MKEHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 716
- 1,144
Tumekuwa na story za siasa, burdani kwa takribani wiki sasa. Kuhama kwa Lowassa toka CHADEMA kurudi CCM na kifo cha kijana wetu Ruge Mtahaba, Mungu ampe pumziko la amani huko aliko.
Jana nimepita barabara ya Mbeya,Iringa,Morogoro mpaka Dar nikitokea Tunduma.
Nilikasirika sana na kuumia roho baada ya kuiona sehemu yetu pendwa Comfort Hotel pale mlima Kitonga ikiwa imebaki ni ruins. Kwa wale waliokuwa wakitumia barabara ya Nyanda za juu kusini wanajua jinsi pale Kitonga palivyokuwa kiburudisho na sehemu nzuri ya kukutana kwa wasafiri wa ndani ya nchi mpaka nje ya nchi.
Ilikuwa ni burdani tosha kwa wanafunzi waliokuwa wakisoma shule za ukanda ule kama vile Tosamaganga, Mkwawa, Iringa girls,Songea girls and boys, Kaigo,Kantalamba na nyingine nyingi.
Ilikuwa baada ya kurudi mabwenini stori zote ni kuhusu menu za Kitonga. Watu wengi tulipenda sana menu ya pale iwe nzuri au mbaya. Cha kushangaza ni kwamba sijaona sehemu nyingine nzuri za kula njiani . Nimeumia sana kuona hali ile pale Comfort Kitonga kwani pana historia nyingi kwa watu wengi.
Sent using Jamii Forums mobile app