Congo Rebellion: Clinton Defends Kagame


Kwahiyo Kagame kushauriwa mkutanoni na Kikwete haifai, ila Kikwete kushauriwa na Slaa hadharani inafaa?

Slaa is a total disappointment...
 

wewe ndio una uongo wa kipuuzi hasa, na wala wewe na Slaa wako hamjui kuwa JAKAYA KIKWETE alishakaa na Utawala wa Rwanda na Burundi huko Arusha 05/April/1994 akiwa Waziri wa Mambo ya Nje
Kagame akiwa Msituni akiandaliwa na Utawala wa Clinton kuitawala Rwanda na RPF yake saa 2.21 usiku wakamtungua Habyarimana.
Sasa Jk kweli atakuwa na busara tena wakae Meza moja waelezane nini tena wakati kisa kizima kilivyoanza na mpaka wanagoma kupatana wao km ndugu (INTARAHAMWE na BANYAMULENGE) anakijua.
JK yupo sahihi kabisa 'Ndugu wagombanapo warudi wakapatane kwani bila ya hivyo hawatakaa wapatane mpaka mwisho
At 8:21 p.m., around Kigali airport, the pilot Habyarimana, a French, radioed the control tower received permission to land. But during the descent from the runway, took off two missiles from Masaka Hill to the presidential plane. Nobody on board survived.
President Habyarimana was forced to go to Dar-Es-Salaam on 6 April 1994, for a meeting infamous He never returned home.
So, what happened that day? On 6 April 1994, Bill Clinton ordered the Pentagon to send 450 U.S. rangers in Burundi to assist CIA in Rwanda to execute the assassination smoothly. That day, in the morning, Madeleine Albright, Clinton’s Ambassador to the UN, ordered General Roméo Dallaire (Canada) who was in Rwanda as commander of the UN forces, facilitate the RPF and the CIA to travel to Akagera National Park, with UN vehicles to monitor the return of Tanzania Habyarimana’s plane in the evening, and alert the team to Terrorist Masaka Hill to prepare for the explosion in flight. The same day, President Yoweri Museveni has received the order for Clinton to make sure that the Habyarimana back to Kigali to be done at night. A 20H 01 ‘, the spies detected the CIAs Habyarimana’s plane above the Akagera National Park, immediately warned headquarters in Mulindi Kagame and called U.S
 
Mkuu si wana JF wamekwisha spill beans kwanini Clinton anakujakuja kwa Mh.Kagame, hebu jaribu kuangalia sura ya Clinton hivi unaweza kuamini kwamba jamaa huyu anaweza kuwa mkatili kiasi kile, nilisema hapa kwamba Clinton is a formidable ACTOR - sasa hivi anatafuta njia ya kujinasua hasihusishwe na operation ya kuhangusha ndege ya Habyalimana na kuua abiria wote na marubani, Dunia ilikuwa inamlahumu PK wakati hakuhusika moja kwa moja, PK yuko clever and shrewed hatakubali kubambakizwa kesi ambazo hazimuhusu moja kwa moja, wakimlazimisha atataja kila mmoja aliye husika - PK hatakubali kuwa kafara ndio maana nchi za magharibi huwa hazitaki kuzungumzia suala hilo kiundani. Clinton kama ana mpago wa kununua nyumba hiyo itakuwa ni mbinu za kutaka kuziba watu mdomo wasiseme wanacho kijua. Unaposema Clinton anamshangaa JK eti kwa kuwa hajui historia ya Rwanda! Nani ambaye anataka kujua historia ya mauaji ambayo Clinton Mwenyewe na Serikali yake aliyo kuwa anaongoza wakati huo ndio walihusika moja kwa moja na majanga yaliyo kuja kuikumba Rwanda! Baada ya kusoma taarifa hizi sitataka tena kumuona Clinton Maishani mwangu.
 

Mkuu ulichoandika ni kweli kabisa. Hii information inapatikana ndani ya secret document entitled "BILL CLINTON BEHIND THE PRECONCEIVED PLOT IN THE RWANDAN GENOCIDE". Walio na paper hiyo ni watu nyeti! Ziara ya Clinton nchini Rwanda lengo ni kukutana na Kagame ili kujadili namna ya kujinasua kwa kile kinachoelekea kuwakuta huko The Hague. Time will tell!
 
Clinton has been working in Rwanda for long time now,what u need to hear from him.he has NGO there called chai which has been paid a lot of dollas from donors.although who knows if they benefit from congo minerals.its not a supprise to hear that from him or Tony Blair.
 
MUNGU ni mkubwa iko siku wataumbuliwa hata wakificha namna gani kizazi kijacho kitaelezwa ukweli
Tupo pamoja Mkuu Beka Nurdin
 
Last edited by a moderator:
hata mimi nilishangaa sana jinsi watu wenye akili fupi walivyokuwa wakiandika kiushabiki kwenye vyombo vya kinyarwanda eti slaa amamuunga mkono kagame, wanashindwa hata kutofautisha sisa za ndani na mambo ya nje!
Mkuu, wakati mwingine ni vyema Kiongozi wa Siasa/Chama kuwa makini kwa kuangalia upepo wa siasa wa wakati huo unavuma kuelekea upande gani kabla hujatoa a political statement/comment more-so kama maisha ya kiongozi mwenzako yanatishiwa na nchi jirani. Mkuu, kitendo cha media za Rwanda kusifia/kufurahishwa na kauli za Dk. Slaa ni ushahidi tosha kwamba alifanya vitu vya ndio sivyo!! Tunaweza kuwa na tofauti zetu za kitikadi as a NATION lakini linapo kuja suala la Usalama wa Taifa letu na Viongozi wake tunapashwa kuhungana na kuwa kitu kimoja - mbona kuna window of opportunities nyingi tu za kumzidi kete mshindani wako kisiasa, lakini siyo hili linalo husu usalama wa TAIFA letu, hapo tukubaliane kwamba jamaa alinoa step kwa bahati mbaya nafikili - no wonder Rwandese are rejoicing kutokana na kauli za Dk.Slaa, wenyewe hawawezi kutofautisha siasa za ndani na mambo ya nje na wala siamini kama Dk.Slaa hakujua kwamba kauli yake inaweza kuwa-quoted na media za nchi za nje.
 
Lol,vipi na hawa European wanaosema Rwanda is not a problem but part of the solution nao ni actors or what part of conspiracy hapa unatueleza leo
European partners bury hatchet


Both Sweden and Netherlands last year suspended aid to Rwanda, citing allegations that government supports M23 rebels in eastern DR Congo.


When asked whether the financial grants represented a shift in their position, both Sweden and Netherlands representatives acknowledged that Rwanda "is not the problem but part of the solution in DR Congo."



"We have a good relationship with Rwanda and our development cooperation has continued through this year. What happened was that some disbursements were temporarily frozen in response to serious allegations from the UN Group of experts," Maria Håkansson, the chargé d'affaires at the Swedish Embassy in Kigali, said.


"Sweden is a small country multilaterally and the UN has always been a strong component of our foreign policy. In such a situation it was very difficult to ignore this kind of information… but obviously Rwanda is part of the solution in the region."


On his part, Pietre Dorst, the Netherlands Head of Cooperation, said that his country decided to work with Rwanda and other countries in the region to find stability and peace in the region.


"We will continue to work with Rwanda in order to find means to reduce poverty and realise Vision 2020 and have normal bilateral and mutual interests," Dorst said.
 
Mkuu KOBA, yaani sasa hivi sijui tuamini mhandishi gani tuache yupi mambo yanaonekana ni vurugu tupu! Jana kwa mfano kuna sehemu nilisoma mwandishi (tena wa Ulaya) anasema Mwami PK ana mipango ya kutungua ndege ya OBAMA i.e Airforce ONE, mkuu hapo nilishika kichwa! Jamani PK tunamsema mambo mengi lakini hili la kutungua ndege ya OBAMA naona ni uzushi uliopitiliza maelezo na aliye andika madahi hayo sijui alikuwa anafikilia kitu gani kichwani mwake!! Mh.Kagame atakuwa na sababu gani ya msingi ya kutaka kutungua ndege ya Rais wa dunia? Je Mh.Kagame na family yake hawajipendi! Je, Mh.Kagame ana tekinolojia gani ya kutungua a such Impregnable flying Battle TANK. Tusipokuwa makini kila mtu atahibuka na taarifa nyingine za kuchonga TU kwamba jana PK alifanikiwa kusafiri kwa Hypersonic vehicle kwenda kwenye MARS na kurudi duniani with half HOUR!
 
