Commander Kova - unalielewa hili kuhusu vituo vyako vya polisi?

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Jana jioni majira ya saa 2 usiku nilikuwa maeneo ya Ilala kumtembelea rafiki yangu mmoja aishie Mtaa wa Utete. Nikakuta hakuna umeme maeneo hayo – biula shaka kutokana na mgao.

Nilipita mtaa wa Pangani na nilishtuka sana nilipoikuta ile police station ya mtaa huo iko kwenye giza totororooo.

Hakuna hata mshumaa ulikuwa unawaka kutoka ndani. Hiyo ni station kubwa – siyo police post. Yaani hakuna hata jenereta?

Jamani hii si hatari hasa katika kipindi hiki cha wasiwasi hapa nchini? Wavamizi wangeweza kuvamia amory na kuondoka na silaha, askari wangewazuia vipi?

Aidha mtu aliyeumizwa vibaya atapataje fomu ya P3 kwenye giza. Ripoti zitaandikwaje kwenye RB gizani?

Jamani tunacheza na haya mambo. Komanda Kova – unalielewa hili? Au unakazania tu kutimiza amri za mahakama za kuwakamata viongozi wa upinzani?

Hebu fikiria scenario hii: Mtu anakwenda kuripoti majambazi yameonekana mahala fulani yanapanga njama zao. Akifika hapo wakati huo haoni kitu, ni giza tupu! Atajua ofisi gani ya kuingia? Au klwanza polisi wakaanunue mshumaa duka la jhirani? Halafu bila shaka gari iliyopo hapo itakuwa haina petroli!

Hii nchi imefikia hali mbaya sana – Kova na Chagonja wanachojua ni kupambana na upinzani kwa kutoa kauli za hovyo lakini masuala haya ya msingi ya kuboresha vituo vya polisi hawana kabisa habari nayo.

Ni aibu tupu kwa jeshi letu na kwa wakuu wanaloliongoza. Nyumba ya tatu kutoka kituo hicho cha polisi cha Pangani kulikuwapo jenereta inafanya kazi.

Yaani tuseme siku hizi wananchi wana hela kuliko serikali? Ndiyo matunda ya ufisadi?
 
Hawana pesa ya kupoteza kununua jenereta au mshumaa,

Pesa waliyonayo ni kwa ajili ya kukodisha ndege tu ya kumpeleka freeman mbowe arusha!!!
 
marksman kamanda kova anashughulikia shutuma za kumiliki malori,nafiki hawezi kukusikia,hali sio shwari kwake
 
Pesa nyingine kuwapa watu wa Tarime rambirambi baada ya kuua ndugu zao .
 
Mkuu mshumaa wa nini wakati vituo vya polisi kwa sasa ni vituo vya madili? Mi nkipita polisi karume,polisi pale kamata karibu na HQ ya tigo,oysterbay n.k utashangaa sana. Yani kuna askari zaidi ya 50 kila kituo wamekusanya viti vibovu vya plastic ,wamevifungafunga na kukalia wakigawana madili. Utasikia sijadaka leo! Apo anamaanisha ajapata dili siku iyo! Wana pikipiki utoka kwa zamu na kwenda kuwinda elf5 tano barabarani. Kwa kweli Tanzania polisi wetu ovyo,najua ni kutokana na viposho kiduchu na lack of planning kwa gvt.maana vituo vingine nje ya mji utakuta askari 3 na bunduki moja,aidha hamna hata risasi,au na risasi2 na virungu! Sasa eti wameleta polisi jamii,nani atatulipa polisi jamii wakati kazi tumewapa nyie?? Polisi wamegeukia madili!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom