Computer inaleta chenga pamoja na mawimbi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Computer inaleta chenga pamoja na mawimbi.

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Jumakidogo, Jan 23, 2012.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Jan 23, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hii mashine 'Computer desktop Dell' nilikuwa nimeituliza bila kuiwasha kwa miezi karibu mitatu sasa. Leo nimeiwasha naona Screen yake inaleta chenga na mawimbi ya kufa mtu. Naona picha inachezacheza kama inatingishwa. Wataalam wa JF Huduma ya kwanza tafadhali kwa wanaojua.
   
 2. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  hebu antena yake igeuzie mjini itashika tu.
   
 3. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #3
  Jan 23, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Wewe kweli haufai....
   
 4. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,812
  Likes Received: 2,584
  Trophy Points: 280
  Naona muda si mrefu yote itageuka kuwa bluu
   
 5. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,158
  Trophy Points: 280
  tupa nunua mpya.
   
 6. Mr.mzumbe

  Mr.mzumbe JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 803
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 60
  Ipige pige zitatoka zote!
   
 7. networker

  networker JF-Expert Member

  #7
  Jan 24, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  chek nyaya zake kama ziko connected vizuri
   
 8. IT Guru

  IT Guru JF-Expert Member

  #8
  Jan 24, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 616
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Angalia wire wa CPU to monitor kama mzima au umeunganisha vizuri na wire zingine pia.ikiwezekana jaribu hata kubadilisha hizo wires
   
 9. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #9
  Jan 24, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Situpi! Bora niweke iwe mzinga wa nyuki.
   
 10. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #10
  Jan 24, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,581
  Likes Received: 848
  Trophy Points: 280
  tafuta/azima monitor mahali ujaribu ili kugundua tatizo, inaweza kuwa monitor au vga card
   
 11. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #11
  Jan 24, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,158
  Trophy Points: 280
  Watanzania wanajulikana kwa kuweka makorokoro. Hivi vitu vina life span, ikifika, inakuwa ni hasara kujaribu kuvitengeneza ndio maana walioviunda huko juu wana dump kwetu huku, utakuta huo mtumba hauna wakala hapa wala hauna kutegenezeka. Na hata ukitengenezeka unakuwa "out dated" kompuuta ni dynamic. Wapelekee watu ulaji.

  Nnakuambia hivyo kwa kuwa yashanikuta na usifikiri nakudhihaki. Nakuomba soma hizi links, labda utanielewa:

  Life of a PC laptop - CNET Miscellaneous laptop discussions Forums

  What is the Average life of an Average Desktop computer? - CNET Desktops Forums
   
 12. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #12
  Jan 24, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,581
  Likes Received: 848
  Trophy Points: 280
  @ff - hata kama ni kutupa ni lazima ukumbuke hiyo ni desktop hivyo iko separated kati ya cpu na monitor. Ni vyema akajua tatizo upande lilipo na kama ni desktop tambua parts zake zinaweza kubadilishika na zipo madukani.. Pia tambua na hali ya kifedha ya watanzania bado ipo chini kwa hiyo swala la kutupa haliwezekani kwa jamii yote
   
 13. Vinci

  Vinci JF-Expert Member

  #13
  Jan 24, 2012
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 2,641
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  ha ha ha....Pole mkuu...odoa hofu hiyo PC iko vizuri sana bado. hiyo nadhani tatizo ni resolution iko juu sana na monitor haiwezi kuhimili hizo pixels, unaweza kufanya yafuatayo.
  1. zima hiyo computer washa kwenye safe mode, by pressing F8 ikiwa kwenye post screen, pindi tuu unapoiwasha, baada ya hapo unaweza kubadilisha screen resolution AU
  2. Tafuta display ingine jaribu kuifunga hapo uone kama itawaka vizuri
   
 14. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #14
  Jan 24, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Bado hatujafikia hatu ya wenzetu, ndo mana nikakwambia siitupi isipokuwa ntaitundika shamba ili nifanye mzinga. Nyuki wakiingia ntarina asali mama, kuliko kutupa jalalani.
   
