Coming soon: Mpanda International Airport!

Coming soon: Mpanda International Airport!

aha! si hasa za kwetu.........akija waziri mkuu au presidaa toka Tabora......tutakuwa na project hiyo huko.........then akija toka IR .....tunahamishia huko..................akitoka Kagera ....................tunahamishia huko. Ni mwendo wa viporo vya miradi mpaka cycle ije tena ya PM au Presidaa atoke sehemu hiyo, then project inafufuka.

Ni kweli kabisa, hatufanyi mambo strategically, bali kwa ajili ya kuwaridhisha wakubwa. Huo uwanja hauna manufaa sawa na kuimarisha reli ya kati. Reli ya kati inaweza ikaleta mabadiliko makubwa kiuchumi maana itahudumia kanda ya ziwa, kigoma, tabora na mizigo ya landlocked countries kama Rwanda na Burundi.
Ndio maana inatarajiwa kujengwa bandari bagamoyo, chuo kikuu cha kilimo katavi (wakati graduates wa SUA serikali haiwatumii) na sasa uwanja wa kimataifa wa mpanda. Akija mwingine, atajenga barabara za juu na chini Kigoma, sio kwasababu ameona ya mbele, bali kwakuwa anataka kupendezesha kwao. Lazima tupangilie vipaumbele maana hatuna resources zakutosha.
Uwanja wa Kimataifa wa Mbeya uko wapi? Kwani ungemaliziwa usingetosha kuhudumia nyanda za juu kusini-ikiwemo Mpanda? Au wa Mbeya ukimaliziwa utampa sifa Mwandosya?Hatuwezi kujenga uwanja leo ambao utashindwa kujiendesha kwa faida kwa miaka 20 ijayo, wakati kuna vipaumbele vinavyoweza kulipa na kubadilisha uchumi wa nchi leo. Yaani watu wameanza kupanda nyasi Mpanda wakati wizara ya miundombinu haikutenga fedha kwa ajili ya reli ya kati, mpaka wamerudishwa na kamati? No wonder we are so poor!
 
Akili za kuigiza majina International airport !uwanja wa ndege ni muhimu lakini kwa kiwango gani? ndege ngapi zitatua kwa saa kama sio ndege mmoja ndogo kutua kwa mwezi,na ndege ya Raisi mara mmoja kwa mwaka ?Gharama za kuujenga na kuuendesha kimataifa zitatoka wapi?Acha kuchezea uchumi wa nchi,weka pesa za walipa kodi kwa yale yatakayosukuma maendeleo ya taifa letu mbele.
binafsi nashindwa kufahamu jinsi tunavyopanga vipaumbele jamani.. sielewi sielewei sielewi.. may be vipaumbele vinapangwa kulingana mkubwa anatoka wapi!! ni afadhali wangeweka resources na kukamilisha kwanza uwanja wa Mbeya na pia kuangalia strategic locations nyingine kama Mtwara, Kigoma, Bukoba na Mwanza.. jamani kama ukifika uwanja wa Mwanza utashangaa kabisa na kujiuliza maswali mengi bila majibu.. abiria na mizigo mingi lakini uwanja wenyewe hovyoooooo!! JAMANI SERIKALI JIFUNZE JINSI YA KUTENGENEZA VIPAUMBELE!!
 
Ati Mpanda International Airport! - wabongo kwa kamba hata hawawezekani...
 
huo utakuwa uwanja wa kutua bundi tu. kama kuna flight itatua hapo basi itakuwa ni zile za kusafirisha maliasili kwa magendo. au ni njia nyengine ya kupitishia mihadarati. Mpanda ijiandae kwa janga la vijana kuwa mateja.

Watasafirisha tembo, twiga na hippos toka Katavi! Pia watavutia watalii kwenda kuangalia Lyamba lya mfipa! Tehetehe!!!
 
Twende taratibu jamani, kwanza International Airport ni uwanja wa aina gani? Unatakiwa uwe wapi na je tulivyonavyo vime perform kiasi gani?

International Airport ni uwanja wa KIMATAIFA yaani kuna International arrivals & departures hivyo facilities zake zinatakiwa kuwa ina hadhi ya kimataifa. Lakini pia hizo departure na arrivals ni abiria ndo wanatakiwaa wawe wanasafiri na kuingia.

