Confusion ya Marafiki, Please help!

hivi kweli mtu anaweza kukulazimisha kuiga tabia zake ambazo huzipendi?
watu wengi wanaamini hivyo e.g. my friend drinks so I will also start drinking. ni tatizo la kutokuwa na msimamo/kutojitambua ambalo huwaponza wengi
 
Mie sikubaliani na hizo kauli....

"Ndege wenye wafananao huruka pamoja"

"Nioneshe rafiki zako nitakwambia tabia zako'

Nakataa kwa sababu hii, unnaweza jenga urafiki ili upate kitu fulani either biashara au kazi.

Mfano 1. Kuna watu wanaofanya research katika mazingira magumu kama katikati ya machangudoa na mateja. Ili kufanikisha kazi yako kitu cha kwanza unajenga urafiki ndipo utapata data za kutosha. Hii haimaanishi ukiwa na urafiki na watu kama hao utaiga tabia zao.

Mfano 2. Kuna watu wanaotafuta tender mbalimbali na ili kupata hizo tender hujenga urafiki na hao wanaozitoa tender hizo haijalishi wana tabia gani, ili mradi tu afanikishe adma yake.

Hivyo basi kuna urafiki mwingine huwa ni kwa kusudi maalumu. Nakuwa na rafiki huyu kwa sababu ninahitaji kitu.kutoka kwake na sio FRIENDS WITHOUT BENEFIT....
 
Exactly....
Wakati tunakua (bado tupo kwa wazazi) mdogo wangu (mdada) alikuwa na misimamo mikali sana. alikuwa na uwezo wa kukaa na baba na mama kuwaambia kwa nini hakubaliani na wanachokitaka yeye, anatoa hoja zake na mwisho wa siku anashinda. hayo ya kuangalia jamii itamfikiriaje hakuwa nayo kabisaaaaa!
nakumbuka siku moja kuna kitu kilitokea baba akasema hiki ngoja kwanza tujadiliane na fulani atuambie msimamo wake, maana baba na mama walikuwa na different views......
Ukiwa na misimamo yako unaheshimika bila mwenyewe kujijua......
 
Kwanza ni kujua hizo tabia ambazo wengine wanaziita mbaya ni zipi, Yawezekana mtu hampendi mtu akasema anatabia mbaya hivyo anataka na wewe usiongozane naye wakati wewe hujakwazika na hizo tabia zake.

Mimi naamini kuwa tabia ni mtu hasa unapokuwa mtu mzima kwa watoto kwa sababau wanajifunza then inategemea mzazi anataka mwanawe awe wa aina gani hapo anweza muepusha na vijiwe anavyoona havifai. but mtu mzima ni ngumu kuiga atakuwa ameamua kuwa hivyo, au alikuwa hivyo hakujionyesha mapema.
 
Je tukiangalia urafiki ambao haujaundwa kwa ajili ya benefit yoyote?
 
kwa mfano rafiki yako ni mwizi.... na wewe kweli unalijua hilo, lakini mna mambo mengi tu ambayo mnaendana kasoro hilo la wizi. Je na wewe utajiingiza kwenye wizi sababu rafiki yako ni mwizi?
 
"friends with benefits" means urafiki wenye 6x6.
sikuwa na maana hiyo....
ndo maana toka mwanzo nimezungumzia urafiki ambao sio wa kimapenzi.
benefits kama hizo za kupata data au tender na vitu kama hivyo
 
Hili suala la marafiki lina negative na positive...
Kwa maana ya kwamba unaweza kuwa na hao rafiki wenye tabia mbaya na wewe ndo ukawa mwokozi wao kuwa influence na kuwatoa huko.Pia unaweza ukawa wewe ndo umevutwa kwenye ubaya huo na ikala kwako.
Wanadamu tuna uwezo tofauti wa ku-adapt mazingira..Kwa hiyo inategemea nguvu yako ikoje na ipi ya kuwavuta watu waje kwako au wewe ndo unavutwa.Kila mtu anajua udhaifu wake.Hivyo ni busara kujipima mwenyewe na kuamua kuwa na rafiki huyo au laa.
 



Nakubaliana na ww kwa upande mmoja na pia nitofautiane na ww kwa upande mwingine, Hivy;-
- Kwanza hapo wife yako anaonekana ni mkubwa kwa huyo kijana pia kidigo ana pesa na hapo ndo heshima imekuwepo,
-Kwa upande mwingine sikubaliani na ww kwa mantiki hii, hasa bale mnakuwa rika moja na level moja ya kimaisha au kipato, ni vigumu sana kuwa na nguvu kubwa ya kumshawishi rafiki yako abadilike. mfano marafiki zako ni malaya, na katika mazingira yoyote yale wanaweza kumkubaliwa mwanaume, sasa hapo utawezaje kuwa karibu na kuongozana mara kwa mara ktk matukio na starehe mbali mbali? kwani stori zo kubwa zitabase huko, na pia utajisikiaje unapoona wanchukuliwa kirahisi na wanume mbele yako?
 
sikuwa na maana hiyo....
ndo maana toka mwanzo nimezungumzia urafiki ambao sio wa kimapenzi.
benefits kama hizo za kupata data au tender na vitu kama hivyo
true, i was just explaining maana ya msemo wa "friends with benefits".
 
kwa mfano rafiki yako ni mwizi.... na wewe kweli unalijua hilo, lakini mna mambo mengi tu ambayo mnaendana kasoro hilo la wizi. Je na wewe utajiingiza kwenye wizi sababu rafiki yako ni mwizi?

Si rahisi na mimi niwe mwizi, sana sana ntamkanya tu na ntamwambia akiwa na mimi uizi wake auweke kando. mfano mimi nilikuwa na rafiki yangu yuko too good tatizo tukienda maduka ya vipodozi ataiba hata wanja au lipshine ili mradi tu amedokoa na pesa anayoyakutosha si ya kuunga na akidokoa hakwambii mkitoka nje anakuonysha look!
 
hapo kwa RED ndo muhimu zaidi, kujitambua.....
kuna kakangu mmoja aliwahi kufungwa sababu rafiki zake ambao walifanya uhalifu sehemu fulani walikuja kukamatwa akiwa nao. Kiukweli kabisa yule kaka hakuwepo kabisa kwenye huo uhalifu sababu muda ambao wenzie walifanya huo uhalifu yeye alikuwa sehemu nyingine, na wengi walijua hiyo kitu. hakuweza kutoka kwenye huo mtego sababu alikuwa close sana na hao jamaa... na polisi kwa vile walikuwa wanawafwatilia kwa muda mrefu hawakuamini kuwa yeye hakuwepo kwenye tukio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…