 15. IT Guru

  IT Guru JF-Expert Member

  #15
  Jan 24, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 616
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  sasa mkuu badala utoe feedback ulipofikia we unabaki kubishana tu?
   
 16. Reserved

  Reserved Content Manager Staff Member

  #16
  Jan 24, 2012
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 750
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  FF nio hapo sasa vigezo vyako vya upigamaruku vinaonekana ni vya kisiasa. gari inaweza kutumika kwa miaka mitatu ikawa Mileage 20,000. Gari nyingine ikatumika mwaka mmoja ikawa na Mileage 80,000.
  Ndio Maana jibu lako la kutupa sio zuri sababu hujamuuliza muhusika kompyuta yake ni model gani. ili japo ujue ni ya mwaka gani. Na hata kama kama ingekuwa ina zaidi ya miaka mitano bado kutupa sio suluisho kwnaza mpaka bila kujiridhsiah nini imeharibika.

  Unawezeza kusema kutupa kumbe inafaa kutolewa msaada kwenye chuo au college. So jibu la kutupa sio ptin ya kwanza kama unavyofanya wewe kwenye comment zangu sometime kwenye huu ukumbi

  Yaani comment na ushauri wako ni sawa na dakatari anakuja mgojnwa anakumbia kichwa kinamuuma . Theunamuandikia Dozi ya ARV za HIV bila kuchukua vipimo........lol
   
 17. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #17
  Jan 24, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,158
  Trophy Points: 280
  Lazima uwe na threshold, na threshold inayotumika kwa sasa kulipia ushuru wa magari ni uchakavu wake wa miaka na si wa kilomita ngapi. Hata wahasibu hutumia kigezo hicho.

  Huyo ataefanya hivyo si daktari, wala si mganga wa jadi. Nikisema huwa sikisii. Hiyo inatokana na vigezo vya sasa, hata gari ikiwa na kilomita 200 lakini ikiwa imevuka miaka 10 basi unalipia ushuru wa uchakavu. Mimi ushuru wa uchakavu usingekuwepo na mwisho kuiingiza ni miaka mitatu na exception ingekuwa kwenye antiques tu.

  Tena nataka nimuandikie kwa kirefu Mkulo aone ni vipi haya magari chakavu yanavyotutia hasara, mfano, Trucks za miaka 10 mpaka 20 nyuma ambazo ndio nyingi zilizopo barabarani, zinaletwa kama mitumba, zinatumia mafuta 10% - 40% zaidi ya trucks ambazo zinatengenezwa mwaka huu. Piga hesabu ya kutumia miaka 10 na gharama za spare na gharama za break down utakuta tunatumia zaidi kuya maintain magari chakavu kuliko mapya.
   
 18. zeus

  zeus JF-Expert Member

  #18
  Jan 24, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unakumbuka ni lini ulimuazima huyo rafiki yako kompyuta? i mean tarehe au muda?
  kama unakumbuka unaweza kufanya system restore---function ambayo inafuta mabadiliko (ina-reverse/rewind-undo) yaliyofanywa na rafiki yako. kwa hiyo kumbuka mara ya mwisho tarehe na au muda kabla hujampa rafiki yako kompyuta, then reverse mabadiliko hayo kwenye komputa yako hadi tarehe ambayo bado kompyuta ilikuwa mikononi mwako...kama hukumbuki, unaweza ku restore hadi siku moja kabla ya ile uliyopeana. sijui hiyo ni dell ya aina gani au unatumia OS gani ila fuata maelekezo hapa.

  Click Start-----Accessories-----System tools-----system restore

  Welcome to system restore----------------Restore to an earlier time------next------choose restoration point (siku kabala ya kuazimisha kompyuta)....kurudisha kompyuta katika hali ya awali

  link: How to restore Windows XP to a previous state
   
 19. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #19
  Jan 24, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Aisee nipo maeneo ya town, lakini nimenunua waya mwingine nataka nikatest nikirudi.
   
 20. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #20
  Jan 24, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hapana, sikumuazima mtu. Niliizima tu kawaida kisha sikuitumia tena kwa miezi mitatu sasa. Jana jioni nilipoiwasha ndo ikaleta matokeo hayo.
   
Loading...