Waswede nawakubali sana hawana papala katika kutekeleza majukumu yao, vile vile wana kawaida ya kufanya upelelezi wao independently bila ya kutegemea sana taarifa za nchi nyingine i.e third party.
 
Clinton anajisafisha tu ... hana ubavu wa kusema chochote negative kuhusu PK kwa sababu .. genocide ilitokea wakati alipokuwa madarakani na alilaumiwa sana kwa kutochukua hatua yoyote. Hata Blair naye amejikuta kwenye mtego huo huo..
 
All I can say is that: Clinton has no idea that Kagame is a cold blooded killer and a terror in his country. It is HE who started genocide and is responsible for all the murders that occurred thereafter. Kagame should be brought to justice. 90% of Rwandese know that Kagame is a killer but they cannot talk against him as he made it against the law to talk about genocide. It is known, the one's in government who talk highly of him are scared but have no choice but to praise him so they can eat and support their families(some serious ass kissing there)...Kagame, You are a serial killer, everybody knows it by now and soon or later Clinton too will find out the truth about you. Don't be fooled, the world is waking up and remember, the truth always prevails no matter how you try to hide it by killing witnesses but one day, you'll be brought to justice. You are a killer. Africa does NOT deserve people like You and and Al Bashir of Sudan. You all should be hanged just like the people you have killed to hide evidence.
 

Kwa hili Dr.slaa alichemka sana,hakuusoma mchezo mapema,ndio maana huwa namsifu sana zito kabwe ana akili ya ziada
 
Aliyekuwa Rais wa Marekani Bill Clinton, hivi majuzi amemtetea Kagame kutokana na tuhuma zinazomkabili za kuwasaidia waasi wa M23 nchini DRC.

Kwa muda wa miezi takriban minne kumekuwa na maneno ya kejeli kutoka kwa Serikali ya Rwanda na kwa hakika maneno hayo yanatoka mdomoni mwa Rais Paul Kagame na maofisa wa ngazi za juu katika Serikali yake.

Kagame amekuwa mbogo baada ya Rais Jakaya Kikwete kumshauri afanye mazungumzo na wapiganaji wa Kihutu waliokimbilia Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) baada ya kutuhumiwa kufanya mauaji ya kimbari nchini mwake mwaka 1994.

Inakadiriwa kuwa Watutsi na Wahutu 800,000 wenye msimamo wa wastani waliuawa wakati huo, ingawa takwimu hizo zina utata, kwani wako wanaodai kuwa nchi hiyo wakati huo ilikuwa na idadi ndogo ya watu ambao idadi hiyo inasemekana ndio waliouawa.

Pia, wapo wale ambao wanaweza kushangaa kwa nini Kagame amekuwa hivyo na kuikosea heshima Tanzania, nchi ambayo imekuwa mstari wa mbele kupokea wakimbizi wake toka miaka ya 1960 na kwa nini Rais Kikwete alitoa ushauri huo.

Kagame hakupendezwa na ukweli huo kwani kila mara amekuwa akikataa kuwa hana mkono katika mapigano yanayoendeshwa na vikundi vya msituni vinavyoanzishwa nchini DRC kila inapotokea hali kutulia.

Kikwete amekuwa akijua jambo hili kwa muda mrefu kwani amekuwa Waziri wa Mambo ya Nje kwa kipindi cha miaka kumi na amekuwa akihudhuria mikutano ya kutafuta amani ya DRC bila mafanikio kwa sababu kila kikundi kinapoingizwa katika jeshi la DRC na kudai kuwa kimemaliza vita kinazuka kikundi kingine ambacho nacho kinaanzisha mapambano dhidi ya serikali.

Kofi Annan, Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa (UN) alikuwa mkuu wa shughuli za kijeshi za umoja huo kabla hajapanda cheo na kuwa katibu mkuu wa umoja huo, alipotembelea Rwanda baada ya kumalizika kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe, msafara wake ulirushiwa nyanya.

Hiyo ilikuwa ni kama kumpa ujumbe kuwa hakuna alichofanya wakati ule Watutsi walipouawa na Wahutu mwaka 1994.

Masikini! Annan angefanya nini wakati alipokuwa akiyaomba mataifa makubwa kuingilia kati ili kusitisha mauaji kila moja lilikuwa likiangalia maslahi yake na ulikuwepo mpango wa uchelewashaji wa makusudi.

Baadaye Annan alipokuwa akigombea Ukatibu Mkuu wa UN ni Rwanda pekee katika nchi za Afrika ndiyo iliyopinga na hata alipokuwa akiomba kuongezewa muda ni nchi hiyo iliyokuwa kinara wa kumpinga wakati ukweli ni kuwa mambo yote yaliyokuwa yakifanyika wakati huo Kagame alikuwa akiyajua.

Aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Rwanda, Meja Jenerali Kayumba Nyamwasa, alinukuliwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) akiwa uhamishoni Afrika Kusini akithibitisha kuwa vikundi vyote vimekuwa vikianzishwa na Kagame kwa nia ya kuhakikisha kuwa Wahutu na jeshi la zamani la nchi hiyo ambalo kwa sehemu kubwa linaundwa na waliokuwa vijana wa Inteharamwe hawapati muda wa kujijenga.


Kwa maneno mengine, Kagame ameifanya ardhi ya DRC kama uwanja wa mapambano kati yake na wapinzani wake ambao wako mashariki mwa nchi hiyo.

Jenerali Nyamwasa, ambaye kabla ya kukimbilia Afrika Kusini alikuwa Balozi wa Rwanda nchini India anasema kuwa Kagame ndiye aliyeamrisha kutunguliwa kwa ndege iliyokuwa imebeba ujumbe wa nchi hiyo pamoja na Rais Juvenal Habyarimana na Cyprian Ntyaramira wa Burundi ambao ulikuwa umetokea Tanzania kwenye mkutano wa kujadili amani ya nchi hiyo.

Baada ya vita kumalizika na hatimaye RPF kuchukua uongozi, Ufaransa, mtawala wa zamani wa Rwanda ilimtuhumu Kagame kwa kusababisha mauaji ya kimbari kwani Wahutu wasingianzisha chinja chinja ya Watutsi kwa wakati huo kwani mazungumzo yale yalikuwa yanaelekea ukingoni na hatua ya mwisho ingekuwa kwa RPF kuwa chama cha kisiasa ambacho kingeshiriki kwenye uchaguzi.

Nia ya Kagame ilikuwa ni kuchukua uongozi Rwanda kwa nguvu kwa sababu kwa mizania ya siasa za nchi hiyo ambazo zimejikita zaidi kwenye ukabila ingekuwa vigumu kwa Watutsi walio wachache kushinda.

Sababu ya pili ambayo ndiyo iliyowafanya RPF wakatae au watumie nguvu ilikuwa ni juhudi ya Marekani ambayo ilikuwa mfadhili mkuu wa RPF kuhakikisha kuwa ushawishi wa Ufaransa katika eneo la Maziwa Makuu unaondoshwa kwa gharama yoyote.

Hii inathibitishwa katika kitabu Global Intelligence; the world’s secret services today ambacho kimeandikwa na waliberali, Paul Todd na Jonathan Bloch.

Waandishi hao wanabainisha kuwa wakati huo kulikuwa na vita vya kijasusi baina ya Marekakani na Ufaransa ambavyo baadaye vilibadilika na kuwa ni vita vya kijeshi.

Kagame alikuwa Mkuu wa Idara ya Usalama wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda kabla ya kujiunga na RPF.

Ufaransa ikimsaidia Habyrimana na Marekani ikiwasaidia RPF ambao tayari walikuwa wakisaidiwa na Uganda walijipatia taarifa za kijasusi kutoka kwa Serikali ya Rwanda na wapiganaji wake.

Majasusi wa Marekani ambao walikuwa wakitumia njia za kijasusi za siri za kunasa taarifa za mawasiliano katika eneo la Afrika Mashariki walifanikisha mipango ya RPF katika uwanja wa mapambano.

Marekani ilikiri kuwa kuanzia 1994 ilikuwa ikiwasaidia RPF kwa kuwapatia silaha na Kagame alipewa simu ya satelaiti aina ya Motorola INMARSAT ambayo licha ya kufungwa kitaalam (encryption) ili mawasiliano yake yasinaswe na wapiganaji wa Serikali ya Rwanda au yeyote yule, kwa bahati mbaya shirika la Ujasusi la Kimataifa la Ufaransa, DGSE (Direction Generale de la Securite Exteriure) lilifanikiwa kunasa mawasiliano yale na Ufaransa iliituhumu Marekani kwa kutoa kombora lililoiangusha ndege iliyokuwa imembeba Rais Habyarimana.

Kwa maana nyingine, ni kuwa Kagame hawezi kukwepa mkono wa sheria wakati utakapofika kwani taarifa muhimu za namna mambo yalivyokuwa yakienda katika uwanja wa mapambano, mawasiliano yake yamehifadhiwa na taasisi hiyo ya kijasusi ya Ufaransa.


Waandishi hao wamebainisha kuwa kwa kuwa Rais Mobutu Seseseko wa Zaire (sasa DRC) alikuwa akimsaidia Jonas Savimbi ambaye Wamarekani walikuwa wameishamchoka na walimtaka aache vita ili utulivu urejee Angola, nao wavune madini na mafuta huko wakiwa na sababu ya kumwondoa Mobutu madarakani ili kukata mizizi ya usaidizi aliokuwa akiupata Savimbi, ambaye wakati huo alikuwa kiongozi wa UNITA, iliyokuwa ikipigana vita vya msituni dhidi ya Serikali ya Angola chini ya MPLA.

Sababu nyingine ilikuwa kwa Mobutu kuwasaidia Wahutu ambao walikuwa kipenzi cha Ufaransa ilibidi aondolewe ili kuhakikisha kuwa Wamarekani wanalishika na kulidhibiti eneo lote la Maziwa Makuu.

Ikumbukwe kuwa wakati huo Rais Bill Clinton ambaye hivi majuzi amemtetea Kagame kutokana na tuhuma zinazomkabili za kuwasaidia waasi wa M23 nchini DRC, ndiye aliyekuwamadarakani wakati huo na alifanya juhudi kubwa kuhakikisha kuwa shughuli za kijasusi zinaendeshwa katika mtindo ambao utakuwa na manufaa zaidi kiuchumi na siyo kisiasa kama ilivyokuwa wakati wa vita baridi.

DRC ilikuwa muhimu kwa majasusi wa Marekani, hasa kwa uzarishaji wa madini ya coltan ambayo hutumika kutengenezea simu za mkononi, madini hayo hayapo sehemu nyingine yoyote duniani zaidi ya DRC.

Clinton alihakikisha kuwa anafanya kila awezalo kuondoa ushawishi wa Ufaransa nchini Sudan kwa kuwataka viongozi wa SPLA wakati huo, Kanali John Garang na wengine wadai uhuru kamili na siyo utawala wa shirikisho kutoka Sudan ili mradi Ufaransa ikose mafuta yaliyokuwa yakichimbwa kutoka Sudan Kusini.

Waandishi hao wamebainisha kuwa Marekani ilitoa dola 100 milioni ili kumsaidia Laurent Kabila kuanzisha jeshi la watoto waliokuwa wakijulikana kama Kadogoo wakiwa na malengo ya kumwondoa Mobutu.

Kufikia mwaka 1997, Shirika la Kijasusi la Marekani (NSA) lilikuwa imejenga vituo vya kuendesha shughuli za kijasusi ili kunasa taarifa za mawasiliano kupitia simu, nukushi, redio katika sehemu mbalimbali za eneo la Maziwa Makuu kama vile, Fort Portal nchini Uganda, Kigali Rwanda na Kongo Brazaville.

Ufaransa ambayo ilikasirishwa na jinsi Marekani ilivyofanikisha kuwaondoa vibaraka wake katika DRC na Rwanda ilihakikisha kuwa inawaandaa wanajeshi ambao walimpindua Rais Pascal Lissouba wa Congo Brazaville ambaye alikuwa ni kipenzi cha Marekani.
 
Kagame ni mroho wa madaraka na mikono yake inanuka damu ya wanyarwanda
 
Namshauli pk asiwe msahaulifu tuu.akumbuke kuwa serikali ya usa na washirika wake hawana rafiki wala adui wa kudumu.
 
Mnaacha kujadili katiba mpya, mnajadili kagame...wabongo ni zero.
 
kagame sehemu ya mafunzo yake amepata marekani. hivi miwatu myeusi hatuwezi
kujifunza kujitegemea zaidi ya kuwa vibaraka?. ona sasa wamarekani wanamgeuka. kagame ni kibaraka wa mataifa makubwa, shame on him.
 
Kagame hata akifanya nini dunia ya leo huwezi kutawala kibabe tena mwisho wake unakuja tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…