Congo's M23 rebels end rebellion, say ready to disarm

Congo's M23 rebels end rebellion, say ready to disarm

Yaani wewe lolote unaloambiwa na Zitto ni habari JF? You're boring
 
hii habari iko bbc sasa sijui kama ulikua una haja ya kusema umesikia kwa zito? ina maana wewe huwez amin kitu mapak uckie kwa zito?

Mimi niliiona post ya Zitto Facebook kwa hiyo nika mquote yeye. Shida iko wapi kama taarifa ni ya kweli?
 
Ngoma ya watoto haikeshi! M23 waliambiwa wasichezee koki wataloa wenyewe wamechezea,sasa yamewakuta. Unaambiwa sasa hivi 'kila wanachoambiwa' wanasema sawa!
 
According to Zitto Kabwe, MP, waasi wa M23 wamesalimu amri huko nchini Kongo. Kama ni kweli nitow pongezi kwa makanda wetu wa JWTZ, wameipa heshima nchi na wametendea haki makamanda wenzao walio uawa.
Hii taarifa ya M23 kusalimu amri nimeiona BBC unaweza kuingia kwenye mtandao wao ukaipata kwa urefu.
 
Wanaomchukia dogo zitto kwanini wasijitundike kwenye tawi la mpapai?
 
130913125600_m23_congo_304x171_afp_nocredit.jpg

Waasi wa M23 katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wametangaza kumaliza uasi wao ndani ya nchi hiyo muda mfupi baada ya kupigwa katika ngome yao ya mwisho na majeshi ya serikali ya Congo yakishirikiana na kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa kilichopewa uwezo wa kupigana na waasi hao.

Katika taarifa walioitoa waasi hao wamesema badala ya kufanya uasi sasa wataendesha harakati zao kutumia njia ya kisiasa.

Muda mfupi uliopita Kiongozi wa waasi hao Bertrand Bisimwa ametangaza kuwaamuru mkuu wa wapiganaji wa M23 na makamanda wa vikosi vyote muhimu wa kundi hilo kuwaandaa wapiganaji wao kusalimisha silaha, kutawanyika kuondoka katika eneo la mapigano na kukubaliana na matakwa yatakayowekwa na serikali ya Congo

Awali Msemaji wa Serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Lambert Mende aliambia BBC kuwa majeshi ya nchi yameishambulia ngome ya mwisho ya waasi na wamekimbia na wengine huenda wakawa wamejisalimisha.

Majeshi ya serikali ya Kongo yakishirikana na kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa kilichopewa uwezo wa kupambana na waasi hao walianza mapambano dhidi ya M23 Octoba mwaka huu na kufanikiwa kuwaondoa katika eneo la Bunagana kwenye mpaka wa Uganda ambayo ni ngome yao muhimu.

Source: BBC Swahili
 
Jipeni Moyo ila Kwa Wanaojua Theories za Propaganda Watawaelewa Hao M23 Na Wakifanyacho Sasa ni Re Organizing na Watarudi Kwa Jina Lingine na Renegade Mpya. Kwa Wale Wazoefu wa Masuala Ya Intelligence ( Espionage ) Watanielewa na Mimi Najua Walichokifanya hapo Ni Kuwazuga tu na Kubadilisha Upepo ambapo Sasa Shughuli Imehamia Kwa Uganda ambao Nao Kwa Sasa Wanaingia Mzigoni na DRC ili Kuwapumzisha Rwanda Kwa Kipindi Fulani na Pia Kuwasahaulisheni Kuhusu Kagame na Watarudi baadae Kidogo Wakiwa na Nguvu Mpya na Tactics Mpya Kabisa. Kwa Sasa Shughuli Anaachiwa Baba Museveni Mtoto wa Marehemu Mama Esteeri Kokundeka na Marehemu Baba Amos Kaguta na Msiojua Kijana Wenu Joseph Kabila ila Kwa hapa Dar Tulioishi Nae Tulikuwa Tunamwita na Kumfahamu Sana Kwa Jina la KABANGE na Alikuwa Akipenda Sana Kutumia Gari la Rambourgine Nadhani Watoto wa Oysterbay Mitaa Ya Haile Selasie Mtakuwa Mnamkumbuka na Marehemu Baba Yake wa Kipropaganda Mzee Laurent Desire Kabila Alikuwa Anajulikana Mno Kwa Jina La Mzee Mwale! Dogo Ni Mtutsi Pure na Anacheza tu Dili na Wazee Wake wa Uganda na Rwanda na Jina Lake Halisi ni ADRIEN HYPOLYTE CHRISTOPHER KANAMBE. Nimemaliza na Kazi Kwenu Mimi Simo..............!
 
usifanye mchezo na TPDF, hiyo ni habari nyingine hapana chezea wao kabisa
 
Nawewe umeweka propaganda japo huyo mtoto nakiri unamfahamu na mission yake.
na walomuweka pale ni Kagame+M7 japo alilelewa tz..na siyo mtoto wa kabila baba bandia + jina bandia
 
Nashukuru Kwa Kunielewa na Huyo Mtoto Amewakaribisheni Kulinda Amani Kwake ili Ajue Mbinu Zetu na Hadi Silaha Zetu Kisha Anawataarifu Baba Zake KK's na Sisi huku Anatutia Ndimu tu Tanzania na Tunabaki tu Kujisifu humu Kijinga na Kipumbavu Kuwa JWTZ Limewashinda M23 ilhali Majeshi Ya MONUSCO Yanaundwa na Nchi Tatu tu South Africa tena Ambao Ndiyo Wana Askari Wengi Kisha Malawi na Sisi Tanzania ambao tuna Batch ndogo Mno Ya Askari Wetu Huko Ambao Wanafika Sasa 800. Tuache Sifa za Kijinga na Kujisifu Kwani Rwanda, Uganda na Sasa Kenya Wanatudharau Mno na Sishangai Tumetengwa ktk COALITION OF THE WILLING na Kwa UMBUMBUMBU WETU Tumetumia Jazba na Hasira Kutaka Kujiunga na DRC na Burundi ambapo DRC bado Kuna Vita na Human Rights Abuse Nyingi tu Huku Burundi ikiwa bado Politically Unstable na Bado Wana Lile Kundi la Hatari La INTARAHAMWE! Hii Ni AKILI au MATOPE? Kwa Kitendo tu cha Kuanzisha New Grade System Ya Kuwa na DIVISION FIVE Kwanini Akina TRIPLE K's Wasitudharau Kwa Kuanzia Kwa Mjomba na Kumtenga na Hadi Sisi akina PANGU PAKAVU? Tunajisifia huku Wenzetu Wakipiga Hatua in Social Economical Development! Bravo Kaguta, Kagame na Kenyata and Well Done K Wa Msoga na Magogoni.
 
The end of the M23 would send an intimidating message to the other groups, raising hopes of an end to two decades of conflict, BBC Africa security correspondent Moses Rono says.
Chezea JWTZ ww....wakianza tu kwa sasa muziki wake mpaka kigari....heeeeheee wapi mukamasimba na koba...
 
Jamani naomba kufundishwa Jwtz ni Watanzania wenzetu lakini Mbona marazote wanapopewa majukumu wanafanya kwa uhakika?Lakin Watz haohao ktk sekta nyingine hasa kusimamia rasilimali za taifa Hali tete?!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom