Confessions of an Economic Hitman & Tanzania

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
Kuna watu humu wamekuwa wanaingangania niwape kuhusu DFID au shirika la maendeleo la Uingereza Tanzania. Well.. kuna mengi ya kusema na naweza kuwaambia kuwa DFID inatutia umasikini sana pale Tanzania na baadhi yenu mnalijua hili lakini nimeona bora tuanzie hapa. Mind you this content may be old but it still holds considerable importance. Nishakisoma hiki kitabu lakini kwa wale ambao hamja kisoma nashauri mtazame hii video.

Kutokana na event zinazoendelea Tanzania sasa hivi I wouldnt be surprised kuwa kuna watu wamekuwa held ransom na hawa jamaa










Part I
http://www.youtube.com/watch?v=yTbdnNgqfs8

Part II

http://www.youtube.com/watch?v=29GhXsx7-Rs






 
..game,

..dfid inahusika vipi?

..kuna any big project walio-help to get through ambayo inatuchosha hivi sasa?

..shusha data zaidi!
 
GT,

Swali zuri sana. Unajua wakati ule tunasamehewa madeni, mimi nilikua nauliza, what is behind that offer? Watu wengi sana niliona kwenye forum za kitanzania wakijisifia kufutiwa madeni.....Ukweli, hayo madeni kufutwa yana masharti yake. Yapi? Hapo sijui, lakini kila kitu kinachotokea Tanzania mmh. Watu hawasiani mikataba ovyo bila kuwa na economic hitmen.

Halafu mimi bado najiuliza, nini kimetokea tangu 1985 mpaka hapa tulipo. Watu waliokula chumvi either hawana data, hawataki kusema au hawajui.........

Hiyo Conf of Econ Hitman, one of the best book ever. Tatizo nchi za kiaafrika hazijaguswa/ongelewa katika kitabu.....baada ya miaka 10, kitatoka kingine kuhusu Africa.
 
Ukisoma hii story utapata kuona jinsi hao watu wanafanyakazi so its real. Muda unavyozidi kwenda China inaweka pressure kwa westerners nao wanareveal maovu, tusubiri tuone


A
 
Kwa amabo hawajaiona hiyo video nawashauri............waiangalie......its very interesting and educative on number of issues about our National Economy and Security na jinsi Mafisadi "Vijisenti" wanavyoshirikiana na mashirika makubwa ya Dunia
 
Kwa amabo hawajaiona hiyo video nawashauri............waiangalie......its very interesting and educative on number of issues about our National Economy and Security na jinsi Mafisadi "Vijisenti" wanavyoshirikiana na mashirika makubwa ya Dunia

Badala ya kutu-direct kuangalia hizo video, naomba discussion. Kama tuko na Kitabu cha Confession of an EHM basi naomba tuanze hiyo discussion.
Niliisoma kitabu hiki zamani lakini najaribu kuisoma upya alafu naomba tuanze mjadala.
BTW, mnaona mtanzania yupi anaweza akawa ni EHM na wale wa ughaibuni kuna mtu mnamwona anaelekea.
I think that hao EHM si wengi sana hapa kwetu au wamejificha vizuri.
Mtu ambaye nina uhakika ni EHM ni Andy Young, hapo hakuna ubishi. Mi yangu macho tu na hii Sullivan summit na akina Masters and AY! They are really 'hitting' us
 
Ogah,

Mimi niliyajua haya miaka 10 iliyopita...As a fact kuna vitabu vingi sana vimeandikwa kuhusiana na hali hii isipokuwa tulishindwa kuamini ama kufuatilia kwa sababu hakuna Ushahidi.. Na kibaya zaidi kati yetu kuna Manyapala kama hao kina The truth ambao ndio viongozi wenye elimu na imani za kufungiwa..
Tatizo kubwa la mtu mweusi ni madai ya Ushahidi!.. hapa tunashindwa kuelewa kwamba Ushahidi hauwezi kuwepo hadi siku wamekwisha kamata nguzo hizo za Kiuchumi na hatuna la kufanya Kisheria. Ukimwambia Mdanganyika mtu fulani ana Ukimwi basi ni lazima umwambie kesha muua nani?...laa sivyo utaitwa mwongo na watakukimbia. Hivi kujitahadhali na mtu huyo kuna kosa gani?..Je, kumwita mtu ana Ukimwi ni tusi maanake hawa wazungu kuitwa exploiter huonyesha kana kwamba tunawasingizia, tusi kubwa na halina ukweli...
Ni hulka ya Utumwa kutoamini maneno kama mababu zetu walivyopakiwa ktk meli wakipelekwa utumwani walidhani wanapelekwa peponi na kibaya zaidi hapakuwepo na Ushahidi kwani kila aliyechukuliwa hakurudi alikotoka!..
 
Ulaya nzima wana hoja tu kutunyonya, wanatujua vema kuwa sisi waafrica ni wachovu, leo utasikia wametusamehe madeni, kesho tumepewa msaada, ila cha msingi Waafrica tujiulize hebu hawa bwana zetu wakigoma kutusaidia itakueje? Ama siku wakisema wanataka watugeuze nyuma ndipo watusaidie tutakubali? Hebu sisi tuna akili kweli?
 

..yawezekana!

..ila,case iliyozungumziwa katika confessions ni tafauti ya kwetu huku! hebu tutazame barrick & co. and the price of gold currently!

..hiyo ni case moja! ipo mifano kadhaa ambayo unaweza iweka,ila,inatafautiana na kile kilichokuwa kinafanyika huko latin america and asia. nyakati zimetafautiana so hata modus operandi inawezakuwa tofauti!
 
Mwafrika kwa kukisia nje ya nguo zake hatujambo yaani kweli mnaamini hakuna dalili za vibaraka wa EHM Tanzania?..
Basi nasema tena kama nilivyosema miaka ya nyuma kule Bcstimes....Mkapa ni namba moja!
 
Basi nasema tena kama nilivyosema miaka ya nyuma kule Bcstimes....Mkapa ni namba moja!

..mkuu,

..tusichanganye mambo,unless tunataka ku-define ehm kwa case yetu inamaanisha mtu yupi.

..mkapa hana tafauti na suharto! ina maana nae suharto alikuwa ehm?
 
Inaelekea ukoloni umerudi; tena mawakala wao ni ndugu zetu wenyewe. Vita dhidi ya mafisadi itakuwa ngumu kuliko waasisi wa Taifa letu walivyomung'oa mkoloni.

Zamani tulifundishwa historia shule za Msingi (nadhani ilikuwa darasa la 7); wakieleza jinsi Sultani Mangungo wa Msovero alivyouza nchi yake kwa Carl Peters wa Ujerumani; kwa taarifa zenu wakati wa utawala wa 'Mr. Clean' syllabus ilibadilishwa na somo la historia likafutwa!

 

..nafikiri tunaongelea ehm as kwenye kitabu chenyewe,kama mjadala ulivyo-evolve post chache zilizopita.

..i'm on point!
 
Sultani Mangungo wa Msovero alivyouza nchi yake kwa Carl Peters wa Ujerumani; kwa taarifa zenu wakati wa utawala wa 'Mr. Clean' syllabus ilibadilishwa na somo la historia likafutwa!

..kwa ufupi,unasema tuna historia ya kuuza nchi!

..kweli ukitaka kujua umefikaje sehemu leo na kesho utaenda wapi,angalia ulikotoka;soma historia!
 
Dar si Lamu,

nafikiri tunaongelea ehm as kwenye kitabu chenyewe,kama mjadala ulivyo-evolve post chache zilizopita.

..i'm on point!
Hakuna mahala nimesema haupo on point!
Umesema nachanganya, nachochanganya ni kipi! nipe elimu mkuu..nipo kujifunza.
Kumbuka tu maneno ya Nyani Ngabu kabla hujafikia maamuzi yako.
 
Dar si Lamu,


Hakuna mahala nimesema haupo on point!
Umesema nachanganya, nachochanganya ni kipi! nipe elimu mkuu..nipo kujifunza.
Kumbuka tu maneno ya Nyani Ngabu kabla hujafikia maamuzi yako.

..usiwe na haraka;no hurry in africa!

..baada ya muda utaelewa ninachomaanisha. mi nshakuelewa tayari.

..tuendelee kukata issue!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…