Abiria hawa ni pamoja na watalii, wafanyabiashara, dilpmats, wanasiasa etc. Hivyo lazima mji ambao International Airport unajengwa lazima kuwe na potentials. Ok inawezekana plan ya 2030 kila wilaya iwe na International Airport ila kwa kuzingatia hali ya kifedha ya nchi yetu this is not supposed to be of the priority. I can BET kama wakiendelea kuujenga basi utakuwa under utilized at 99% (WHITE ELEPHANT)

For your information KIA is underutilized for almost 80% kwani ndege inayo land pale ya kimataifa ni KLM, ETHIOPIAN, na kandege kengine kamenza hivi karibuni toka RSA. And gues what hizi ndege hazitui kila siku.

Hivi kuna businessman, mtalii, diplomat, celebrities ambao anataka kwenda Mpanda sasa HIVI?

USHAURI - Serikali waweke strategies za vivution Mpanda then ndio waangie kwenye miundo mbinu. AU HIZO HELA ZIONGEZWE KWENYE BAJETI YA MIUNDO MBINU THEN ZIPELEKWE TRL KWANZA WANA MPANDA WANGEFURAHI SANA.
Hizo ndege zenyewe zikowapi?
 
I wish you would have understood it better! I personally visited the place April 2011, ni kweli kuna uwanja mzuri wana wa ndege unajengwa kwa kiwango cha lami lakini ule uwanja haujengwi kwa bajeti ya Serikali wala pesa za walipa kodi. Ni shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa(UNHCR) linaujenga ili kurahisisha shughuli zake katika kanda hiyo ambayo imekuwa ikiwapokea na kuwahudumia wakimbizi kwa muda mrefu sasa.

There is no hidden ajenda and its not an international airport kama walivyoiita hapo juu! Its just a mere Air Strip!
 
hata pale Dom ,huwezi kuuita AIRPORT!Ni air strip!
 
hii serikali ya majuha,unajenga international airport sumbawanga wakati barabara za kawaida ni shida wiki iliyppita tu tbc walionyesha hukohuko namna ya watun wanavyosafiri kwa shida,leo mnajenga int airport,mbona ule wa mbeya usongwe unamiaka zaidi ya kumi hauishi?Acheni hizo bwana
 
Kwa taarifa yenu mpaka Senetor Arnold Schw... ana hotel/Campsite Katavi,zipo hotel/Campsite zaidi ya 4 hapo Katavi... na ndani ya hifadhi kuna viwanja vya ndege ndogo zaidi ya vi3 hivyo basi ili Ma-celebo wa ughaibuni waje moja kwa moja bila kupitia Dar/KIA/Mwanza...
Nina wasiwasi sana kama umejengwa na SIRIKALI yetu... Nchi ISHAUZWA HII...
 
Washukuru UNHCR bila ndege zao kutua pale sijui wangetua KUNGURU? Magamba vihiyo. Mkifika kwenye huo uwanja tu wote mtaanguka kwa shock, leo hii ni international?
 
I wish you would have understood it better! I personally visited the place April 2011, ni kweli kuna uwanja mzuri wana wa ndege unajengwa kwa kiwango cha lami lakini ule uwanja haujengwi kwa bajeti ya Serikali wala pesa za walipa kodi. Ni shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa(UNHCR) linaujenga ili kurahisisha shughuli zake katika kanda hiyo ambayo imekuwa ikiwapokea na kuwahudumia wakimbizi kwa muda mrefu sasa.

There is no hidden ajenda and its not an international airport kama walivyoiita hapo juu! Its just a mere Air Strip!

Mkuu hiyo ndiyo habari ya kweli. Ni kweli unajengwa na UNHCR kwa madhumuni uliyoyataja pia ni asante yao kwa upande huo kwa kuwatunza wakimbizi. Pia huo si uwanja wa Kimataifa kwa kuwa runway yake ni kama 1.3km na kwa standard yoyote uwanja wenye runway ya 1.3km hauwezi kuwa International Airport, unaweza ukawa International Airport kama tafasiri ya International Airport ni uwanja ambao zinatuwa ndege za kitalii kama Wilson Airport ya Nairobi. Kwa habari za kitaalumu nilizozipata ni kwamba pale inaweza kutua Boeng 737 kama ilivyokuwa ikitua Mtwara ama Mwanza na sijawahi kusikia Mtwara ama Mwanza vikiitwa International Airport! Kuuita uwanja wa Mpanda ati International Airport ni tetesi tu. Ila kilichonishangaza ni kwamba huo uwanja umejengwa 0.1km (zero point one km) toka ulipo mji wa mpanda wa sasa. Hapa naona itabidi mji wote wa mpanda uhame ili kuupisha uwanja vinginevyo ni hatari tupu.
 
Back
Top Bottom