Confusion ya Marafiki, Please help!

Yesu hakuwa rafiki watenda dhambi kwa muda mrefu zaidi ya kuwakaribisha ili wabadirike.
hii ni according to summary ya matukio ya Yesu kwenye Biblia au ulikuwa unajua miaka yote 30 aliyoishi duniani alikuwa anaambatana au kukutana na nani?
 
Ndo maana ukawa mdogo wangu, lol!
salama lakini? umepotea sana mdogo wangu
 
FP kwangu mimi na ona ni tofauti kabisa kwanza si kweli ukiwa na rafiki mwenye tabia fulani lazima na wewe huwe na tabia kama yake, kuna huwezekano mkubwa mtu akawa na tabia tofauti na marafiki zake, mimi binafsi nina marafiki wenye tabia tofauti na zangu lakini kinacho fanyika ni kurekebishana na kujaribu kupeana ushauri!

Hili la ndege wafananao huruka pamoja linaweza lika tumika sana kwa watu ambao hawaja panuka kifikra( watoto) na ndio maana tunaona wengi wao huigana tabia na ukiwakuta marafiki lazima tabia zina fanana kabisa lakini ni tofauti kwa watu wazima!

 
Last edited by a moderator:
Kumbe bado inaendelea........!

Hivi ni uchaguzi wa mtu kuwa na rafiki wa tabia fulani ? Au urafiki ndio unaongoza na tabia ya mtu sio muhimu?

Kwa mfano nina rafiki ambaye anapenda dhuluma ingawa siipendi tabia hiyo siwezi kumbadili japo nilijaribu, tena ukizingatia tofauti zetu za umri nimekwama. Anyway hilo nimelivumilia na nayatazama yale mengine mazuri.

Lakini nilicho na hakika ni kwamba siwezi kuwa na rafiki ambaye ni shoga (gay)........Hata kama tuna urafiki mkubwa lakini nikipata hakika ndivyo alivyo hapo ndipo utakapoishia.

Mtu anaweza kusema mshauri abadilike.........Sina ujuzi huo wa kuibadili tabia yake. Na kuna wengine wanasema haina tatizo kama wewe mwenyewe huzishiriki tabia hizo, Nawauliza wanaweza kuhimili kuwa na rafiki shoga na wakamvumilia?
 
Kiunguru huruka na kunguru!! Na kunguru mweupe haruki na kunguru mweusi!! Kunguru na mwewe hawaruki karibu!! Mara nyingi hata watu wazima wanakuwa influenced na watu wanaokaa sana nao karibu!!!! Wewe ukitaka subiri mumeo akutane na jamaa anayependa nyumba ndogo halafu wawe marafiki wa karibu!!! Mumeo atajeuka kuwa fundi wa vimada!! Amini usiamini ila habari ndiyo hiyo.
 
mimi pia naamini hivi, ila ndo tunasema mawazo yanatofautiana
 
hapo kwa font kubwa ngoja wakaka waje wajibu, lol!
ni vizuri kama unafahamu tabia mbaya ya rafiki yako ukajitahidi kumrekebisha, ila kama itashindikana na unaweza kuivumilia akiwa naye na haiingiliani na mambo yako, mi nadhani poa tu
 
akijitwalia nyumba ndogo nitaona kaamua tu kuwa na nyumba ndogo...
kwani huyo rafiki ndo kamlazimisha kuwa na hiyo nyumba ndogo?
 
Heshima mbele, mambo mengine baadaye. Back to the Topic. Jesus lived friendly life to all people including sinners
nilijaribu sana tusiingie kwenye huu upande ingawa mtu aliyenifanya niandike hii mada alikuwa anazungumzia kwenye mtazamo wa kidini.... mimi nikataka tuuangalie kwenye mtazamo wa maisha yetu ya kila siku kwa sababu ninazozijua mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…