimeuzwa, vimeporwa.

Hakuna bilionea atakubali kufilisika. Atapigania Mali zenu kwa damu, hongo, ushirikina, kuwagawa nk.
 
7. Kufisadi tOne tOne zinazokusanywa kutoka kwa maskini wa Hali ya chini kabisa.
Tonetone inayokusanywa kwa mwaka ni pesa ya siku moja tu ya fisadi mmoja tu anayovuna kwa makusanyo ya pesa ya mafuta.

Usijifanye hujui Nchi inavyodhulumiwa. Hao tone tone hata waruhusiwe kukusanya kila siku, hawafikii hata % 0.00005 ya ufisadi wa mapapa nguli wanaopora billions of money
 
Mada za namna hii siku hizi nasoma kichwa cha mada tu basi, na kuondoka na maumivu yangu moyoni.

Haya nayo yatapita, au ndio basi tena tumegeuzwa kuwa watwana wa wengine milele?
 
Mada za namna hii siku hizi nasoma kichwa cha mada tu basi, na kuondoka na maumivu yangu moyoni.

Haya nayo yatapita, au ndio basi tena tumegeuzwa kuwa watwana wa wengine milele?
Hatutakuwa watwana milele lakini tutapitia vipindi vya kutisha sana
 
Tonetone inayokusanywa kwa mwaka ni pesa ya siku moja tu ya fisadi mmoja tu anayovuna kwa makusanyo ya pesa ya mafuta.

Usijifanye hujui Nchi inavyodhulumiwa. Hao tone tone hata waruhusiwe kukusanya kila siku, hawafikii hata % 0.00005 ya ufisadi wa mapapa nguli wanaopora billions of money
Sijawahi kuona watu wenye akili finyu kama chawa na kunguni wa chama cha majambazi.. Halafu ndio mabingwa wa kumiliki ma ID 1000
 
Tatizo huwa hamueleweki mnataka. Alikuwepo JPM alijaribu kupambana na hayo mnayoyasema mkamuita dictator na majina mabaya yote mnayoyajua, kitu ambacho kiliwashushia heshima sana. Kifupi ni kwamba JPM aliungana na wananchi dhidi ya uhalifu wowote wa kiuchumi nanyi mliunguna na wahalifu dhidi ya JPM na wananchi na huo ndio ukweli, mliacha misingi yenu mliyoijenga kwa muda mrefu. Leo kiongozi yeyote wa Chadema akikemea ufisadi wananchi wanajua hamaanishi.
 
JPM alijiharibia mwenyewe kwa kuanzisha mauaji ya wapinzani kwa siri au wazi bila kujali ni watumishi wa Serikali, wanasiasa, wasanii nk.

Lwajabe, Lissu, Sanane, nk.

Nilimpenda toka moyoni JPM, ila kitendo cha kufanya maendeleo kwa damu za watu, hakihusiani na ushujaa wowote. Ni ukichaa tu wa madaraka. Tanzania Kiongozi ana mamlaka makubwa mno. Hahitaji kuua ili atawale.

Angetulia kama Mwinyi kule Zanzibar, akafanya miradi na maendeleo bila kuwadhuru watu, na maisha yakasonga.
 
Hatutakuwa watwana milele lakini tutapitia vipindi vya kutisha sana
Mifano ipo 'live', mkuu 'Mshana Jr'. Haita unadhani watatoka lini kwenye hali yao, karibu karne na ushee baada ya uhuru wao!
Lakini nilishangaa juzi kuwakuta wakishiriki kwenye kombe la dunia la FIFA.
 
Mifano ipo 'live', mkuu 'Mshana Jr'. Haita unadhani watatoka lini kwenye hali yao, karibu karne na ushee baada ya uhuru wao!
Lakini nilishangaa juzi kuwakuta wakishiriki kwenye kombe la dunia la FIFA.
Tuombe sana Mungu apindue meza. La sivyo...!
 
Back
Top Bottom